Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Haram Toharifu ya Imam Ridha AS |
 |
21/03/2013 |
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni (Alkhamisi) ambayo ni siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kiirani wa 1392 Hijria Shamsia, ametoa hotuba muhimu sana mbele ya umati mkubwa wa maelfu ya wafanyaziara na watu wanaoishi jirani na Haram toharifu ya Imam Ali bin Musa Ridha AS waliokuwa wamekusanyika kwenye haram hiyo.
Sambamba na kutoa tathimini ya mafanikio na maendeleo ya kimsingi na makubwa liliyopata taifa la Iran katika mwaka uliopita wa 1391 Hijria Shamsia licha ya kuweko vizuizi vingi na vikubwa sana vya kivitendo na kipropaganda vya watu wanaolitakia mabaya taifa la Iran, ametolea ufafanuzi nukta kadhaa za kimsingi kuhusu mazungumzo na Marekani na pia masuala ya lazima na yanayohitajika katika hamasa ya kiuchumi na hususan wajibu wa kuacha kutegemea mafuta katika bajeti ya nchi na kuzipa mazingatio makubwa siasa kuu za kiuchumi pamoja na kuchukua hatua za kiwerevu kabla adui hajatekeleza njama zake.
Vile vile amezungumzia mambo ya lazima katika hamasa ya kisiasa na hasa hasa kushiriki vilivyo wananchi katika uchaguzi wa mwaka huu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, katika uchaguzi huo inabidi watu wa mitazamo na mawazo tofauti na wa mirengo mbali mbali ambao ni wafuasi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, washiriki kwenye uchaguzi huo na kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu na hima ya wananchi wa Iran kuweze kushuhudiwa uchaguzi wa kufana kwani uchaguzi wa Rais una athari kubwa katika masuala yote makuu ya nchi.
Ayatullah Udhma Sayyid Khamenei ameanza hotuba yake kwa kutoa mkono wa baraka kwa mara nyingine tena kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia na baadaye ametoa tathmini juu ya nukta chanya na nukta dhaifu zilizoshuhudiwa nchini Iran katika mwaka uliopita na kusisitiza kuwa ni jambo la dharura kuwa na mipangilio mizuri kwa kutegemea msingi wa tathmini hiyo kuu. Ameongeza kuwa: Kama ambavyo mtu anahitajika mara zote kutathmini na kuchunguza masuala yake ya kila siku, ni vivyo hivyo katika masuala ya nchi, kunahitajika tathmini na ukadirifu wa kitafa na hilo ni jambo muhimu sana kwani linatoa ibra na funzo na kuonesha njia ya kufuata katika masuala yaliyopo na yanayokuja.
Vile vile ameashiria jinsi mataifa, wasomi na watu muhimu wa nchi mbali mbali wanavyoangalia kwa kina kazi na mafanikio ya taifa la Iran ili waweze kupata somo na kigezo cha kufuata, na namna maadui wanavyoangalia kwa kina mafanikio ya taifa la Iran na baadhi ya wakati udhaifu unaojitokeza kwa taifa hilo na kusisitiza kwamba: Katika upande huo pia taifa la Iran linapaswa kuwa na mtazamo mkuu na unaokubaliana na uhakika wa mambo na vile vile liwe na tathmini sahihi kuhusu hali ilivyo nchini.
|
-6.821150
39.241447
Like this:
Like Loading...
Related
About Asadiq Media
Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq
Leave a comment
Comments 0