MAULANA SHEIKH JALALA KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA NCHINI IRAN

Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mudir mkuu wa Hawza Imam Sadiq- Kigogo, Dar es Salama  akiongoza ujumbe kutoka Tanzania akiwemo Sheikh wa BAKWATA, Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim na Kadhi mkuu wa Tanzania Sheikh Abdallah Mnyasi wanatarajiwa kuungana na Maulamaa wengine zaidi 500 wa Kiislamu kutoka nchi za kigeni jijini Tehran ambapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa kongamano la kimataifa la ‘Maulamaa na Mwamko wa Kiislamu’ ambalo litafanyika Tehran wiki hii.

Dk Velayati amesema, kongamano hilo litachunguza matatizo ya nchi za Kiislamu na vile vile changamoto zilizopo katika harakati za Mwamko wa Kiislamu. Aidha ameashiria njama za maadui za kuibua vita vya kimadhehebu nchini Syria na kusema maadui wameanzisha njama hizo baada ya kushindwa kuvunja muqawama nchini humo. Amesema maadui hao wa Uislamu watafeli katika njama zao za kuibua vita vya kimadhehebu nchini Syria. Velayati amesema, Iran inapinga harakati za Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu na kieneo dhidi ya Syria. Amesema Iran inazihesabu njama hizo dhidi ya Syria kuwa ni chuki na uadui dhidi ya Waislamu.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu amesema Waislamu na nchi za Kiislamu zinapaswa kuchukua tahadhari ili zisitumbukie katika mtego wa mifarakano ambao umewekwa na maadui.

Dkt. Ali Akbar Velayati ameyasema hayo mjini Tehran alipokutana na ujumbe wa wahadhiri wa vyuo vikuu na mawakili kutoka Misri. Ameongeza kuwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfumo wa demokrasia ya kidini na kwa hivyo wanaotaka kushiriki katika uchaguzi nchini huchunguzwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Dkt. Velayati ambaye ni mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema sababu muhimu ya kustawi Iran ni irada imara ya wananchi. Ameongeza kuwa kuhuisha thamani, utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu ni nukta muhimu zilizoimarisha Mapinduzi ya Kiislamu Iran na kuipa nguvu nchi hii. Dkt. Velayati ameelezea masikitiko yake kuwa baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati zina dhana potofu ya kwamba, kuwa uhusiano na madola ya kibebebru ndio dhamana ya kubakia tawala zao.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on April 29, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings