HOTUBA YA MUHESHIMIWA AL-ALLAMAH AL-QADHI AS-SAYYID OMAR IBN AHMAD IBN SUMAIT AL-ALAWI. ALIYOITOA KATIKA UFUNGUZI WA HAFLA YA KUMBUKUMBU YA MAUAJI ALIYOFANYIWA IMAM HUSAIN (A.S.)

image

HOTUBA YA MUHESHIMIWA AL-ALLAMAH AL-QADHI AS-SAYYID OMAR IBN AHMAD IBN SUMAIT AL-ALAWI. ALIYOITOA KATIKA UFUNGUZI WA HAFLA YA KUMBUKUMBU YA MAUAJI ALIYOFANYIWA IMAM HUSAIN (A.S.) KUMBUKUMBU HIYO ILIFANYIKA MJINI ZANZIBAR TAREHE 21 MUHARRAM 1361 A.H SAWA NA TAREHE 8 FEBRUARY 1942

Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu, na tunaziomba rehma na amani zake zimshukie Mtume Muaminifu, na ziwashukie watu wa nyumba yake, Masahaba zake na wafuasi wake wema.

Ama baada ya shukurani na salamu, Mwaka wa sitini na moja B.H. ndani ya mwezi kama huu, Umma wa Kiislamu uliingia khofu na mila yake nayo ilitetereka na kuingia dosari. Uongozi wa Umma ukabadilika baada ya kuuawa kwa kipenzi cha waumini na bwana na mashahidi Husain mwana wa Imam Ali ibn Abi Talib r.a

Usiku huu wa leo ni mara ya kwanza katika Historia kwa Mashia Ithnaasharia wa hapa Zanzibar kuadhimisha karne ya kumi na tatu tangu tukio hilo baya lilipotokea. Na ni kwa mara ya kwanza pia wao kuwaalika ndugu zao miongoni mwa Waislamu wa mji huu ili washirikiane nao katika makusudio haya matukufu, kama ambavyo mimi binafsi wameniomba nizungumze japo kidogo kumuhusu bwana wetu Husain a.s. Kwa hakika mimi nimejizuwia kuzungumzia tukio hili kama lilivyo kwa ufafanuzi kutokana na mazingira ya kihistoria yaliyonilazimisha kufanya hivyo. Kwa upande wangu nimechagua kukubainishieni wale watu walioutendea uovu Uislamu na Mtume wa Uislamu pamoja na Husain ambaye ni kipenzi cha Mtume s.a.w.

Hapana shaka kwamba watu hao waliwanyanganya watu wa nyumba ya Mtume s.a.w nguvu na uwezo wa kuhukumu pale (watu hao) walipojipatia wafuasi wengi duniani na wafuasi wao wakawa wengi. Si hivyo tu bali waliwahamasisha watu mhamasisho uliopelekea watu wa nyumba ya Mtume s.a.w na wafuasi wao watambulikane kwa jina la Mashia, kitu ambacho siyo cha ajabu kwani waislamu wengi ni Mashia (wafuasi) wa nyumba ya Mtume s.a.w na hujisikia uchungu kutokana na misiba iliyowafika.

Hebu msikilize Imam Al- Busari anasema. “Mashahidi wawili hawanisahaulishi siku ya Karbala kutokana na msiba uliowapata. Basi tafadhali walilie kiasi unachoweza.

Nitakutoshelezeni Masikio yenu baada ya kusikia usemi huu kwamba, Sababu zilizopelekea mashia wa nyumba ya Bw. Mtume s.a.w wawe wengi ni dhulma, ujeuri na mateso yaliyowafika. Kwa hakika mnyonge hata akawa mnyonge vipi lakini hawezi kukosa watu wa kumtetea kila mahali.

Amma chanzo cha Ushia na sababu za kudhihiri kwake kilianzia kile kipindi cha mwaka wa thelathini na tano hijiriyyah wakati Banu Umayyah wliposimama kupora ukhalifa kutoka kwa Bani Hashim wa kutaka kuupokonya toka mikononi mwa Imam Ali (k.w).

Matokeo ya hali hiyo ni kuvunjika kwa umoja wa Waislamu na kuanguka kwa mahusiano ya kidugu yaliyokuwepo miongoni mwao.

Mimi naamini ninyi hamna haja nikwambieni kwamba, “Udugu ndiyo msingi uliojenga umoja wa Waislamu kiasi kwamba mambo yao waliheshimika ulimwenguni na nguvu zao ziliimarika na kamwe unyonge haukuwasogelea isipokuwa baada ya kuukosa umoja huo ambao mara nyingi sana bwana Mtume s.a.w. aliusisitiza mno katika maneno yake.

Mpaka hapa inapasa nihitimishe maneno yangu na sote tumuelekee Mwenyezi Mungu tukaugonge mlango wa mema yake na ukarimu wake ili awarudishie umoja wa Waislamu kama ulivyokuwa hapo awali, na amlinde mfalme wetu Maulana Sayyid Khalifa ibn Habibu, kisha ampe umri mrefu pamoja na hekima na tawfiq katika shughuli zake zote.

Wasalam alaikum warahmatullahi wabarakatuh.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on November 9, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: