KIONGOZI MUADHAMU AKUTANA NA WAJUMBE WA BARAZA LA WANAZUONI WATAALAMU

Kiongozi Muadhamu akutana na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu
05/09/2013

Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asubuhi ya siku Alkhamisi alikutana na Mkuu na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu na kutoa hotuba muhimu, ambapo aliwausia viongozi wote pamoja na wapangaji na wachukuaji maamuzi katika ngazi tofauti za Mfumo wa Kiislamu kuwa na mtazamo mpana na uliokamilika juu ya masuala ya nchi, eneo na ulimwengu na kuchukua msimamo usio na udhaifu na unaoambatana na urazini na uono mpana. Alisisitizia juu ya hilo kwa kusema: Katika uchukuaji wao wa maamuzi na misimamo, viongozi wote wanapaswa watilie maanani misingi mitatu mikuu ya “ghaya na malengo”, “mikakati mikuu na ya umma” na “hali halisi” na kupiga hatua mbele katika kuimarisha muundo wa ndani wa Mfumo, kutatua matatizo na kusimama imara katika kushikamana na misingi mikuu kwa mtazamo wa mantiki, busara na matumaini juu ya mustakabali.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema ni jambo muhimu sana kuwa na mtazamo uliokamilika, mpana na wa pande zote juu ya matukio na masuala, na akaongezea kwa kusema: Moja ya matukio haya ni kuasisiwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ambako kulitokea katika mkondo wa tufani na dhoruba kali, kwa kuutegemea Uislamu na wakati dunia ikiwa inaelekea upande wa umaada; na tukio hili lilifanana zaidi na muujiza. Ayatullah Khamenei aliashiria upinzani na uadui ambao umekuwepo dhidi ya Mfumo wa Kiislamu tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi sasa na akasema: Sababu kuu ya uadui wote huu pia ni Uislamu. Alisema ili kuweza kufanya uhakiki sahihi wa hali ya hivi sasa katika eneo na ulimwenguni na mpangilio wa kambi zinazokabiliana na Mfumo wa Kiislamu kuna ulazima wa kuwa na uoni mpana, wa pande zote na unaowiyana na uhalisia wa mambo, na akasisitiza kwa kusema: Japokuwa tangu miaka kadhaa nyuma eneo la Magharibi mwa Asia limekuwa likidhibitiwa na kuhujumiwa na Uistikbari, lakini katika mazingira kama hayo limetokea tukio kubwa la Mwamko wa Uislamu kinyume na matakwa ya Uistikbari.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: Hii dhana kwamba Mwamko wa Kiislamu umemalizika si dhana sahihi, kwa sababu Mwamko wa Kiislamu si tukio la kisiasa tu la kumalizika kwa kuja baadhi ya watu au kuondoka kwao, bali Mwamko wa Kiislamu ni hali ya kuzinduka, kupata hali ya kujiamini na kushikamana na Uislamu ambayo imeenea katika jamii za Kiislamu.

Ayatullah Khamenei alifafanua kwa kusema: Kwa kweli tunachokishuhudia leo hii katika eneo ni radiamali ya Uistikbari ukiongozwa na Marekani dhidi ya Mwamko wa Kiislamu.

Aliashiria mpango wa kambi ya Uistikbari wa kutaka kuyatatua masuala ya eneo kwa kuzingatia manufaa na maslahi yao na akasisitiza kwa kusema: Uwepo wa Uistikbari katika eneo hili ni wa kichokozi, wa kiubabe, wa kiuchu na wenye lengo la kuufuta kila aina ya muqawama ulio dhidi ya uwepo huo, lakini kambi ya Uistikbari imeshindwa hadi sasa kuufuta muqawama huo na baada ya hapa pia hautoweza kufanya hivyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema lengo kuu la Uistikbari katika eneo ni kulidhibiti kwa kuzingatia maslahi ya utawala wa Kizayuni na akaongezea kwa kusema: Katika kadhia za hivi karibuni za Syria pia ambazo zimeanza kwa kisingizio cha silaha za kemikali, lengo ni hilihili pia, lakini Wamarekani wanajaribu kucheza na maneno ili kutaka kuonyesha kuwa wamejiingiza kwenye kadhia hiyo kwa lengo la ubinadamu.

Ayatullah Khamenei alisisitiza kwamba kitu ambacho hakina umuhimu kwa wanasiasa wa Marekani ni masuala ya ubinadamu, na akafafanua kwa kusema: Wamarekani wanatoa madai juu ya masuala ya ubinadamu katika hali ambayo rekodi yao ya nyuma ni ya magereza ya Guantanamo na Abu Ghuraib, kunyamazia kimya utumiaji wa silaha za kemikali uliofanywa na Saddam huko Halabche na katika miji ya Iran na mauaji ya raia wasio na hatia wa Afghanistan, Pakistan na Iraq.

Alisisitiza kwa kusema: Suala la ubinadamu si kitu anachoweza kuamini mtu yeyote duniani kwamba ndilo wanalofuatilia Wamarekani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliongezea kwa kusema: Sisi tunaamini kwamba wanachokifanya Wamarekani hivi sasa katika kadhia ya Syria ni ghalati na makosa, na ni kwa msingi huo pia watalihisi pigo watakalopata na bila ya shaka yoyote watapata hasara tu.

Ayatullah Khamenei alisisitiza kwa kusema: Hivi sasa baada ya miaka thelathini ya uadui, njama na hali iliyopo wakati huu, Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sio tu haujawa dhaifu bali umezidi kuwa imara kinguvu, kiuwezo na katika kupanua satua na ushawishi wake.

Baada ya kuelezea matukio yaliyopelekea kuasisiwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kuongezeka zaidi nguvu na uwezo wake licha ya uadui wote na mpangilio wa kambi za eneo na kimataifa, Ayatullah Khamenei alisema: Viongozi wote wanapaswa wazingatie misingi mitatu mikuu katika uchukuaji wao maamuzi na misimamo: 1 – Ghaya na malengo,  2 – Mikakati mikuu na ya umma na 3 – Hali halisi.

Katika kubainisha ghaya na malengo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: Ghaya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni “kujenga Ustaarabu wa Kiislamu” na jamii yenye ustawi kwa upande wa kimaada na kimaanawi.

Ayatullah Khamenei aliongezea kwa kusema: Mikakati ya kufikia ghaya hii inajulikana wazi. Mikakati hiyo ni pamoja na kushikamana na Uislamu, kutomchelea dhalimu, kutokubali kudhulumiwa katika miamala mbalimbali, mkakati wa kutegemea kura za wananchi, mkakati wa uchapaji kazi na ufanyaji juhudi wa umma na mkakati wa umoja wa kitaifa.

Alisema, kuwa na mtazamo sahihi juu ya hali halisi ambao ni msingi wa tatu ni jambo lenye umuhimu mkubwa sana na akafafanua kwa kusema: Matarajio ya kufikia ghaya yanapasa yaende pamoja na hali halisi, hata hivyo kuangalia mambo kwa kuzingatia hali halisi kunapasa kufanyike kwa namna sahihi, ya pande zote na kujiweka mbali na mtazamo wa upande mmoja.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria kuwepo hali halisi ya matukio matamu na machungu katika jamii na akasema: Katika uchukuaji maamuzi na mtazamo juu ya masuala ya nchi isiwe ni kuyaangalia matukio machungu tu bali inapasa kuyaangalia pia matukio mengine kadhaa ya hali halisi ikiwemo kuwepo fikra nzuri na watu amilifu, wachapakazi na wabunifu katika jamii, kuenea dini miongoni mwa wananchi na hasa katika kizazi cha vijana, kuendelea kubakia sha’ar za kidini na za Kiislamu na kuongezeka satua na ushawishi wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika eneo na ulimwenguni; na kwa kutegemea hali halisi ya matukio matamu kufanya juhudi za kufuta au kupunguza hali halisi ya matukio machungu.

Ayatullah Khamenei aliongezea kwa kusema: Kuwepo hali halisi ya baadhi ya matukio machungu ni mithili ya kizuizi kilichopo mbele yetu, hivyo hicho kisitufanye tughairi kuendelea na harakati yetu bali inapasa kutumia mtazamo sahihi wa kukiondoa au kukivuka kizuizi hicho.

Alisema mwenendo wa Imam Muadhamu (Khomeini) (Mwenyezi Mungu Amrehemu) katika muongo wa kwanza wa Mapinduzi nao pia ulifuata msingi na njia hiyohiyo na akafafanua kwa kusema: Imam (MA) hakuipa kisogo hali halisi ya mambo lakini pia hakulegeza msimamo katu katika misingi na usuli.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliongezea kwa kusema: Imam Khomeini (MA) ndiye yeye yeye aliyesema ”Utawala wa Kizayuni ni dondandugu la saratani ambalo lazima litokomezwe” na hakuwahi asilani kutumia taqiyya kuhusiana na utawala wa Kizayuni.

Ayatullah Khamenei alisisitiza kwa kusema: Imam Khomeini (MA) hakutumia taqiyyah pia katika kukabiliana na Marekani na uafriti wake, na ile sentensi maarufu ya “Marekani ni Shetani Mkubwa” ni maneno ya Imam.

Alisema: Hii ibara kwamba “Kutekwa ubalozi wa Marekani yalikuwa mapinduzi ya pili na pengine ni muhimu zaidi kuliko mapinduzi ya kwanza” nayo pia ni maneno ya Imam (MA).

Katika kuelezea mwenendo na utendaji wa Imam Khomeini (MA) katika muongo wa kwanza wa Mapinduzi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria kadhia ya vita vya kulazimishwa na akasema: Katika wakati uleule ambapo watu walikuwa wakitoa sha’ar za “vita vita hadi ushindi”, Imam alikuwa akisema: “vita hadi fitna iondolewe .”

Katika kufanya majumuisho ya sehemu hiyo ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei alisisitiza kwa kusema: Kulikuwa ni kusimama imara huko kwa Imam Muadhamu (MA) ndiko kulikoifanya misingi ya Mfumo wa Kiislamu iwe madhubuti zaidi.

Aliongezea kwa kusema: Hali za watu au nchi ambazo ziliachana na misingi yao kwa sababu ya kutaka kuziridhisha nyoyo za Waistikbari tunaziona hivi sasa mbele ya macho yetu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliendelea kwa kusema: Laiti kama nchini Misri kungekuwepo na sha’ar za kupambana na Israel na watu wasingelegeza msimamo mbele ya ahadi za Marekani bila ya shaka isingekuwa hivi kwamba dikteta aliyewadhalilisha wananchi wa Misri aachiliwe huru kutoka jela na wale waliochaguliwa na wananchi wa Misri waende jela na kufunguliwa mashtaka.

Ayatullah Khamenei alisema: Nchini Misri, kama wananchi wangesimama imara kushikamana na misingi, wale wapinzani waliosimama dhidi ya viongozi waliochaguliwa na wananchi hao wangejiunga na wao.

Katika sehemu hiyo ya hotuba yake alikumbusha pia nukta moja, nayo ni kuhusu mkakati mkuu wa Uistikbari wa kuzusha hitilafu za kimatapo na kimadhehebu katika eneo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: Ili kutekeleza mkakati wake huu na kuwasha moto wa fitina, adui anayatumia makundi mawili ya mamluki, kundi moja ni la mamluki wa ukufurishaji linalotumia jina la Usuni na kundi jengine ni la mamluki wanaoendesha harakati zao kwa jina la Ushia.

Ayatullah Khamenei alisisitiza kwa kusema: Majimui yoyote au nchi yoyote ile itakayohadaiwa na njama hii kubwa bila ya shaka itatoa pigo kwa harakati ya Kiislamu.

Aliongezea kwa kusema: Maulamaa wakuu wa Kishia na wa Kisuni wanapaswa wawe macho ili hitilafu zilizoko baina ya madhehebu za Kiislamu zisije zikapelekea kuanzishwa kambi mpya za kukabiliana wao kwa wao na kughafilika na adui wa asili.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliendelea na mazungumzo yake kwa kubainisha ulazima wa kuwa na mtazamo mpana na uliokamilika juu ya masuala na hali halisi ya jamii na akaashiria baadhi ya matatizo yaliyoko nchini kwa kusema: Njia kuu ya utatuzi wa matatizo ya nchi ni kuimarisha muundo wa ndani wa Mfumo kwa kutumia mtazamo wa mantiki na busara.

Ayatullah Khamenei alikumbusha kwa kusema: Kuimarisha muundo wa ndani nako pia kunawezekana kupitia maendeleo ya kielimu na uendeshaji sahihi wa uchumi.

Aliongezea kwa kusema: Sababu inayoyafanya mafuta ya nchi leo hii yaandamwe na mashinikizo, ni kwamba baada ya vita, sisi hatukuweza kupunguza utegemezi wetu kwa mafuta, kwa hivyo inapasa kila mara tuchukue hatua ya kuimarisha muundo wa ndani na kutatua matatizo kwa msaada wa irada na uwezo wetu wenyewe.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikumbusha kwa kusema: Moja ya fursa nzuri katika hali ya hivi sasa ni kuja madarakani serikali yenye nguvu mpya na yenye majimui ya watu wenye uwezo na dhamira ya kuifikisha nchi kwenye malengo yaliyokusudiwa.

Ayatullah Khamenei alimuelezea Rais Rohani pia kuwa ni shekhe mwenye rekodi na harakati katika nyuga mbalimbali na mtu mwanamapinduzi, na akasisitizia nukta hiyo kwa kusema: Katika mazingira kama haya watu wote wanapaswa kuisaidia serikali, na mimi kama ambavyo nimekuwa nikizisaidia na kuziunga mkono serikali zote nitaisaidia na kuiunga mkono serikali hii pia.

 Alifafanua zaidi kwa kusema: Bila ya shaka uungaji mkono wangu kwa serikali zote si kwa maana ya kukubaliana na yote zinayoyafanya bali inawezekana zikawepo na kasoro pia lakini kasoro hizo zisiwe kizuizi cha kutoisaidia serikali.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliongezea kwa kusema: Mbali na kuisaidia serikali inatakiwa kuipa nasaha zenye nia njema pia.

Ayatullah Khamenei alisisitizia nukta hiyo kwa kusema: Viongozi nao pia wanapaswa wazikubali nasaha wanazopewa kwa nia njema hata kama baadhi ya wakati nasaha hizo zitakuwa kali.

Aliashiria pia mpangilio wa wazi kabisa wa kambi za kieneo na kimataifa na akafafanua kwa kusema: Ulainifu na upole wa kiustadi na wa kishupavu katika nyuga zote za kisiasa ni jambo zuri na lenye kukubalika lakini ufanyaji manuva hayo ya kiustadi usiwe na maana ya kuivuka mistari myekundu na kurudi nyuma kutoka kwenye mikakati ya msingi na kuzipuuza ghaya.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikumbushia kwa kusema: Kimsingi kila serikali ina ubunifu na mbinu zake mbalimbali itakazofuata katika kutekeleza kazi zake.

Katika kufanya tathmini juu ya hali ya nchi, Ayatullah Khamenei alisema mustakabali uko safi kabisa na ni mzuri sana na akafafanua zaidi kwa kusema: Mimi nina imani na matumaini kamili juu ya mustakabali na ninaamini kwamba matatizo yote ya nchi yakiwemo ya uchumi, ya kisiasa na ya kiutamaduni ambayo ndiyo makubwa zaidi kuliko mengineyo yanaweza kutatuka.

Katika sehemu nyengine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliisifu hatua ya maana na yenye faida kubwa iliyochukuliwa na Baraza la Wanazuoni Wataalamu la kushiriki kwenye maziko ya mashahidi wa vita na akasisitizia nukta hiyo kwa kusema: Kuhudhuria waheshimiwa Mkuu na wawakilishi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu katika maziko ya mashahidi wa vita lilikuwa somo kubwa kwa jamii, kwa sababu nchi na jamii zinahitajia muda wote kudumisha kumbukumbu na kuendeleza njia ya mashahidi.

Mwanzoni mwa mkutano huo Ayatullah Mahdavi Kani, Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu alieleza kuwa kikao cha siku mbili cha baraza hilo kilikuwa kizuri na akaashiria masuala yaliyozungumziwa katika kikao hicho kwa kusema: Katika kikao hiki mheshimiwa Rais alitoa ripoti juu ya masuala na hali ya nchi, na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu nao pia walitoa dukuduku na mapendekezo yao.

Ayatullah Mahdavi Kani aliongezea kwa kusema: Baraza la Wanazuoni Wataalamu limesisitiza juu ya ulazima wa kuisaidia serikali kwa ajili ya kutatua matatizo. Vilevile Ayatullah Hashemi Shahroudi, Naibu Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu alitoa ripoti kuhusu masuala yaliyojadiliwa katika vikao na akaashiria uchaguzi wa rais na kuundwa serikali mpya na akasema, huko kulikuwa ni kuthibiti kwa ‘Hamasa ya Kisiasa’ iliyokusidiwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Aidha aliongezea kwa kusema: Tab’an sambamba na tukio hilo tamu tunashuhudia matukio machungu katika eneo ambapo fitna za Marekani na utawala wa Kizayuni zimeliingiza eneo kwenye machafuko.

Naibu Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu alisema, kutoa dukuduku juu ya masuala ya kiutamaduni na ya kiuchumi, masuala ya Syria, matukio yanayohusiana na Mwamko wa Kiislamu na udharura wa kusimama imara Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na njama mbalimbali, ni mada nyengine zilizozungumziwa na wajumbe katika kikao cha kumi na nne cha Baraza la Wanazuoni Wataalamu.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on September 8, 2013, in Habari na Matukio and tagged . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: