NAFASI YA BI FATMAT ZAHRAA (as) KATIKA AYA YA MUBAHALA

fATIMATU ZAHRAA KATIKA AYA YA mUBAHALA

 

Tukio la Mubahila ni maarufu na linajulikana kwa Waislamu wote. Wasomi wote wa Kiislamu wanakubaliana kwa pamoja juu ya ukweli kwamba aya ya Mubahala iliteremshwa kuhusiana na ujumbe wa Wakristo ambao walikuja kutoka Najran kupingana na Mtume (SAW) kuhusiana na suala la Nabii Isaa Ibn Maryam/ Isa mwana wa Mariamu (as) Katika Juzuu ya 6 Bihar, Imamu Ali (as) analieleza tukio husika kwa njia zifuatazo:

Ujumbe wa Najrani Wakristo wakiongozwa na watu watatu maarufu, Al-Aqib, Muhsen, na Askofu Mkuu; pamoja na Mayahudi wawili maarufu walikuja kwa Mtume (SAW). Wakitaka kuhojiana naye;

askofu mkuu ilianza: “Abu Qasim, Ni nani alikuwa baba yake Musa ?” Mtume akajibu: “Imran.”

kisha Askofu mkuu akauliza:” Nani alikuwa baba wa Yusuf?” Mtume akajibu: “Yaaqub.”

Askofu mkuu aliendelea: “Najitoa sadaka kwako; Ni nani baba yako?” Mtume akajibu: “Abdullah Ibn Abd al -Muttalib.”

Kisha askofu mkuu aliuliza: “Ni nani baba yake Isaa (Yesu)?” Mtume (SAW) akasubiri kitambo kidogo Malaika Jibril akamshushia Wahyi ufufuatao: “(Sema) alikuwa Roho wa Mwenyezi Mungu na neno lake”

Askofu mkuu kisha akauliza: “Je, anaweza kuwa Roho bila kuwa na mwili?”

Kwa Mara nyingine tena ufunuo (Wahyi) ukashuka kwa Mtume (SAW) kama ifuatavyo: “Mfano wa Isaa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama ule wa Adamu; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa’ na akawa”

Alipoyasikia hayo Askofu mkuu, akaruka na kupinga maneno ya Mtume aliyoyasema kuwa Isaa (AS) aliumbwa kutokana na udongo, askofu akasema: “Muhammad, hatukulipata hilo katika Taurati, Biblia, au katika Zaburi. Wewe ni mtu wa kwanza kusema hilo. ”

Huu ukawa ndio wakati Aya ya Mubahala ilipoteremshwa.

Aya ikisema “Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo)!  (Qur’an 3:61)

Baada ya ujumbe wa wakiristo kusikia Aya hiyo, walisema: ” Tupangie muda kamili kwa ajili ya kikao hicho cha maombi (ambao kila upande Utaomba dua kwa Mwenyezi Mungu kulaani upande mwingine kama wao ni wafuasi wa uwongo).”

Jibu la mtume kwa dai lao hilo ilikuwa “Kesho asubuhi, Inshallah.”

Asubuhi ilipowadia, Mtume baada ya kumaliza Swala ya Asubuhi akamuamuru Ali na Fatima wamfuate, na Ali akiwa amewashikilia Hassan na Hussein.  Mtume (SAW) akawaambia: “Wakati mimi nitakapokuwa naomba dua mtapaswa kusema : Amina.”

Pindi ujumbe wa Wakristo ulipoona msafara familia takatifu na kwamba Mtume (SAW) alikuwa amekwisha tandika mkeka kwa ajili yake mwenyewe na familia yake, Wakasemezana miongoni mwao: “Kwa jina Mwenyezi Mungu, Huyu ni Mtume wa kweli, na kama atatulaani sisi hakika Mwenyezi Mungu atajibu maombi yake na kutuangamiza sisi. Kitu pekee ambacho kinaweza kutuokoa, ni kumwomba ututoe sisi katika kikao hichi. “.

Razi, katika tafsiri yake ya Qur’an inasema:

Askofu Mkuu alisema: “Enyi Wakristo, hakika mimi naziona nyuso za watu, watu ambao kama watamuomba Mwenyezi Mungu kuhamisha Mlima, bila ya shaka atafanya hivyo. Msikubali kufanya kikao hicho, au nyote mtaangamia na hakutabakia Mkiristo yeyote katika dunia hii mpaka Siku ya Kiyama. ”

Basi hapo Ujumbe wa wakiristo ukamuendea Mtume na kusema: “Abu Qasim, tukubalie sisi kuondoka kuachana na Kikao hichi kitukufu”.

Mtume akasema: “Hakika mimi nitawakubalia, lakini mjue yule aliyenituma kwa haki ni shahidi yangu Lau mimi ningeliwalaani, Mwenyezi Mungu asingalimuacha Mkristo yeyote juu ya uso wa dunia.”

Huu ulikuwamuhtasari wa hadithi husika. Mambo muhimu kwetu hapa ni maneno aloyasema Mwenyezi Mungu katika Qur’an Sura ya 3 Aya ya 61 Maneno Wanawake wetu na wanawake wenu.

Waislamu wote wamekubaliana kuwa Mtume (SAW) alimchukua Ali (as) pamoja naye kuwakilisha ” neno “sisi wenyewe”, na akamchukua Hassan (AS) na Hussein (AS) kuwakilisha “Watoto wetu,” na Fatima Zahra (SA) kuwakilisha neno “Wanawake wetu,” pia ni ukweli usiopingika kuwa Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) hakuongozana na Mwanamke mwingine yeyote ikiwemo wake zake, shangazi zake, au hata Mwanawake mwingine yoyote wa kiislamu.

Huu ni uthibitisho tosha kwamba kulikuwa hakuna mwanamke aliye bora, Mchamungu, Mtakatifu, na Msafi kama Fatima (SA). Mtume alimwita Fatima mwanamke peke yake kuongozana nae, kwa sababu yeye pekee ndiye mwanamke alikuwa uwezo kutimiza vigezo vya Aya husika.

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 30, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: