FADHILA ZA ZIYARA ASHURAA

3-b

Hebu tuangalie Riwaya ambazo zinaonyesha na kuashiria Umuhimu na uhalali wa akisoma Ziyara Ashura.

Riwaya ya Kwanza (1)

Alqamah bin Mohammed bin Hazrami (ra) anasimulia “nilimuomba Imamu Baqir (as) kunifundisha Dua nitakayoisoma siku ya Ashura baada ya kumaliza kusoma Ziyaarat ya Imamu Husein (as) karibu kaburi lake au kutoka mbali na kaburi lake”. Imamu (a.s) akajibu:

“O Alqamah, wakati wowote utakapotaka kusoma Ziyaarat ya Imamu Hussein (as), kwanza Swali rakaa mbili kisha geuka kuelekea kaburi la Imamu Hussein (as) na wakati ukiwa unanyooshe kidole kuelekea huko, kwanza sema “Salam” kisha “Takbir” Baada ya hapo, soma Ziyaarat hii (Ziyarat Ashura). Kama utafanya hivyo, basi utakuwa ni kama vile unasoma dua iliyosomwa na Malaika wanapotemebelea kaburi la Imam (as). Aidha, wakati wewe unasoma Ziyaarat hii:

a)      Mwenyezi Mungu atakunyanyua daraja yako mara milioni moja zaidi.

b)     Na utajumuishwa pamoja na watu wale ambao walikuwa mashahidi pamoja na Imamu Hussein (as),

c)      Na siku ya Hukumu, utafufuliwa pamoja na Mashahidi, na

d)     Utapata ujira wa Mitume wote (as) ambao walitembelea kaburi la Imamu Hussein (as) kutoka siku aliuawa mpaka leo.

Na namna ya kusoma Ziyaarat yenyewe ni kama hivi…”(Kisha Imamu (as) akamsomea Alqamah Ziyarat Ashura yote) (al- Kaamil Ziyaarat, Ibn Qulawayh, Sura ya 71. Uk.194).

Mwisho wa Riwaya hii, Imam Baqir (as) anasema:

“Ewe Alqamah, kama unaweza, basi soma Ziyaarat hii kila siku kupeleka salamu kwa Imamu Husein (as) na utapata fadhila (sawa na mwenye kuisoma siku ya Ashura).”

Riwaya ya Pili (2)

Imamu Sadiq (as) anasema: “Mtu ambaye atatembelea kaburi la Imamu Hussein (as) katika siku ya Ashura au kukesha usiku karibu na kaburi lake (as), basi ni sawa na ambaye amepata Shahada pamoja nae (Imam Hussein) “. (Al-Kaamil Ziyaarat, Sura ya 71, Uk. 191) (Aina nyingi za Ziyaaraat zimetajwa kuwa zinaweza kusomwa siku ya Ashura. Lakini Ziyaarat iliyotajwa na Janab Safwan (ra) ni maarufu zaidi na ni katika Hadith Qudsi).

Riwaya ya Tatu (3)

Imamu Sadiq (a.s) amesema kuwa:

“Mtu ambaye atafanya Ziyaara ya Imamu Hussein (as) katika siku ya Ashura, hakika pepo ni wajibu juu yake.” (Al-Anwaar Behaar, Juz. 101, Uk.104)

 

Riwaya ya Nne (4)

Imamu Sadiq (a.s.) anasema:

Mtu ambaye atatembelea kaburi la Imamu Hussein (as) akijua haki yake (ya Uimamu) basi ni kama amefanya ziara ya kumzuru Mwenyezi Mungu katika Arsh.” (Al-Kaamil Ziyaarat, Sura ya 71, Uk. 192.)

Riwaya ya Tano (5)

Abdullah bin Fazl anasimulia, “Siku moja nilikuwa mbele za Imamu Sadiq (as) wakati mtu kutoka katika mji wa “Tuusi” alikuja kumtembelea (as). Na kuuliza “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww)! Una nini cha kusema kwa mtu ambaye atatembelea kaburi la Aba Abdillah (as) katika siku ya Ashura?”

Imamu (a.s) akasema:

“Oh Tuusi mtu ambaye atatembelea kaburi la Aba Abdillah (as) wakati akitambua kuwa utii wake kwa Imamu ni wajibu utokao kwa Mwenyezi Mungu! Atasamehewa dhambi zake zote ziliyopita na zijazo. Na atapewa nafasi ya kuwaombea watu sabini (70) wenye Madhambi. Na hakutakuwa na dua atakayoiomba kutoka kwa Mwenyezi Mungu karibu na kaburi la Aba Abdillah (as) isipokuwa itakubaliwa.” (Bihaar al- Anwaar, Juz. 101, Uk. 23).

Kwa kuwa tunajadili juu ya maisha ya mtukufu wa tano kati watu watakatifu wa nyumba ya Mtume (a.s), kwa hapa tutatosheka na masimulizi ya riwaya hizi Tano (5). Kwa wale watakaohitaji kuingia kwa undani zaidi katika mada hii wanaweza kurejea katika “Kamil al-Ziyaarat, Bihaar al- Anwaar Juzuu ya 101, Thawaab al- A’ Maal na “Shifa al- Sudur “.

Kama tutazingatia na kutafakari juu ya Riwaya hizo hapo juu, tutatambua miujiza na Athari zilizomo katika kusoma ziyarat Ashura. Riwaya hizi pia zinabeba ushuhuda wa ukweli wa matukio yaliotokea hapo awali.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on November 8, 2013, in Habari na Matukio and tagged , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings