Kiongozi Muadhamu Aonana na Wanachuo na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari

wpid-329348_leader-hajj.jpg

Kiongozi Muadhamu Aonana na Wanachuo na Wanafunzi wa Shule za Msingi na SekondariAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi, (Jumapili) ambayo imesadifiana na siku ya kukaribia maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari nchini Iran, ameonana na maelfu ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wa daraja nyingine za elimu nchini Iran na sambamba na kutoa miongozo na ufafanuzi muhimu sana kuhusu mizizi ya uadui wa ubeberu kwa taifa la Iran pamoja na kutangaza uungaji wake mkubwa na madhubuti kwa viongozi wa Iran kutokana na jitihada zao kubwa wanazofanya, amesisitiza kuwa: Uzoefu uliopatikana kutokana na vitendo vya Marekani unaonesha kuwa, kadhia ya nyuklia ni kisingizio tu kinachotumiwa na nchi hiyo kwa ajili ya kuendeleza uadui wake dhidi ya Iran. Amesema, mtu yeyote hapaswa kupumbazwa na wala kuhadaiwa na tabasamu za kilaghai za adui. Amesema, kama mazungumzo yanayoendelea yatazaa matunda mazuri, ni bora, lakini kama haitakuwa hivyo basi itakuwa ni kuthibitisha na kuzidi kuzitia nguvu nasaha ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara kuwa, utatuzi wa matatizo yaliyopo nchini, umo ndani ya nchi.Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria matukio matatu ya kihistoria yanayohusiana na tarehe 13 Aban, (Novemba 4) na kusema kuwa, mwaka 1343 Hijria Shamsia (Novemba 4, 1964) Imam Khomeini (quddisa sirruh) alifukuzwa nchini Iran kutokana na hotuba aliyoitoa dhidi ya mfumo wa ukandamizaji na udhalilishaji uliokuwa ukifanywa na maafisa na wanajeshi wa Marekani nchini Iran, wa kupewa maafisa hao wa Kimarekani kinga ya kutoshitakiwa nchini Iran hata wanapofanya kosa kubwa namna gani, tarehe 13 Aban mwaka 1357 Hijria Shamsia (tarehe 4 Novemba, 1978 Milaadia), kulitokea mauaji ya kikatili yaliyofanywa na askari wa utawala wa kidikteta wa Kifalme nchini Iran uliokuwa ukiungwa mkono kikamilifu na Marekani dhidi ya wanafunzi mjini Tehran, na tarehe 13 Aban 1358 Hijria Shamsia (Novemba 4, 1979 Milaadia), wanafunzi wa Iran walichukua hatua ya kishujaa ya kuuteka ubalozi wa Marekani mjini Tehran, matukio yote hayo matatu yanahusiana na Marekani kwa namna moja au nyingine na ni kwa sababu hiyo ndio maana tarehe 13 Aban ikatangazwa kuwa Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari.

Ameendelea na hotuba yake kwa kubainisha neno la Qur’ani kuhusu uistikbari lakini kabla ya hapo amekumbushia nukta moja muhimu na kuongeza kuwa, vijana wenye imani thabiti na mashujaa kutoka Vyuo Vikuu mwaka 1979 waliuteka ubalozi wa Marekani mjini Tehran na kuwatangazia walimwengu uhakika na sura hasa ya ubalozi huo ambao kwa hakika lilikuwa pango la kijasusi kwa maana halisi ya neno.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, siku hiyo vijana wetu waliupa ubalozi wa Marekani jina la pango la kijasusi na leo hii, baada ya kupita zaidi ya miongo mitatu, ofisi za kibalozi za Marekani katika nchi za Ulaya ambazo ni marafiki na waitifaki wa karibu wa Marekani, zimepewa jina la mapango ya kijasusi, jambo ambalo linaonesha kuwa vijana wetu walikuwa mbele ya kalenda ya historia ya dunia kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Baada ya kubainisha nukta hiyo, Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuhusu maana ya ubeberu na uistikbari kwamba: Neno uistikbari hutumiwa kwa watu au tawala ambazo zinalihesabu suala la kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine na kuyatwisha matakwa yao kuwa ni haki yao na kwamba hakuna mtu aliye na haki ya kuwauliza.

Ameongeza kuwa: Katika upande wa pili, mkabala na neno uistikbari ni mataifa na watu ambao hawako tayari kuburuzwa na wala hawaruhusu madola ya kibeberu yaingilie masuala yao ya ndani na kuwatwisha matakwa yao na ambao wanasimama kidete kupambana na ubeberu huo ambapo taifa la Iran ni miongoni mwa mataifa hayo.

Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa serikali ya Marekani ni serikali ya kibeberu ambayo inajipa haki ya kuingilia masuala ya ndani ya mataifa yote ya dunia na kuongeza kuwa: Kwa mapinduzi yake iliyofanya, taifa la Iran kwa hakika limesimama imara kukabiliana na ubeberu na uistikbari wa Marekani na hata baada ya kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia, mapambano hayo yaliendelea na taifa la Iran lilikata mzizi wa mababeru ndani ya nchi na tofauti na baadhi ya nchi, taifa hili halikufanya mambo nusu nusu likaja likapata madhara baadaye, (bali limeenda mpaka mwisho na faida zake zinaonekana).

Aidha amesisitiza kuwa, kumlegezea kamba muistikbari hakuna faina yoyote kwa nchi na kwa taifa lolote lile na kuongeza kuwa, msimamo wa kibeberu wa Marekani umeyafanya mataifa mengine duniani kuwa na hisia ya kutoiamini nchi hiyo na kujitenga nayo, kama ambavyo pia uzoefu unaonesha kuwa, taifa na serikali yoyote ile ambayo inaiamini Marekani basi mwisho wake hupata pigo hata kama itakuwa ni katika marafiki wa Marekani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mifano kadhaa kuhusu suala hilo ikiwa ni pamoja na jinsi Dk Mosadiq nchini Iran alivyowaamini Wamarekani na majibu ya Marekani yakawa ni kuipindua serikali ya Dk Mosadiq tarehe 28 Mordad (Agosti 18, 1953), na vile vile jinsi Wamarekani walivyomsaliti Muhammad Reza Pahlavi baada ya mfalme huyo wa zamani wa Iran kuikimbia nchi na kuongeza kuwa: Leo hii Marekani ndilo dola linalochukiwa zaidi na mataifa ya dunia.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Kama leo kutafanyika uchunguzi wa maoni ulio huru, salama na wa kiuadilifu duniani, basi walimwengu watathibitisha kwa wingi mkubwa kuwa hakuna serikali inayoweza kuishinda ya Marekani kwa kuchukiza ulimwenguni.

Aidha ametoa majumuisho ya mazungumzo yake kuhusu jambo hilo akisisitiza kwa kusema: Hivyo suala la kupambana na ubeberu wa kiistikbari na maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari wa Kimataifa, ni suala la kimsingi kabisa lililotokana na uchunguzi na uchanganuzi sahihi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa nasaha kwa vijana nchini Iran kuwa na uchanganuzi mzuri, sahihi na wa kina kuhusiana na suala la kupambana na ubeberu na kuongeza kuwa: Vijana wa mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu hawakuwa na haja ya kuwa na uchanganuzi kuhusu suala la kupambana na Marekani kwani dhulma na ukandamizaji wa Marekani na uungaji wa dola hilo la kibeberu kwa utawala katili wa kitaghuti uliokuwa ukitawala nchini Iran wakati huo, waliuona kwa uwazi kabisa, lakini vijana wa leo wanapaswa kufanya utafiti na wanahitaji wapate ufafanuzi sahihi wa mambo kuhusu ni kwa nini taifa la Iran linapinga uistikbari na misimamo ya Marekani na sababu za taifa la Iran kuichukia Marekani ni nini?

Baada ya hapo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha nukta nyingine kadhaa muhimu na za kimsingi kuhusu masuala yanayoendelea hivi sasa kati ya Iran na Marekani. Sambamba na kuunga mkono timu ya viongozi wa Iran inayofanya mazungumzo na kundi la 5+1 na kusisitiza kuwa: Hao ni wana wa Mapinduzi ya Kiislamu ambao wametumwa na Jamhuri ya Kiislamu kwenda kufanya kazi hiyo na wanafanya jitihada kubwa katika kufanikisha kazi hiyo nzito, hivyo, mtu yeyote hapaswi kuwadhoofisha, kuwadharau au kudhani kuwa ni watu wenye nia ya kuliletea madhara taifa.

Ayatullah Udhma Khamenei aidha amesema kuwa, mazungumzo ya Iran na nchi sita ambapo Marekani imo katika nchi hizo ni kwa ajili ya kadhia ya nyuklia tu na si kwa jambo jengine na kuongeza kuwa: Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Iran haitopata madhara kutokana na mazungumzo hayo, bali taifa la Iran litapata tajiriba na uzoefu ndani ya mazungumzo hayo kama ilivyopata uzoefu katika kusimamisha kwa muda urutubishaji wa urani katika miaka ya 2003 na 2004 uzoefu ambao uliongeza uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo wa watu wetu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo na kuongeza kuwa, muongo mmoja uliopita, mazungumzo ya Iran na Ulaya yalikuwa na namna fulani ya kulegeza misimamo, kusitisha baadhi ya kazi na kwa aina fulani yalikuwa ya kutwishwa mambo lakini baada ya kupita miaka miwili ya kusimamisha na kuacha kazi zetu nyingi, watu wote walifahamu kuwa hata kwa kuchukua hatua zote hizo, kamwe hakuwi na matumaini ya kupatikana ushirikiano mzuri kutoka kwa nchi za Magharibi.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa, lau kama tusingelifanya vile, kuna uwezekano baadhi ya watu wangelidai kuwa, kama mtarudi nyuma japo hatua moja tu basi mambo yote yatatatuka na faili la nyuklia la Iran litakwenda kwenye mkondo wake wa kawaida, lakini uzoefu uliopatikana katika kusimamisha kwetu kwa muda kazi zetu za nyuklia kuliwafanya watu wote waelewe kuwa, upande wa pili unaokabiliana nasi, una malengo na shabaha nyingine na wanatumia kadhia ya nyuklia kama kisingizio tu, na ndio maana tuliamua kuendelea mbele na kazi zetu.

Aidha amesema, hali ya leo ya Iran katika suala zima la nyuklia inatofautiana kikamilifu na ilivyokuwa miaka 10 iliyopita na sambamba na kutangaza uungaji mkono wake kamili, wa kweli na mkubwa kwa timu ya Iran inayofuatilia masuala ya hivi sasa na Marekani, ameongeza kuwa: Mimi sina mtazamo mzuri na wala sina matumaini na mazungumzo yanayoendelea hivi sasa, (kati ya Iran na Marekani) kwani haijulikani iwapo mambo yanayotarajiwa na taifa yatapatikana au la, lakini tunaamini kuwa, tajiriba na uzoefu huo ni mzuri kwa sharti kwamba tuwe macho na tujue ni kitu gani kinaendelea.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewalaumu vikali baadhi ya watu wanaofanya propaganda zenye mtazamo finyu au wa kupinga tu mambo bila ya sababu yoyote na kusema kuwa, kuna baadhi ya watu wanatumia vyombo vya habari vya maadui kufanya njama za kuwapotosha wananchi na kujaribu kuonesha kuwa, kama tutasalimu amri kuhusu kadhia ya nyuklia, basi matatizo yote yaliyopo, ya kiuchumi na mengineyo, yatatatuka.

Ametoa hoja za kubatilisha propaganda hizo kwa kutoa ushahidi wa njama za Marekani na mipango yake ya kiuadui dhidi ya Iran hata kabla ya kujitokeza kadhia ya nyuklia ya Iran na kuwataka wananchi wote hususan vijana wa Vyuo Vikuu na wa daraja mbali mbali za elimu nchini kutaamali vizuri na kuwa na muono mpana kuhusu suala hilo.

Ayatullah udhma Khamenei ameuliza maswali kadhaa akisema: Je, mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu wakati Marekani ilipoiwekea vikwazo Iran na kuendelea na vikwazo vyake hivyo dhidi yetu, je, wakati huo kadhia ya nyuklia ilikuwepo? Je, wakati Wamarekani waliposhambulia ndege ya abiria ya Iran na kuwaua kwa umati wasafiri 290 waliokuwemo kwenye ndege hiyo, kulikuwa na kisingizio kinachoitwa nyuklia? Je, pale mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wakati Wamarekani walipofanya njama za mapinduzi ya kijeshi ya kambi moja ya kijeshi, lilikuwepo suala la nyuklia? Je, uungaji mkono wa kila namna wa kisilaha na kisiasa wa Marekani kwa makundi ya wapinzani wa Mapinduzi ya Kiislamu baada ya ushindi wa mapinduzi hayo ulitokana na miradi ya nyuklia ya Iran?

Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia majibu ya hapana ya maswali hayo na kusisitiza kuwa: Hivyo suala la nyuklia linatumiwa kama kisingizio tu. Ametoa mfano mwingine akisema, hata kwa mfano tujaalie kuwa siku moja tumelegeza kamba na kurudi nyuma na kadhia hiyo ya nyuklia imetatuliwa, basi bila ya shaka yoyote mabeberu watatafuta kisingizio kingine cha kuifanyia uadui Iran yetu azizi, watatafuta makumi ya visingizio vingine kama vile maendeleo yetu ya makombora, upinzani wa taifa la Iran kwa utawala wa Kizayuni, uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu kwa muqawama n.k.

Baada ya kutoa hoja hizo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Wamarekani wanaifanyia uadui Jamhuri ya Kiislamu kwa sababu taifa la Iran limekataa matakwa yao na linaamini kuwa Marekani haiwezi kufanya upuuzi wowote dhidi ya taifa la Iran.

Amesema, kimsingi Marekani inapinga uwepo wa Jamhuri ya Kiislamu yenye ushawishi, nguvu na yenye mfumo wa utawala unaochaguliwa na wananchi.

Maneno haya yanaowana kikamilifu na matamshi ambayo yametolewa na mmoja wa wanasiasa na wanafikra wa Marekani aliyesema wazi wazi na bila ya kificho kuwa, Iran itaendelea kuwa hatari, ni sawa tu iwe na atomiki, au isiwe na atomiki, kwani ina ushawishi na nguvu au kama wanavyoiitadai hao maadui, kuwa mamlaka na satua ya Iran inatawala katika eneo (la Mashariki ya Kati).

Ayatullah Udhma Khamenei ametoa majumuisho ya mazungumzo yake kuhusu suala hilo akisisitiza kuwa: Kadhia ya nyuklia ni kisingizio tu kinachotumiwa na Wamarekani na kwamba uadui wa Wamarekani dhidi ya Iran utaisha pale itakapoona taifa la Iran limetengwa, halina itibari na halina hadhi wala heshima yoyote.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea na hotuba yake kwa kuzungumzia umuhimu wa kutegemea nguvu na uwezo wa ndani akilitaja jambo hilo kuwa ndio utatuzi wa kweli wa masuala na matatizo yaliyopo na kuongeza kuwa: Wakati taifa linapotegemea nguvu na uwezo wake lenyewe, kamwe haliwezi kutetemeshwa na hamaki na vikwazo vya adui na sisi tuna wajibu wa kupigania kulifikia lengo hilo.

Ameongeza kuwa: Maneno yetu yote ambayo tumekuwa tukiwaambia viongozi wa hivi sasa na wa huko nyuma ni kuwa, wanapaswa kutegemea uwezo wa kila namna na mkubwa wa nguvu kazi ya watu, wa kimaumbile na wa kijiografia wa Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesisitiza kuwa, harakati za kidiplomasia nazo ni jambo la lazima na kuongeza kuwa, kutegemea nguvu za ndani hakuna maana ya kuachama na harakati za kidiplomasia lakini inabidi kuzingatia kuwa harakati za kidiplomasia ni sehemu tu ya kazi na kwamba mhimili mkuu na wa kimsingi ni kutegemea nguvu za ndani na ni uwezo huo mkubwa wa ndani ndio unaoweza kuleta nguvu, hadhi na itibari katika meza ya mazungumzo.

Kiongozi Muadhama wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile amewataka wananchi na viongozi nchini Iran kuzingatia nukta hii muhimu kwamba, katika kukabiliana na maadui, tangu awali ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi hivi sasa kamwe Iran haijawahi hata mara moja kukata tamaa na kulazimika kwenda kumpigia magoti mtu yeyote yule na kwamba katika siku za usoni pia hali itakuwa hiyo hiyo.

Ayatullah Udhma Khamenei ametoa sababu za yeye kusema maneno hayo akibainisha kwamba: Sisi katika muongo wa kwanza wa Mapinduzi, hatukuwa na vitu vingi sana muhimu vya kimaada ikiwa ni pamoja na fedha, silaha, uzoefu, mipangilio mizuri na jeshi lenye nguvu wakati ambapo kambi inayopambana na Mapinduzi ya Kiislamu yaani utawala wa Kibaath wa Saddam na madola makubwa ya Magharibi na Mashariki yaliyokuwa yakimuunga mkono Saddam yalikuwa katika upeo wa juu wa nguvu na uwezo, lakini pamoja na hayo walishindwa kulipigisha magoti taifa la Iran.

Amesema: Hivi sasa hali ya Iran na hali ya kambi inayokabiliana nayo ina tofauti kubwa sana ikilinganishwa na miaka hiyo ya mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, kwani hivi sasa tena Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshapiga hatua kubwa za kielimu, kiteknolojia, kisilaha na itibari na heshima ya kimataifa na tayari ina mamilioni ya vijana wenye vipaji vya kila namna walio tayari kulitumikia taifa lao, wakati ambapo katika upande wa kambi inayokabiliana na taifa hili, yaani Marekani na washirika wake, wamekumbwa na matatizo mengi ya kisiasa, kiuchumi pamoja na ugomvi na hitilafu za kila namna.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, mizozo ya kisiasa ndani ya Marekani kwenyewe, mfano wa wazi ukiwa ni mzozo wa hivi karibuni uliopelekea kwenda likizo ya lazima serikali na kushindwa serikali ya Marekani kufanya kazi kwa muda wa siku 15, pamoja na matatizo mengine makubwa ya kiuchumi, nakisi na upungufu wa mapato ya mabilioni ya dola, mizozo mizito baina ya Marekani na nchi za Ulaya na masuala mengine mbali mbali ikiwa ni pamoja na suala la shambulizi la kijeshi dhidi ya Syria ni mifano ya hali mbaya iliyoikumba kambi inayokabiliana na taifa la Iran na kusisitiza kuwa: Leo hii taifa la Iran liko macho, limeelimika, lina nguvu na lina maendeleo makubwa, na kamwe haliwezi kufananishwa na lilivyokuwa miaka 20 au 30 iliyopita.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Tab’an madola hayo yataendelea kuliwekea mashinikizo taifa la Iran lakini tunapaswa kuvumilia na kuyavuuka mashinikizo hayo kwa kutegemea nguvu zetu za ndani.

Vile vile kwa mara nyingine amesema kuwa anaunga mkono hatua na jitihada zinazofanywa na serikali na viongozi nchini Iran katika upande wa kidiplomasia na mazungumzo kama haya yanayoendelea hivi sasa baina ya Iran na kundi la 5+ na kuongeza kuwa, Hatua ya hivi sasa ni ya kupata tajiriba na uzoefu na yumkini ikawa ni kazi yenye matunda mazuri. Amesema, Kama matunda mazuri yatapatikana hilo ni jambo zuri, lakini kama matunda mazuri hayakupatikana maana yake itakuwa ni kwamba inatubidi tujitegemee wenyewe katika kutatua matatizo yetu.

Wakati huo huo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Hapa napenda kutoa tena nasaha nilizowahi kuzitoa huko nyuma kwamba hatupaswi kuziamini tabasamu zinazotolewa na adui.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Nasaha zangu kwa maafisa wanaofanya juhudi zao kwenye uwanja wa kidiplomasia na mazungumzo ni kwamba kuweni macho msije mkapumbazwa na tabasamu za kilaghai za adui na hivyo kukufanyeni mutelee na mwende kombo.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Viongozi nchini Iran wanapaswa kufuatilia kwa kina na kwa tahadhari kubwa matamshi na mitazamo inayotolewa na upande wa pili. Wakumbuke kuwa watu wa upande huo kwa upande mmoja wanatoa tabasamu na vicheko na kuonesha kuwa wanapenda mazungumzo lakini katika upande wa pili hapo hapo utawasikia wanasema, machaguo yote yako juu ya meza kwa ajili ya kukabiliana na Iran, sasa ni ghalati na upuuzi gani wanataka kuufanya, haijulikani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia matamshi ya mwanasiasa mmoja wa Marekani aliyetaka kutumiwe silaha za nyuklia kushambulia Iran na kusema kuwa: Kama Wamarekani ni wakweli katika madai yao kuwa ni wanalipa uzito mkubwa suala la mazungumzo, basi wanapaswa kuifunga midomo ya hawa watu wanaoropoka na kupayuka mambo yasiyo na msingi.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Serikali ambayo ina njozi na ndoto kama hizo za kwamba ndiyo iliyobeba jukumu la masuala ya dunia na masuala ya nyuklia, inajidanganya kudhani kuwa inaweza kuzitisha nchi nyingine kuwa itatumia nyuklia dhidi yao.

Ameongeza kuwa: Leo hii, kutokana na serikali ya Marekani na Congress ya nchi hiyo kudhibitiwa na mabepari wenye nguvu na makampuni ya Kizayuni yenye ushawishi mkubwa ndani ya Marekani, Wamarekani wanalazimika kuuonea muhali utawala wa Kizayuni, na maskini wengine kama wao pia wanalazimika kuwazingatia Wazayuni katika maamuzi yote hayo, lakini sisi Iran hatuna wakati wa kuwaonea muhali Wazayuni.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Sisi tangu siku ya kwanza kabisa tulisema, hivi sasa pia tunasema, katika siku za usoni aidha tutasema, kwamba sisi tunauona utawala wa Kizayuni kuwa ni utawala usio halali na ni mwana wa haramu.

Vile vile ameashiria kuweko macho na welewa wa wananchi na viongozi wa Iran na kusema kuwa: Sisi tunaunga mkono hatua yoyote inayochukuliwa na viongozi wa nchi yetu kwa ajili ya maslahi ya nchi lakini napenda kuwapa nasaha hizi wananchi na viongozi wetu na hasa vijana kwamba daima yawekeni wazi kikamilifu macho yenu kwani njia pekee ya kuweza kufikia malengo ya taifa ni kuwa macho na kuwa wetambuzi wazuri wa mambo.

Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Ni matumaini yangu kuwa kwa uwezo na taufiki ya Mwenyezi Mungu, vijana wataichukua nchi kwa moyo wa furaha na bashasha kubwa na kuifikisha kwenye vilele vya juu kabisa vya ustawi na maendeleo kwa ubunifu wao mzuri.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on November 6, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: