MUHTASARI WA MAJIBU WA VIPEPERUSHI VILIVYOSAMBAZWA

Ashukuriwe allah mwingi wa rehema mwenye kurehemu, ziada na rehema na amani ziwe juu ya kipenzi chake Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbanikwake watukufu. Haya ni majibu muhtasari kwa walokuja tuhumu na kuongelea suala
ambalo ni nyeti katika pande mbili (Mashia na Masunni) kwa madai ya kua Mashia wapambia batili kuwa haki!

Majibu ya vipeperushi vilosambazwa tutajibu kama ifuatavyo:

  1. Mashia waitakidi kuwa Imam Ally (AS) ni maasum yaani hawafanyi kosa kubwa wala kosa dogo

lengo la maneno haya ni kwamba; Kila alobeba majukumu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) lazima awe ni maasum kwa kuwa yeye ndiye alochukua nafasi yake (s.a.w.w) baada yake, akili ya hukumu kuwa kila Nabii lazima awe maasum
kulingana na mzigo alobeba Nabii huyo, vivyo hivyo akili yakubali kuwa atakaechukua nafasi hiyo lazima awe kama yeye
. Kama upande wa Sunni wanapinga kuwa anaekuja baada ya Mtume atakiwi kuwa na sifa kama za mtume basi upande washia sivyo hivyo.

  1. SUALA LA KUMUOZESHA IMAM ALLY (AS) MTOTO WAKE UMMU KULTHUM KWA OMAR (RA) ITAJIBIWA KWA NUKTA MBILI ZIFUATAZO;

Wapokezi wa hadith wanamatatizo ya upokezi.

 • Walopokea hadith hii upande wa Masunni ni; IBN SAAD (TABAQATUL KUBRA, JUZ 8, UK 462.) ALKHATIB ALBAGHDADI (TARIKHUL BAGHDADI, JUZ 6, UK 182.) IBN ATHIR (USUDUL GHABA, JUZ 5, UK 614)
 • IBN HAJAR AL-ASQALANI (AL-ISABA, JUZ 4, UK 492.) na wengine wengi kama HAKIM NAISHABURI, BAIHAQI NA IBN ABDULBAR na..
 • La ajabu ni kwamba SAHIH BUKHARI NA SAHIH MUSLIM hadith hii haikupokelewa, na kuna baadhi ya hadith kuwa hazipo ndani ya vitabu hivyo (SAHIH BUKHARI NA SAHIH MUSLIM) hupingwa,
 • aidha MUSNAD AHMAD NA MUSNAD IBN ABII YAALAA haikupokelewa!!! Pia Vitabu SITA SAHIHI kwa upande wa Masunni haikupokelewa hadith hii
 • BAIHAQI asema wapokezi wa hadith hiyo ni MADHAIFU HAWAKUBALIWI HADITH ZAO, REJEA TAHDHIBU TAHDHIB JUZ 11, UK 382, JUZ 1, UK 44, JUZ 8, UK 27, JUZ 4, UK 106.
 • Na vitabu vyengine kama; MIZANUL ITIDAL JUZ 4, UK 334, TARIKHUL BAGHDADI JUZ 13, UK 472, WADHOOFISHA WAPOKEZI WA HADITH HIYO.
  1. MANENO YA HADITH.
   • Watu waliposikia kuwa Omar (RA) ataka kumuowa Mtoto wa Ally (AS) walishangaa na Omar (RA) aliwajibika kuwaeleza watu lengo la kumuowa Binti huyo kwa kusema: nilimsikia mtukufu mtume (s.a.w.w) akisema: kila kizazi kitatoweka isipokua kizazi cha huyu akiashiria kwa ally (as). Hii ndiyo sababu ya kwanza kutaka kumuowa Binti wa Ally (AS).
   • Katika hadith hiyo pia yaeleza kuwa Ally (AS) alitowa udhuru kwa Mtoto wake kuwa bado ni mgodo, na kueleza kuwa binti yake yupo tayari kwa ajili ya Watoto wa Jaafar (RA).
   • Baadhi ya wapokezi wa hadith waeleza kwamba: IBN SAAD NA KHATIB ALBAGHDADI katika Vitabu vyao walieleza kuwa; kipindi ambacho Omar (RA) alimtaka Ally (as) kumuoza Binti yake, ally (AS) alimtuma Ummu Kulthum Kitambaa Msikitini ili Omar (RA) kama atavutiwa na Binti yule, alipoingia na Kitambaa kile Omar (RA) alimpandisha nguo yake hadi kuonekana muundi wake. IBN ATHIR asema: Baada ya Omar (RA) kumpandisha nguo alimshika kwenye paja lake (Ummu Kulthum). DAULABI nae alisema: Baada ya kumpandisha nguo hiyo
   • alimkumbatia (Ummu Kulthum). Ila Sheikh ALHAKIM NAISHABURI NA BAIHAQI hawakupokea maneno kama hayo. Na IBN JAUZI asema: si vyema kunasibishwa maneno hayo kwa omar (ra), kwa kuwa wamekubaliana waislamu wote kuwa hairuhusiwi kumshika mwanamke ambaye waweza kumuowa ndani ya msikitini.
   • Kama kweli kulikuwa na ndoa baina ya Ummu Kulthum na Omar (RA) walikuwa na watoto wangapi?!!…
   • baadhi ya riwaya zaeleza kuwa walipata mtoto mmoja aitwa ZAID…Riwaya zengine watoto wawili RUQAIYA na ZAID…SHEIKH NAWAWI katika Kitabu chake cha TAHDHIBUL ASMAA WA LUGHAT alikuwa na watoto wawili Fatima na Zaid…watoto hao kuna tofauti hadi hii leo.
   • Hata katika kifo chake kuna tofauti na siku ya kuzikwa na aliemsalia ni nani!! Baadhi yao wasema alisaliwa na SAAD IBN ABII WAQAS au HASAN NA HUSEIN au ABDALLAH IBN OMAR au SAID IBN AL-AAS. Ajabu mtoto gani asiye fahamika na Baba yake ni mmoja katika Maswahaba wa kubwa na maarufu wa Mtume (S.A.W.W)!!! Hata siku ya kufariki na aliyemsalia hafahamiki!!.
   • Kwanini izungumzwe siku ya kuowa Omar (RA) ila siku ya kufariki haifahamiki? yote ni kutokana na kuwa habari ya kuolewa Ummu Kulthum inautata ndani yake.
  1. Kuolewa Ummu Kulthum na Omar (RA) kwa upande wa Mashia waelezwa kwa mfumo kama ufuatao:

Kuolewa Ummu Kulthum na Omar (RA) ni suala la kisiasa ambalo Omar (RA) alitumia ili kufumba macho
suala la Ukhalifa (Uongozi baada ya Mtume) na kulazimisha Ally akubali kumuoza Ummu Kulthum na Ally akamuakilisha ndugu yake Abbas kuwa msimamizi wa ndoa hiyo, Ummu Kulthum alifariki kabla ya Omar (RA)
na Omar (RA) hakuweza hata siku moja kukutakana na Ummu Kulthum kutokana alikuwa na umri mdogo… na suala kuwa na mtoto upande wa Shia limekanushwa na kupingwa kutokana na riwaya.

  1. Madai ya kusema imekuwaje ally (AS) amuozeshe mtoto wake kwa Omar (RA) ilihali ya kuwa Omar (RA) ni kafiri?!!

Jibu lake ni kwamba; Ally (AS) kumuoza mtoto wake kwa Omar (RA) si kinyume na Isma la hasha kwani kuna manabii waloowa wake wasokuwa wema kama Nabii Nuh (AS) na Lut (AS) sembuse Ally (AS) ambaye si Nabii, pia kuozeshwa Omar (RA) haimaanisha kuwa Ally (AS) hana ugomvi na Omar la hasha Hadith zaeleza kuwa Omar (RA) alilazimisha kuowa ndio maana Ally (AS) alilazimika kumuoza Omar (RA).

 • Madai, kukanusha ugomvi baina ya Bi Fatima (AS) na Omar (RA) na Abubakar (RA)

Ni kitu kilichokuwa wazi kihistoria… Swali; kama kweli kulikuwa hakuna matatizo baina ya Bi Fatima (AS) na Omar na Abubakar,
kwanini leo kaburi la Bi Fatima (AS) halifahamiki sehemu lilipo?! ilihali ya kuwa yeye alifariki baada ya miezi sita ya kifo cha Baba yake Mtume (S.A.W.W)!!,
aidha ushahidi tunao kuwa Bi Fatima(AS) alifariki akiwa na ghadhabu kali kunako mambo walofanya Abubakar na Omar… ushahidi wa maneno ni; SAHIH BUKHARI, JUZ 3, UK 1126, HADITH 2926. SAHIH BUKHARI, JUZ 4, UK 1549, HADITH 3998. SAHIH BUKHARI, JUZ 6, UK 2474, HADITH 6346.

 • Madai ya kutowa baiya Ally (AS) kwa Abubakar

Sio SAHIHI kutokana na ushahidi wa Hadith kuwa Ally (AS) na Banii Hashim baada ya kufariki Bi Fatima (AS) hawakutowa baiya.. KITABU cha IHQAQUL HAQ, JUZ 1, UK 121….Kwanini
twashadidia (twakazania) kusema baiya ya Ally kwa Abubakar tu, kusahau kwamba baada ya kufariki Mtume (S.A.W.W) Abubakari na Omar hawakushiriki katika mazishi ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W)!!! kwanini suala hilo pia lisizungumziwe hadharani watu walijuwe?!! na madai ya kuwa Abubakari na Omar walikuwa ni watu wa karibu ya Mtume (S.A.W.W)
je! Ukaribu ni kipindi cha uhai wa Mtume tu?!

 • Ukafiri wa Muawiya

hakuna shaka ndani yake, Waislamu wote wakubaliana kuwa Mtume alimuombea dua mbaya Muawiya baada ya Mtume alivyomwita Muawiya akamjibu mwambieni ninakula Mtume(S.A.W.W) alisema: ALLAH ASISHIBISHE TUMBO LAKE.

 • Baiya ya HASAN(AS)
  kwa MUAWIYA

ilikuwa ni mkataba wasuluhu wa kisiasa walokubaliana kua MUAWIYA akifariki kabla ya HASAN(AS) uongozi utarejea kwa HASAN(AS), na kama HASAN(AS) atafariki kabla ya MUAWIYA basi uongozi utakwenda kwa HUSEIN(AS) baada ya MUAWIYA…Kutokana na kwenda kinyume na suluhu na mkataba huo, MUAWIYA alifanya njama za kumuuwa HASAN(AS) ili utawala na uongozi amkabidhi mtoto wake YAZID (alolaaniwa na Allah), kwa hilo MUAWIYA alifanikisha kumuuwa HASAN(AS) na utawala na uongozi akampa mtoto wake YAZID na
ndio maana HUSEIN(AS) hakukubaliana na hayo alikuwa dhidi ya YAZID kwa kuwa YAZID alikuwa ni MUOVU, FASIQ NA KAFIRI kama Baba yake, Hatimae YAZID (laana za Allah ziwe juu yake) alimuuwa HUSEIN(AS)
mjukuu kipenzi wa Mtume(S.A.W.W).

 • Ally (AS) kuwa na watoto wenye majina kama ABUBAKAR, OMAR na UTHMAN,

Tunajibu kama ifuatavyo;

 1. Mtoto wa Ally(AS) mwenye jina la Abubakar, Jina hilo la Abubakar halikuwa jina lake bali ni KUNIA yake
  jina lake lilikuwa ni MUHAMMAD ASGHAR … na KUNIA hiyo haikuwa ABUBAKAR tu bali alikuwa na KUNIA nyingine
  ya UBAIDULLAH..rejea KITABU MUUJAM RIJALUL HADITH, JUZ 12, UK 88.
 2. Mtoto wa Ally aitwae Omar sio Ally alimwita Omar bali Omar mwenyewe ndiye alimwita Omar kutokana na mtoto huyo alizaliwa siku alozaliwa Omar…rejea KITABU SIRAT AALAMU NUBALAA, JUZ 4, UK 134.
 3. Mtoto wa Ally(AS) kuitwa UTHMAN; sio UTHMAN IBN AFAAN KHALIFA WA TATU la hasha jina hilo ni jina la ndugu yake
  alikiitwa UTHMAN IBN MADH-UN na ndio maana akaitwa UTHMAN…rejea KITABU MAQATILU TALIBIN, JUZ 1,UK 23
 • Ally (AS) kukalia kimya UKHALIFA wa ABUBAKAR

Haimaanishi kuwa Ally (AS) alikuwa atambuwi kuwa yeye ni kiongozi kutoka moja kwa moja kwa Mtume(S.A.W.W)
bali alikaa kimya kwa kuhifadhi maslahi ya Uislamu…rejea VITABU, MUSNAD ABII DAUD, JUZ 4,UK 470, HADITH 2875.
MUSTADRAK ALAA SAHIHAIN, JUZ 3, UK 134. Ushadi ni mwingi wa kuthibitisha uongozi wa Ally (AS).

 • Ghaiba ya Imam wa kumi na mbili

si kwa Mashia tu, na Imam wa kumi na mbili si wa Mashia tu ni
wa Waislamu wote, ushahidi rejea VITABU, SAHIH BUKHAR NA SAHIH MUSLIM MLANGO WA KUSHUKA NABII ISSA(AS).

HUU NI MUHTASARI WA MAJIBU WA VIPEPERUSHI VILIVYOSAMBAZWA NA WATU WASOTAMBUA USHIA, KILA SUALA
LILOZUNGUMZIWA KATIKA VIPEPERUSHI HIVYO MENGI NI MADAI TU YASOKUWA NA DALILI, KAMA KUONGELEA QURAN YA IMAM ALLY(AS) ILIKUWA KAMA TAFSIRI YA QURAN ALIANDIKA NA KUPANGILIA KILA SURA NA AYA KUTOKANA NA
MUDA ILOSHUKA AYA NA SURA, QURAN YA LEO NI RIWAYA HAFSI KUTOKA KWA AASIM NA NI QIRAA NA SI ILE QURAN YA IMAM ALLY(AS), KWA HIYO MADAI HAYO HAYANA NAFASI KWANI NI MADA MBILI TOFAUTI KWA WABOBEZI WA
ELIMU YA ULUMIL QURAN. KWAMANTIKI HII KWA KILA ATAKAETAKA ZUNGUMZIA MASUALA KAMA HAYA LAZIMA AWE AMEJITOSHELEZA KIELIMU KUONGEA VITU BILA USHAHIDI WOWOTE ULE.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on December 6, 2013, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: