AYA YA MUBAHALA NI CHANGAMOTO KWA KILA ZAMA

Eid Mubahala

Aya hiyo ni: (Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo)!  (Qur’an 3:61)

Hapa, Wafasiri wote wamekubaliana kwamba neno “wanawake wetu” linahusu Fatimah Zahra (A.S), na hivyo ndivyo alivyotaka Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kuonyesha kwa kivitendo.

Historia ya tukio hili la majadiliano ambalo Mtume (saw) aliamrishwa pamoja na baadhi ya Wakristo, Mtume (saww​​) alichukua njia mbadala ili kukabiliana na hali halisi ya wakati ule pale Majadiliano yalipofikia ukomo, na ni njia hii ya changamoto ambayo aya hizi inazielezea.

Riwaya ya kutoka Ali bin Ibrahim al- Qommi, kutoka kwa Imam al-Sadiq (as) anasema kwamba: ‘Wakristo wa Najran walikuja (Jopo) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu …. na Waswali kwa kutumia kengele; Maswahaba wa Mtume walipinga kwa kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! huu ni Msikiti wako? Akawajibu mtume: Waacheni ( Waombe watakavyo).

Pindi walipomaliza walimwendea Mtume (saw​​) na Kumuuliza: Ni upi ushuhuda wako? Akawajibu: Tuanashuhudia kuwa hakuna mungu  Isipokuwa Allah na kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba Isa ‘ (Yesu) (AS) Ni Mja aliyeumbwa (na Mwenyezi Mungu), Anakula, Kunywa na kwenda choo.

Wakasema: Ni nani basi baba yake? Ndipo uliposhuka Wahyi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ukisema: Sema kuwaambia hao– Mnasemaje kuhusu Adamu, Je aliumbwa ni mja wa Mwenyezi Mungu. Anayekula, kunywa na kwenda choo na kuoa? Mtume (saw) akawauliza na wakajibu: ndiyo.

Kisha akawauliza ni nani baba yake? Hawakuweza kujibu, Ndipo Allah (sw) akateremsha aya “Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akasema: Kuwa! Basi akawa (Qur’an 3:59) Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka. Watakao kuhoji katika haya … Waambie tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo! Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema nawapeni changamoto hii: Kama mimi ninayoyasema ni kweli laana iwashukie, na kama mimi ni muongo laana inishukie wakasema hakika wewe unachozungumza ni haki.

Wakakubaliana siku ya Mubahalah (changamoto). Wakati waliporudi maeneo waliyokuwa wanakaa, Viongozi wao al- Sayyid, al -Aqib na al-Ahtam wakasema: Kama yeye (Muhammad) atotoa changamoto hiyo akiwa na watu wake, basi sisi tutaikukubali changamoto hiyo kwasababu yeye si Nabii , lakini kama atatoa changamoto hiyo akiwa na familia yake hatutakubali changamoto yake, kwa maana yeye hawezi kuwatoa watu wa familia yake isipokuwa ni atakuwa ni mkweli.

Asubuhi ilipowadia, wakaja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na wakamkuta pamoja naye yupo Amiri wa Waumini Ali bin Abii Twalib, Fatima, Hassan na Hussein (as), hapo Wakristo Wakauliza: Ni akina nani hao? Watu wakajibu: Huyu ni binamu yake na mrithi wake, na huyu ni binti yake Fatimah na hawa ni watoto wake Hassan na Hussein. Basi hapo wakingiwa na hofu na wakamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww​​): Sisi tumeridhia na tafadhali turuhusu tuondoke tusiingie katika changamoto hii’

Rejea:

      i).          Tafsiri ya Al-Qummi, Juzuu ya 1, Uk. 104;

    ii).          Sahih Muslim, Juz. 4, Uk. 1871;  

   iii).          Sunan al- Turmuthi , vol. 5, ukr . 638;

   iv).          Shawahid al-Tanzeel , vol. 1, uk. 155 ;

    v).          Sawaiq al- Muhriqah, uk. 148;

   vi).          al- Kamil fil Tareekh , vol. 2, ukr . 393.

…… ‘Na wanawake wetu’: na miongoni mwa wale wanawake ambao wanawakilisha ukuruba wa Kibinaadamu na kiroho kwangu na katika maisha yangu, hapa namtanguliza mbele binti yangu Fatima, Mtukufu wa wanawake wa Duniani, ambaye ni ‘sehemu yangu mimi’ na ‘Mwenyezi Mungu anakuwa na hasira kwa hasira yake na kuridhika kwa kuridhika kwake Namtanguliza katika changamoto hii kubwa ili kuthibitisha kuwa mimi nina uhakika kabisa kuhusu ukweli wa Ushuhuda wangu, kwa hakika ya mtu hawezi kuwaweka mbele ya hatari watu vipenzi vyake isipokuwa anahakika ya usalama wao.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 29, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: