Ayatullah Khamenei Imam Khomeini Kiogozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Wasimamiaji wa Amali ya Hija

11/09/2013

image

Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na wasimamiaji wa amali ya Hija mwaka huu na kuitaja ibada ya Hija kuwa ni chimbuko la nguvu za kisiasa, kiutamaduni na kimaanawi katika jamii ya Kiislamu na huku akiashiria hali iliyopo hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na katika eneo la Mashariki ya Kati pamoja na njama za maadui za kutaka kuzusha mizozo na mapigano baina ya Waislamu wenyewe kwa kwenyewe kwa kutumia kisingizio cha kuwepo tofauti za kimadhehebu baina ya Waislamu na vile vile kwa kutumia vitisho na vita vinavyoendeshwa na madola ya kibeberu duniani amesema kuwa: Tunatumai kuwa msimamo mpya wa Marekani kuhusiana na Syria utakuwa ni wa kweli na ulio mbali na udanganyifu na utakuwa na maana ya Marekani kutambua uhalisia wa mambo tofauti na msimamo ghalati na wa kibeberu uliooneshwa na nchi hiyo katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu amesisitiza kuwa, moja ya mambo ya lazima kwa Hija ya kweli ni kuweko mienendo ya kidugu baina ya Waislamu katika kalibu ya ibada hiyo kubwa na tukufu.
Ameongeza kuwa, kujiweka mbali na mizozo mabishano na malumbano katika siku za Hija kama ilivyosisitizwa na Qur’ani Tukufu kuna maana ya Waislamu kuacha malumbano na ndugu zao wengine wa Kiislamu na kujiepusha huko kunahusisha malumbano na mabishano ya maneno na chuki za ndani ya nyoyo.
Ayatullah Udhma Khamenei ametahadharisha kwa kusema: Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa baadhi ya watu wanashindwa kuelewa maana ya jambo hilo na wanatoa tafsiri potofu kuhusiana na kupigwa marufuku mabishano katika Hija ikiwa ni katika njama zao za kutaka kufuta kabisa falsafa ya kufanyika amali ya kutangaza kujibari na kujiweka mbali na washirikina licha ya kwamba wanatambua kuwa kujadiliana na kuwajengea hoja makafiri na washirikina ni moja ya misingi mikuu ya mafundisho ya Uislamu.
Vile vile ametoa mwito kwa Waislamu kuwa macho mbele ya njama za maadui wanaotaka kushadidisha ugomvi na mizozo ya kimadhehebu katika safu za Waislamu na kuongeza kuwa: Maadui wa umma wa Kiislamu wanaelewa vizuri kuwa, ugomvi na mapigano kati ya madhehebu mbali mbali ya Kiislamu ni kwa faida na manufaa ya utawala ghasibu wa Kizayuni na ni kwa sababu hii ndio maana maadui hao wameanzisha makundi ya kuwakufurisha Waislamu wengine kwa upande mmoja na vile vile kuanzisha vyombo vya habari ambavyo kijuu juu vinaonekana kuwa ni vya Kiislamu kwa upande wa pili huku vingine vikionekana kuwa na hata sura ya Kishia ili kuchochea ugomvi na hitilafu kati ya Waislamu na hatimaye Waislamu wapigane wenyewe kwa wenyewe.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Wanavyuoni wakubwa wa Kishia akiwemo Imam Khomeini (quddisa sirruh) siku zote wamesisitizia umoja na mshikamano katika umma wa Kiislamu hivyo ule Ushia unaonezwa na vyombo vya habari vilivyoko London na Marekani ambao lengo lake ni kueneza hitilafu na ugomvi katika safu za Waisalmu, si Ushia unaofuata njia na misingi sahihi ya Ushia.
Ayatullah Udhma Khamenei ametaja nukta nyingine nzuri ya Hija ambayo inauandalia umma wa Kiislamu mazingira ya kupata nguvu kubwa kadiri inavyowezekana kuwa ni jinsi ibada hiyo inavyotoa fursa kwa Waislamu kubadilishana utamaduni sahihi wa Kiislamu na kuwa na taarifa kuhusu matukio na maendeleo ya jamii nyinginezo za Waislamu wakati wa ibada ya Hija na kuongeza kuwa: Kutokana na kuweko idadi kubwa sana isiyotasawirika ya vyombo vya habari vinavyoipiga vita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, moja ya majukumu ya mahujaji wa Kiirani ni kutangaza na kuwaeleweshwa Waisalmu wengine sura sahihi ya Uislamu na madhehebu ya Kishia na uhakika wa mambo kuhusu maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini Iran chini ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, kupitia maneno na matendo mema ya mahujaji hao wa Kiirani.
Vile vile amesisitiza kuwa, kutia nguvu umaanawi ni moja ya misingi mikuu ya Hija ya kweli na kukumbusha kwamba: Kuwa na imani yenye nguvu, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kuwa na dhana nzuri kuhusiana na ahadi za Mwenyezi Mungu jambo ambalo ni la lazima kwa ajili ya kuvuuka kwenye mashaka na matatizo mengi na kutoogopeshwa na haiba bandia ya madola ya kibeberu, ni katika mambo muhimu yanayopatikana katika Hija.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia jinsi maadui wa umma wa Kiislamu wanavyotumia kisingizio cha Usuni na Ushia na kuendesha vita katika nchi za Pakistan, Afghanistan, Iraq, Syria na Bahrain na kupelekea mamia ya watu wasio na hatia kuuawa na kuongeza kwamba: Waistikbari na madola ya kibeberu hasa hasa Marekani hawaoni tabu hata chembe kuziangamiza na kuziharibu nchi za Kiislamu na kuua watu kiholela kwa ajili ya kulinda malengo yao haramu.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia mabadiliko na matukio ya nchini Syria pamoja na vitisho vya wiki kadhaa zilizopita vya Wamarekani vya kutaka kuzusha vita vipya katika eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa: Wamarekani wako tayari hata kuanzisha vita na kukanyaga manufaa ya nchi na mataifa mengine yote kwa ajili ya kulinda manufaa yao wanayodai ni ya kitaifa wakati uhakika wa mambo ni kuwa hayo ni manufaa ya Wazayuni na mabepari wakubwa tu wa Marekani.
Amesisitiza kuwa ana matumaini msimamo huu mpya wa Marekani kuhusiana na Syria utakuwa ni wa kweli ulio mbali na mchezo wa kisiasa na kuongeza kuwa: Kama itakuwa ni hivyo, basi itakuwa na maana ya kuachana Marekani na msimamo wake wa kibeberu na mbovu iliokuwa nao wiki kadhaa zilizopita.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kwamba: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa kina na kwa umakini mkubwa matukio yanayotokea katika eneo la Mashariki ya Kati.
Ayatullah Udhma Khaenei ameongeza kuwa: Sisi tukiwa ni taifa kubwa katika eneo hili nyeti (la Mashariki ya Kati) tunapaswa kuwa na mtazamo sahihi na tutumie nguvu na uwezo tunaopewa na dini yetu ya Kiislamu kuwatangazia watu wote malengo yetu matukufu na ya kibinaadamu na kuwalingania walimwengu faida na manufaa ya kuishi kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.
Ameongeza kuwa: Manufaa ya kuishi kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu ni kujengeka nguvu ya ndani ya taifa lenye imani thabiti, lenye watu walioshikamana vizuri, lenye viongozi wanaofanya vizuri kazi zao, kuweko mapenzi baina ya wananchi na viongozi wao na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja baadhi ya mambo ya msingi na ya lazima ya kuweza kuwa na nguvu za ndani kuwa ni pamoja na akili, umaanawi, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kwa bidii na hekima.
Ameongeza kuwa: Harakati ya mfumo wa Kiislamu katika njia hiyo ya kuimarisha nguvu zake kadiri inavyowezekana bila ya shaka yoyote itakuwa na athari katika hali ya eneo la Mashariki ya Kati kama ambavyo hali imekuwa hivyo kwa kipindi chote cha huko nyuma.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Hujjatul Islam Walmuslimin Qadhi Askari, mwakilishi wa Fakihi Mtawala na msimamiaji wa mahujaji wa Kiirani sambamba na kutoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Hija na Muongo wa Heshima, ametaja baadhi ya kazi muhimu zilizofanywa na ambazo zinaendelea kufanywa na Biitha ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni pamoja na kutunga hati ya kiistratijia ya Hija, kutilia nguvu na hima Qur’ani tukufu kadiri inavyowezekana, kufanya juhudi za kuleta mabadiliko ya kiroho katika nyoyo za mahujaji wa Kiirani kupita kutoa mafunzo mbali mbali kabla ya kuelekea kwenye maeneo matukufu ya kutekelezea ibada ya Hija, kulinda haki za mahujaji, kutilia nguvu suala la kufanya utafiti na uhakiki kuhusu masuala yanayohusiana na Hija, kuitisha kongamano la wataalamu wa masuala ya Hija, kuongeza kiwango cha elimu cha masheikh wanaoongoza misafara ya Hija, kutoa kozi na masomo maalumu ya lugha ya Kiarabu na kuangalia uzoefu uliopatikana pamoja na matatizo yaliyozikumba ratiba za huko nyuma.
Kwa upande wake, Bw. Jannati, Waziri wa Utamaduni na Miongozi ya Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa ripoti iliyoonesha jitihada mbalimbali zilizofanyika kwa ajili ya kuleta uratibu wa pamoja kati ya taasisi na vyombo vyote vinavyoshughulikia masuala ya Hija nchini pamoja na kuzidi kusahilisha utoaji huduma kwa mahujaji. Amesema: Hija ni fursa nzuri ya kuweza kuyafikishia mataifa mengine utamaduni wa Kiislamu wa Iran.
Vile vile amesisitizia umuhimu wa kuzingatiwa falsafa, siri na mafundisho matukufu ya Hija na kuongeza kuwa: Kuweko mawasiliano baina ya shakhsia na watu wakubwa wakubwa wa kidini na kielimu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na shakhsia wa maeneo mengine ya ulimwenguzi wa Kiislamu kunaandaa uwanja wa kuzidi kupatikana mapenzi na mshikamano katika umma wa Kiislamu.
Kwa upande wake Bw. Awhadi, Mkuu wa Taasisi ya Hija ya Iran ameashiria kwamba mwaka huu kutakuwa na mahujaji 64000 wa Kiirani ndani ya misafara 500 tofauti kutoka vituo 17 vya kurukia ndege kote nchini Iran na kuongeza kuwa, Taasisi ya Hija ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itapokea pia mahujaji 2000 wa Kiirani waishio nje ya nchi.
Vile vile amesema, kuwa na sehemu moja inayoshughulikia suala zima la sehemu wanazofikia mahujaji wa Kiirani na ambacho pia kinashughulikia utoaji wa huduma kwa mahujaji hao na vile vile kuweko vituo maalumu vya matibabu katika misafara ya mahujaji hao na hospitali mbili zinazofanya kazi usiku na mchana katika miji mitakatifu ya Makka na Madina ni miongoni mwa kazi zinazofanywa na Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on September 12, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: