‘IRAN NDIO NCHI PEKEE DUNIANI INAYOTEKELEZA MAAMURISHO YA QUR’ANI

Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefungua rasmi Mashindano ya 30 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yanayofanyika Iran ambapo amesisitiza kuhusu utekelezwaji maamurisho ya Qur’ani Tukufu na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio nchi pekee duniani inayotekeleza maamurisho ya Qur’ani Tukufu.

Akizungumza Ijumaa alasiri hapa mjini Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammadi Golpaygani ametoa hotuba kuhusu umuhimu wa kutekeleza mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Jihad katika njia ya Allah SWT.

Katika hotuba yake ameashiria aya ya 24 ya Surat al Anfaal katika Qur’ani Tukufu inayosema: “Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” Amesema Allamah Majlisi na Fakhr Razi katika kuifasiri aya hii wameitaja kuwa inayobainisha Imani na Uislamu.

Sheikh Golpaygani amesema iwapo katika ulimwengu wa Kiislamu Jihadi katika njia ya Allah itahuishwa kwa maana yake halisi basi hali ya Waislamu itabadilika na kuboreka.

Ameongeza kuwa Qur’ani Tukufu imeharamisha ribaa lakini kutokana na kuenea riba katika ulimwengu wa leo hali imekuwa mbaya sana na aghalabu ya watu wanakumbwa na njaa huku utajiri ukiwa katika mikono ya wachache. Amesema wakati Imamu wa zama, Imam Mahdi (Allah aharakishe kudhihiri kwake) atakaporejea, atairekebisha jamii kwa kutumia Qur’ani Tukufu kiasi kwamba hakutakuwa na masikini wa kupokea Zaka duniani.

Mashindano ya 30 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yanahudhuriwa na washirki 111 kutoka nchi 75 za mabara matano ya dunia. Mashindano hayo yameanza leo Ijumaa tarehe 20 Rajab na yatamalizika Ijumaa tarehe 27 Rajab kwa mnasaba wa Siku ya Mabaath.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 3, 2013, in Habari na Matukio, Hotuba na Mawaidha and tagged . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: