Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Akinamama wenye Vipawa

11/05/2013
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumamosi) ameonana na akinamama wenye vipaji na waamilifu katika sekta mbali mbali za Vyuo Vikuu, Hawza (Chuo Kikuu cha kidini), wanaharakati katika masuala ya familia na wanawake, watendaji katika taasisi za utumishi, waamilifu katika masuala ya Qur’ani, vyombo vya habari na asasi za kiraia, katika mkutano ambao umedumu kwa muda wa masaa mawili na nusu na ambao umefanyika katika wakati huu wa kukaribia kuingia kwenye mwezi mtukufu wa Rajab.
Katika mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu wa ulazima wa kutumiwa aidiolojia ya Kiislamu kuhusu mwanamke, tena kwa sura ya kushambulia aiodolojia nyingine na kujitangaza kwa mapana na kwa ufakhari katika nyuga za kimataifa na ameyataja masuala mawili ya “kutiwa nguvu misingi ya familia” na “kutukuzwa na kuheshimiwa mwanamke ndani ya familia” kuwa ni mahitaji mawili muhimu na ya dharura katika jamii na kuongeza kwamba: Wanawake wanaharakati na waamilifu katika kambi ya Mapinduzi ya Kiislamu wanapaswa kulinda uwepo wao katika medani ili waweze kuonekana kwa uwazi zaidi na kwa nguvu zaidi katika kuyalinda na kuyahami Mapinduzi ya Kiislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia jinsi Waislamu walivyo nyuma katika suala zima la kutangaza misingi ya kifikra ya Uislamu kuhusu mwanamke katika nyuga za kimataifa na kuongeza kuwa: Kuna kazi nzuri imefanyika kwa baraka za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa baraka za harakati ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) kuhusu suala la mwanamke lakini pamoja na hayo inabidi kazi kubwa zaidi ifanyike na inabidi kuundwe kambi ya mashambulizi na ya kuweza kujikinga na mashambulizi ya aidiolojia potofu.
Vile vile ameashiria jinsi ilivyo lazima kufanya kazi kwa bidii kubwa na kutolegeza kamba hata kidogo katika suala zima la kuleta mwamko katika upande wa wanawake na kuongeza kuwa: Kwa nini na licha ya kuweko aidiolojia ya kimantiki kabisa na ya kukinaisha kabisa ya Kiislamu kuhusu mwanamke, lakini bado Waislamu wanakuwa wanachukua msimamo wa woga na uliojaa wasiwasi mbele ya aidiolojia ya Magharibi?
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja aidiolojia ya Magharibi kuhusu mwanamke kuwa ni aidiolojia ya kisiasa na inayoendeshwa kwa malengo na mipango maalumu na kuongeza kuwa: Ijapokuwa hivi sasa aidiolojia na fikra hiyo inaonekana kama vile iko juu kabisa lakini ukweli wa mambo ni kuwa aidiolojia ya Magharibi kuhusu mwanamke inaporomoka kwa kasi kubwa na inazidi kusambaratika.
Ayatullah Udhma Khamenei ametaja masuala ambayo yanaifanya aidiolojia ya Magharibi kuhusu mwanamke izidi kuporomoka na kusambaratika kuwa ni pamoja na kitendo cha aidiolojia hiyo cha kubadilisha maumbile na kumpa sura ya kiume mwanamke na vile vile kumfanya kuwa kitu cha kujistareheshea mwanamme. Amesisitiza kwa kusema, hiyo ndiyo misingi mikuu ya aidiolojia ya Magharibi kuhusu mwanamke.
Amesema, wanachotaka Wamagharibi ni kuona kuwa hata zile kazi ambazo kutokana na udhati wake wa kifikra na nguvu za kimwili zinawafaa zaidi wanaume, zifanywe pia na wanawake na wanadai kuwa eti huko ndiko kulinda haki za wanawake.
Amesisitiza kuwa, kushiriki wanawake katika kazi mbali mbali na kuchukua nyadhifa za utendaji si jambo baya lakini kilicho kibaya na ambacho ni muendelezo wa fikra ile ile ya Magharibi ni kule kujivunia kuwa na idadi kubwa kupindukia ya wanawake katika maeneo ya kazi na nyadhifa za utendaji.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefafanua zaidi akisema: Si sahihi hata kidogo kuwa na fikra kwamba inabidi tuone fakhari na kujivunia kwa kuwa na wanawake wengi katika nyadhifa za utendaji, na kwa kweli kuwa na fikra hiyo kunatokana na misimamo ya pupa, ya woga na isiyo ya kimantiki mbele ya fikra ya Magharibi kuhusu mwanamke.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Kitu ambacho inabidi tujifakharishe nacho ni kuwa na idadi kubwa ya wanawake wasomi, wenye fikra pana na wanaharakati wa kiutamaduni na kisiasa na wanajihadi.
Vile vile ameashiria jinsi Uislamu unavyowapa haki sawa mwanamke na mwanamme katika upande wa kibinaadamu na kuongeza kuwa: Ingawan kwa mujibu wa Uislamu, mwanamke na mwanamme kila mmoja ana sifa zake maalumu za kimaumbile zinazotofautiana na mwanzake, lakini jinsia hizi mbili za mwanadamu hazina tofauti hata chembe katika upande wa ubinaadamu na masuala ya kijamii pamoja na matukufu ya kimaanawi na katika juhudi za kuelekea kwenye daraja za juu za umaanawi na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, mtazamo sahihi kuhusiana na mwanamke ni kumwacha mwanamke abakie katika maumbile yake ya kike aliyoumbwa na Mola wake na kukuza mambo matukufu na yenye thamani kubwa ndani yake bila ya kumbadilisha jinsia yake na kumfanya mwanamme.
Ayatullah Udhma Khamenei pia amesema, mtazamo kuwa mwanamke ni chombo na ni kama bidhaa ya kushibisha na kustarehesha matamanio ya kijinsia ya wanaume kwa kweli ni moja ya mabalaa makubwa na kuongeza kuwa: Hivi sasa baadhi ya wasomi na wataalamu wa Magharibi nao wameanza kuona hatari ya jambo hilo kwani wanajua wazi kuwa, mambo machafu kama vile kuenea ndoa za watu wa jinsia moja yatausambaratisha kabisa utamaduni wa Magharibi.
Vile vile amesisitiza juu ya ulazima wa kuwa macho katika jamii mbele ya vishawishi vya kijinsia kwa wanaume na wanawake na kuongeza kuwa: Tab’an katika nchi yetu suala la kuchunga vazi la stara la Hijab limetusaidia na kutulinda lakini bado hatujafika kunakotakiwa na Uislamu na inabidi juhudi kubwa zaidi zifanyike katika kulipa nafasi yake vazi la staha la Hijabu na lipewe hima kubwa pia suala la kuchungwa mipaka ya maingiliano baina wanaume na wanawake.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa: Si sahihi hata kidogo kuchukua misimamo ya pupa, ya woga na ya kujitetea mbele ya fikra na aidiolojia ya Magharibi kuhusu mwanamke bali inabidi fikra na aidiolojia ya Kiislamu kuhusu mwanamke itolewa kwa sura ya kushambulia fikra potofu za Magharibi na kujitangaza kwa ufakhari mkubwa duniani.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Si sahihi pia kuogopeshwa kivyovyote vile na vitisho vya Wamagharibi.
Vile vile amesema kuwa, moja ya sifa kuu za aidiolojia na mtazamo wa Uislamu kuhusu mwanamke ni kumpa mwanamke heshima yake, kujali maumbile yake ya kike na kumuweka katika nafasi yake aliyowekwa na Muumba wake.
Amesisitiza kuwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiumba jinsia ya kike kwa namna ambayo baadhi ya mambo yanayohitajia upole, malezi na hata usimamiaji wa nyumba hayawezi kusimamiwa na kuendeshwa na mtu mwingine yoyote isipokuwa mwanamke tu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea na hotuba yake hiyo akisema: “Kutiwa nguvu na kuimarisha jengo la familia” na “kutukuzwa na kupewa heshima yao wanawake katika familia” ni masuala mawili muhimu na yanayotakiwa kwa haraka sana katika jamii na kusisitiza kuwa: Inabidi katika sheria na katika ada, mila na desturi za watu kuandaliwe mazingira kwa namna ambayo mwanamke asiweze kudhulumika kwenye matabaka yote ya maingiliano ya kila siku ya watu katika jamii na asidhulumiwe pia kijinsia, kifikra na katika familia.
Ayatullah Udhma Khamenei amefafanua zaidi jambo hilo akisema: Inabidi siku zote watu wa familia wamwangalie mwanamke kwa jicho la kumuheshimu na kumuenzi na inabidi anga ya familia iwe kwa namna ambayo watoto siku zote watakuwa wanawapenda na kuwaheshimu sana mama zao.
Ameongeza kuwa, iwapo utamaduni wa kuwaheshimu wanawake utaimarika, basi bila ya shaka matatizo mengine mengi katika jamii na hasa matatizo waliyo nayo wanawake kama vile kudhulumiwa kwenye jamii, yatatatuka.
Vile vile amezungumzia suala la ndoa, mavazi, maingiliano ya kila siku ya watu, misaada ya kifedha na ya kisheria kwa wanawake pamoja na suala lao la kufanya kazi maofisini na nje ya familia na mipaka yake na kuhimiza kupewa hima kubwa mambo hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia kazi nyingi mbali mbali na za kila namna zilizofanyika kuhusu akinamama nchini Iran na halafu ametoa pendekezo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Inabidi juhudi zifanyike kuhakikisha kuwa kazi hizo za akinamama zinakuwa na mahusiano ya pamoja na ziweze kuchukua mkondo sahihi wa uhandisi wa watu wote na kuundwe chombo na kituo kikuu na cha kudumu chenye watu madhubuti na wenye mitazamo mikubwa na ya mbali kwa ajili ya kulifanikisha jambo hilo.
Amesema, chini ya chombo hicho kunaweza kuweko taasisi na vyombo mbalimbali na kunaweza kuweko pia benki yenye nguvu ya taarifa kuhusu kazi zinazofanyika.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile amewakumbusha nukta moja akinamama wote wanaofanya harakati katika kambi ya kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria jinsi wanawake walivyokuwa mstari wa mbele na walivyotoa mchango mkubwa katika kuundika Mapinduzi ya Kiislamu na kwenye hatua mbali mbali yalizopitia mapinduzi hayo baada ya kupata ushindi na kuongeza kuwa: Wanawake wanaharakati, waamilifu, wasomi, waandishi na wanafikra walioko kwenye kambi ya kuyalinda na kuyahami Mapinduzi ya Kiislamu wanapaswa wajitokeze kwa uwazi zaidi katika medani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile ameashiria nafasi ya Shirika la Redio na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB katika kutoa kiigizo na ruwaza sahihi kuhusu mwanamke muumini, mwanaharakati, mwanajihadi na anayetunza vizuri vazi la staha la Hijab na kuongeza kuwa: Shirika la Redio na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu linapaswa litoe mchango wake kwa asilimia mia moja katika jambo hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Shirika la Redio na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB linapaswa litumikie kikamilifu fikra ya Kiislamu kuhusu mwanamke na liwatangazie walimwengu sifa halisi na sahihi za mwanamke wa Kiislamu.
Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Sisi katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tumepata maendeleo katika suala la mwanamke lakini maendeleo hayo hayajafikia kiwango kinachokusudiwa na dini yetu tukufu ya Kiislamu hivyo juhudi kubwa zaidi zinahitajika katika uwanja huo.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Bi. Khaz Ali, Mkuu wa Baraza la Utamaduni na Masuala ya Jamii la Wanawake; Bi. Sefati, Mkuu wa Taasisi Kuu ya Ijtihad, Bi. Khadivi, Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Wanawake katika Mkoa wa Khorasan Razavi; Bi. Ayatullahi, Mhadhiri na Mtafiti wa Chuo Kikuu na Hawza ambaye pia ni mkuu na kiongozi wa kundi la wanawake katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran); Bi. Nazem Bakai, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha az Zahra katika masuala ya mazingira; Bi. Roh Afza, Mhadhiri wa Chuo Kikuu na Bi. Mojtahid Zade, Mkuu wa Taasisi ya Masuala na Wanawake na Familia katika Ofisi ya Rais wamezungumza na kutoa mitazamo yao mbali mbali kuhusu masuala tofauti yanayohusiana na wanawake na familia katika upeo wa ndani na wa kimataifa.
Mada zao zimelenga zaidi katika masuala yafuatayo:
– Udharura wa kutiliwa hima nafasi ya familia na kuimarishwa taasisi hiyo kwa msingi wa mafundisho ya dini ya Kiislamu na Qur’ani Tukufu.
– Umuhimu wa taasisi na vyombo husika pamoja na vyombo vya habari kuzipa uzito wa hali ya juu siasa za ushajiishaji wa kuongeza idadi ya watu.
– Umuhimu wa kuangaliwa upya maandishi ya somo la Sayansi Jamii katika Vyuo Vikuu nchini na mambo yanayohusiana na masuala ya wanawake.
– Kuundwa Baraza Kuu la Fikihi la wanawake na timu ya wataalamu katika suala hilo.
– Kubuniwa kigezo cha kudumu cha utafiti wa masuala ya familia na vyombo vya kigezo hicho.
– Udharura wa kutiliwa hima vipengee mbali mbali vya masuala ya malezi ya watoto kwa kufuata mbinu za Kiislamu na mbali na misingi iliyowekwa na taasisi zisizo za kidini za haki za watoto.
– Kukosekana chombo kikuu kinachojumuisha masuala yote ya haki za watoto nchini.
– Ulazima wa kubuniwa na kuandaliwa majimui ya fikihi ya watoto na kuanzishwa somo la utafiti wa masuala ya watoto katika Vyuo vikuu.
– Umuhimu wa kupewa mazingatio maalumu suala la stara, hijabu na mavazi ya staha katika vipengee tofauti bila ya kuingizwa siasa katika jambo hilo
– Pendekezo la kupewa nafasi wanawake ya kuwemo kwenye Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
– Ulazima wa kuongezwa idadi ya Vyuo Vikuu maalumu vya wanawake.
– Ufafanuzi wa kielimu na kisheria wa hukmu zinazohusiana na wanawake katika upande wa mirathi, malezi na utunzaji wa familia katika taasisi na jumuiya za kimataifa.
– Na kutumiwa mitazamo na uwezo wa kiutendaji na kiushauri wa wanawake katika masuala ya akinamama kwenye taasisi tofauti nchini.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on May 12, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: