Ibada za Mwezi wa Muharram

lvl120131105103957

Mwezi wa Muharram ni mwezi wa huzuni kwa Ahl al-Bayt (AS) na wafuasi wao. Kwa hali hii, Imam al- Ridha (as) asimuliwa kusema, ” Katika mwanzo wa Muharram, baba yangu (AS) kamwe hakutabasamu wakati wote. Alikuwa ni mwenye kugubikwa na Majonzi na unyongefu kwa siku kumi. Siku ya kumi ya mwezi huwa siku ya msiba wake mkubwa, kilio, na huzuni, na alikuwa akisema kwamba katika siku hii Imam al- Hussein (AS) aliuawa. “

Siku wa kwanza ya Muharram

Sayyid Ibn Nawus, katika Iqbal al-amal, ametaja idadi za swala zilizo kokotezwa kuswaliwa usiku Huu kma ifuiatavyo;

Swala ya kwanza: Rakaa mia moja kwa kusoma Surah al- Fatiha na Sura al- Tawhid.

Swala ya pili: Rakaa mbili katika kila rakaa isomwe Sura al-Fatihah na al-an-aam (No.6) na katika rakaa ya pili Sura al- Fatihah na Yasin (No. 36).

Swala ya tatu: Rakaa mbili ambazo katika kila rakaa sura al- Fatihah isomwe pamoja na Surah al -Tawhid mara kumi na moja.

Mtume (SAW) anasema yeyote atakaye swali swala hizi katika usiku huu na kufunga siku yake inayofuatia, ambayo itakuwa siku ya kwanza ya mwaka mpya, Mwaka mpya wake utakuwa  Mwema kwake yeye, na atakuwa katika ulinzi Mwaka mzima, na kama atakufa ataingizwa peponi.

 Siku ya Kwanza ya Mwezi wa Muharram

Kwa kuwa ni siku ya kwanza katika mwaka mpya, kuna mambo mawili yaliyokokotezwa kufanywa nayo ni;

Kwanza: Imekootezwa kufunga katika siku hii. Rayyan bin Shabib atasimulia kwamba Imam al-Ridha (as) alisema, “Kama vile alivyojibu dua ya Mtume Zakaria, Mwenyezi Mungu hupokea Swala ya mtu ambaye kafunga siku hii na anaye muomba yeye.”

Pili: Imam al-Ridha (as) anahadithia akisema kuwa Mtume (SAW), siku ya kwanza ya mwezi wa Muharram, alikuwa akiswali Rakaa mbili. Alipomaliza, alikuwa akiinua mikono yake kuelekea mbinguni na kuomba dua ifuatayo mara tatu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

Mwenyezi Mungu wangu , Wewe ni Mola wa milele , huu ni mwanzo wa mwaka mwingine mpya ; hivyo mimi , nakuomba wewe kwa nyakati hizi, , kuniweka mbali na Shetani, kwa kunipa mamlaka juu ya “Nafsi yangu” kuiepusha na dhambi na kupotoka , Ili kwayo inikurubishe karibu yako,

Oh! Mwingi wa rehema!  Eeh Mmiliki wa utukufu na wema! O Msaidizi asiye na msaidizi! Ewe Mtoaji asiyehitajia mtoaji! Ewe Mwenye kuona juu yasiye na ulinzi! Ewe umsaidiaye asiye na matumaini ya Msaada! Ewe hazina ya yule asiye na hazina! Ewe ambaye mjuzi mzuri wa kuweka mitihani na majaribu! Ewe tumaini la mwisho! Ewe nguvu ya walio dhaifu! Ewe mkombozi wa wanaozama! Ewe muokoaji wa wanaozama, Ewe mwenye kuokoa kutoka majanga! Ewe ambaye hugawa neema! Ewe ambaye huonyesha hisani na ukarimu! Ewe mwenye kuhudumia kwa wema na ukarimu! Oh ambaye hutenda kwa neema!

Wewe ni yule ambaye kabla yako, kwa utii vimekuwa vikikusujudia weusi wa usiku na mwangaza wa Mchana, Mwangaza wa mbalamwezi,Miale ya jua, mawimbi ya maji, Magome vya miti! Ewe Mwenyezi Mungu, Hakuna wa kukushirikisha umetakasika!

Ee Mwenyezi Mungu tufanya wakarimu, wema na wenye busara, zaidi ya wanavyoweza kutufikiria au kubashiri, Tusitiri na kusindikize kwa yale wasiyoyajua, na wala (wasiweze) kutuhusisha na wasemacho. Anayenitosha ni Mwenyezi Mungu (kwa ajili yangu), hakuna mungu isipokuwa yeye, Kwake yeye naegemeza matarajio yangu, na Yeye ni Mola wa Arsh kuu.

Tunaamini kwamba yote ni kutoka kwa Mola wetu, na wala hasemi (haya) isipokuwa wale ambao wana mioyo safi na akili timamu. Mola wetu Mlezi! Usizipoteze nafsi zetu baada ya kutuongoa na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye mtoaji.

Shaykh al-Tusi anasema: Inapendekezwa kufunga swaumu ya Sunnah siku Tisa za mwanzo za Mwezi wa Muharram. Siku ya kumi imesisistizwa kujizuia kula na kunywa mpaka wakati wa Alasiri. Baada ya hapo, mtu anaweza kula kipande kidogo katika udongo wa kaburi la Imam al-Hussein (turbat al- Hussein) udongo ulichukuliwa kutoka eneo karibu na kaburi takatifu la Imam al- Hussein).

Sayyid Ibn Nawus ametaja fadhila za kufunga mwezi mzima wa Muharram na kuongeza kuwa kitendo kama hicho humlinda mja dhidi ya kutenda dhambi yoyote.

Siku ya Tatu ya Muharram

Katika siku hii, Nabii Yusuf (Joseph) (AS) aliachiwa huru kutoka gerezani. Hivyo, kama mtu atafunga siku hii, Mwenyezi Mungu Mtukufu atamfanyia wepesi katika ugumu wowote utakaomkabili na atamuondolea matatizo yoyote ambayo yatamkabili. Kwa mujibu riwaya kutoka kwa Mtume (SAW), Mwenyezi Mungu atajibu Swala ya yule atakayefunga katika siku hii.

Siku ya Tisa ya Muharram

Siku ya Tisa ya mwezi wa Muharram huitwa Tasu’a1. Imam Swadiq (as) imepokelewa akisema, ” siku ya Tisa (9) ya mwezi wa Muharram, Imam Hussein, pamoja na wenzake, Walizingirwa hapo Karbala wakati Wapiganaji wapanda farasi wa kisyria walipomzunguka na kumuachia mwanya mwembamba sana. Mtoto wa Marjanah (yaani ` ibn Ubaydullah Ziyad) na Umar bin Saad walikuwa na furaha sana kutokana na idadi kubwa ya wapanda farasi ambao walishiriki katika kupambana dhidi ya Imam Hussein (AS). Hivyo, adui akawa na uhakika kwamba hakuna msaidizi angeliweza kujiunga tena na jeshi la Imam Hussein (AS) kumsaidia na hususan watu wa Iraq. “Imam Swadiq (as) kisha akaongeza kusema,” Nimtoe kafara ya sadaka baba yangu kwa aliye Mnyonge na mgeni (yaani Imam Hussein). “

 Usiku wa siku ya kumi ya Muharram; Usiku wa Ashura

Sayyid Ibn Nawus, katika Iqbal al-Amal, ametaja idadi ya sala na idadi kubwa ya Swala ambazo zimekokotezwa kuswali katika usiku huu wa siku ya kumi ya Muharram. Aidha ameelezea fadhila kubwa kabisa zinazopatikana kwa kuswaliwa swala husika na dua zake.  Kwa mfano, inapendekezwa Kuswali swala ya Rakaa mia moja kwa kusoma Surah Fatiha mara moja na Surah Tawhid mara tatu. Baada ya kukamilisha, Kwa sauti ya unongonezo na unyenyekevu soma dua hii mara sabini:

Utukufu wote ni kwa Mwenyezi Mungu ,

sifa zote nyema ni za Mwenyezi Mungu,

hakuna Mungu ila Mwenyezi Mungu ,

Mwenyezi Mungu ni Mkubwa ,

na kuna kitu nguvu wala wala utawala ila kwa Mwenyezi Mungu , mjuzi wa yote na Mwenye nguvu.

Kwa mujibu wa riwaya nyingine, mtu anapaswa kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu na kuomba haja yake baada ya kauli zilizotajwa hapo awali.

Na pia imependekezwa kuswali rakaa nne (4) wakati wa mwisho wa Usiku huu, Ukisoma sura Fatiha mara moja na ukirudia Ayatul Kursi na Sura Tawhid, Falaq, Annas, Mara kumi kila moja.

Na pia imependekezwa kuswali Rakaa nne na kusoma Sura Fatiha mara moja, na Sura al-Tawhid Mara hamsini. Mfanano na Swala ya  Imamu ‘Ali Amirul-Muuminiyn (AS ), ambayo huleta malipo makubwa, Sayyid Ibn Nawus anasema baada ya kutaja swala sala hii, “Baada ya kumaliza rakaa ya nne, unaweza kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuombe baraka zimwendee  Mtume na watu nyumba yake , na kuwalaani maadui wao mara nyingi iwezekanavyo.

Ama kuhusiana malipo ya kujishughulishwa usiku huu nzima na matendo ya ibada, imepokelewa katika riwaya kwamba mtu ambaye atafanya hivyo atahesabiwa kuwa amefanya ibada ya kumcha Mwenyezi Mwenyezi Mungu sawa na ibada ya malaika wote. Aidha, kufanya matendo ya ibada katika usiku huu ni sawa na ibada ya miaka sabini. Aidha, kwa mtu ambaye amefanikiwa kutembelea kaburi la Imam al-Hussein (AS) katika usiku huu na kuutumia usiku mzima huko hadi asubuhi, Mwenyezi Mungu atamfufua, Siku ya Hukumu, akiwa na matone ya damu ya Imamu Hussein (AS) katika kundi la wale ambao walikufa Mashahidi  pamoja naye.

Ziyarat of Ashura

 

 

 

 

 

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on November 5, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: