UTUKUFU WA IMAM HUSSEIN BIN ALI BIN ABI TALIB (A.S.)

image

Imamu Hussein ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewatoharisha na kuwatakasa na machafu kama ilivyo katika Qur’ani Tukufu Sura ya 33:33. Imepokewa kutoka kwa Ummu-Salama (mke wa Mtume) kwamba ilipoteremka Aya hii ya utakaso (33:33) ndani ya nyumba yangu, nikiwa mlangoni pamoja na Mtume na Ali, Fatimah, Hassan na Hussein pamoja na Malaika Jibril na Mikail wakiwa ndani ya nyumba yangu, nilisema:-

“Ewe Mtume! Je! Mimi si katika Ahlul –Bayt wako?. Mtume (s.a.w.w.) akasema,” Hakika wewe Ummu Salama u katika kheri na wewe ni katika wake za Mtume (s.a.w.w.). Rejea: (Durrul Manthur- Juzuu ya 6, Uk. 604-605. na Tafsiri Tabari Juzuu ya 10, Uk. 298 na Tafsiri Ibn Kathir Juzuu ya 3, Uk. 531).

Iliposhuka Aya ya Mawaddatul-Kurba (Sura ya 42:23), Mwenyezi Mungu alimwambia Mtume (s.a.w.w.) katika Qur’an tukufu awaambie Ummah wake hivi:- “Qul laa as-alukum alayhi ajran il-lal Mawaddata fil-Qurbaa” waambie siwataki malipo yoyote juu ya (Utume niliokuja nao) ila mapenzi juu ya Aqraba wangu (42:23). Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa, hawa Mawaddatul-fil Kurba (Aqraba) ni nani na akajibu ni watu wa nyumba yake yaani Ahlul-Bayt. Aya hii inaweka wazi kuwa kuwapenda Ahlu-Bayt wa Mtume ni wajibu usio shaka juu ya kila Muislamu. Rejea: (Tafsiri Ibn Kathir Juzuu ya 4, Uk. 121-123. na Fathul Qadiir Juzuu ya 4, Uk. 760. na Tafsiri Tabari Juzuu ya 11, Uk. 142-145. na Durrul Manthur- Juzuu ya 7, Uk. 348-349.).

Ilipoteremshwa Aya ya kuapizana yaani “Mubahala” alipoambiwa Mtume (s.a.w.w.) Sema; Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu na wake zetu na wake zenu na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuapizane. Mtume alitoka na Sayyidna Imam Hassan na Imam Hussein (watoto wake) Bibi Fatima (mke wa Imam Ali bin Abi Talib), Mtume (s.a.w.w.) na Sayyidna Imam Ali (Nafsi zetu). Makafiri wa Najran walipomuona Mtume (s.a.w.w.) na nyuso za wale watukufu na watoharifu Ahlul-Bayt wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) walikataa kuapizana na badala yake walikubali kulipa jizya (kodi). Rejea: (Ruhul-Maan J. 2 Uk. 180-181. na Fadhul-Qadiyr J. 11 Uk. 524. na Durrul- Manthur J. 2 Uk. 232-233.).

Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Mola! Mimi nampenda Hussein nawe mpende, Hussein anatokana na mimi na mimi ninatokana na Hussein, umpende mwenye kumpenda (Hussein)”. Rejea: (Sahih Muslim J. 4 Uk. 1293.). Na vile vile Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hasan na Hussein ni mabwana wa vijana wa Peponi, anipendae awapende hawa wawili”. Rejea: (Sawaiqul Muhriqa Uk. 522.).

Kuwasalia Aali Muhammad ni nguzo ya Sala na kuacha kuwasalia wao ni kuibatilisha Sala. Rejea: (Sawaiqul Muhriqa Uk. 147.).

Pia amesema Bwana Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Mfano wa Ahlul Bayt wangu kwenu ni mfano wa Safina ya Nabii Nuh (a.s.) waliopanda Safina hiyo waliokoka na wale waliokataa kupanda Safina hiyo waliangamia.” Rejea: (Sawaiqul Muhriqa Uk. 150.).

Na mwisho ni kauli ya Imam Shafi aliposema: “Ikiwa dhambi yangu ni kuwapenda watoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) [Imam Hassan na Imam Hussein] basi ni dhambi ambazo sitatubia”.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on November 9, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: