Kiongozi Muadhamu Aonana na Viongozi wa Mfumo wa Kiislamu na Wageni wa Mkutano wa Umoja wa Kiislamu

image

19/01/2014
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo (jumapili) ameonana na majimui ya viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wageni walioshiriki katika Mkutano wa Umoja wa Kiislamu, na makundi mbali mbali ya wananchi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na mjukuu wake mtukufu, Imam Jaafar Sadiq AS.
Katika mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaka ulimwengu wa Kiislamu kufanya juhudi kubwa za kufanikisha malengo matukufu ya ujumbe wa Mtume wa Mwisho, Bwana wa Mitume na kusisitiza kuwa: Leo hii suala muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu ni umoja na kwamba licha ya kuwepo njama nyingi sana, lakini mustakbali wa umma wa Kiislamu unatoa bishara njema kupitia umoja na mshikamano, welewa wa mambo na mwamko wa Kiislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa sikukuu hii adhimu ya kukumbuka kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW na kuzaliwa Imam Jafar Sadiq AS na kukutaja kujiweka mbali na ndoto na kuwa na mawazo yasiyotegemea uhakika wa mambo na baadaye kufanya jitihada za kujikomboa kutokana na dhulma na ukandamizaji wa tawala za kidikteta na kuunda serikali ya kiadilifu ni mbinu mbili zinazotumiwa na Uislamu kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu na kuongeza kuwa: Mataifa ya Waislamu yanapaswa kuleta ukombozi wa ndani wa kifikra na kufanya jitihada za kujiletea ukombozi wa kisiasa, kuleta tawala za wananchi, kusimamisha demokrasia ya kidini na kufanya harakati kwa msingi wa Sharia za Kiislamu ili kwa njia hiyo waweze kufikia kwenye ukombozi wa kweli unaokusudiwa na dini tukufu na azizi ya Kiislamu.
Vile vile amezitaja njama na hatua zinazochukuliwa na maadui wa Uislamu kwa ajili ya kuzuia kupatikana umoja wa kweli na saada na ufanisi wa umma wa Kiislamu kuwa ni njama tata na zenye upeo na sura nyingi na kuongeza kuwa, kuzusha mizozo na mifarakano kati ya Waislamu ndio msingi mkuu unaotumiwa katika njama za waistikbari.
Ayatullah Udhma Khamenei amezitaja njama za miaka 65 sasa za maadui wa Uislamu za kujaribu kuisahaulisha kadhia ya Palestina na kuwabebesha Waislamu utawala pandikizi na ghasibu wa Kizayuni ambao unafanya kila aina ya jinai dhidi ya Waislamu kuwa ni mfano mwingine wa njama za kiukandamizaji za Marekani na mabeberu wengine duniani na kuongeza kuwa: Vita vya siku 33 huko Lebanon, vita vya siku 22 na vile vya siku nane vya huko Ghaza vimeonesha kuwa, ukitoa baadhi ya tawala ambazo kivitendo zimegeuka kuwa walinzi wa malengo ya mabeberu, mataifa ya Waislamu yako macho na yameuhifadhi utambulisho na uwepo wa Palestina na wanaendelea kutoa vipigo hivi na vile kwa utawala wa Kizayuni na waungaji wake mkono.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, unapoyaangalia kwa upana masuala ya ulimwengu wa Kiislamu utaona kuwa, kukumbwa na mghafala umma wa Kiislamu na kujaribu kuufanya uisahau kadhia ya Palestina ni moja ya malengo makuu yanayowafanya maadui wa Uislamu wazushe vita vya ndani, wachochee mizozo na hitilafu na waeneze fikra za kuchupa mipaka na za kitakfiri za kuwaona Waislamu wengine ni makafiri.
Aidha ameelezea kusikitishwa sana na suala hilo na kuongeza kuwa, kuna baadhi ya watu wanashikilia fikra za kitakfiri za kuwakufurisha Waislamu wengine badala ya kuelekeza nguvu zao katika kupambana na utawala khabithi wa Kizayuni na wanatumia jina la Uislamu na Sharia za dini hiyo tukufu kuwahesabu Waislamu walio wengi kuwa ni makafiri na kuandaa uwanja wa kuzusha vita na machafuko na mizozo na ni kwa sababu hiyo ndio maana kuwepo makundi ya aina hiyo kunawafurahisha mno maadui wa Uislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria aya tukufu ya 29 ya sura ya 48 ya al Fath ambayo sehemu yake moja inasema:
أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ
…wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao… na kuongeza kuwa: Makundi na mirengo ya kitakfiri inadharau amri hiyo ya wazi ya Mwenyezi Mungu na yanawazozanisha Waislamu kwa kuwagawa baina ya makundi mawili ya Waislamu na makafiri na kuwafanya Waislamu waingie vitani kupigana wao kwa wao.
Vile vile amehoji kwa kusema: Kwa kuzingatia hali hii hivi kuna mtu yeyote anaweza kubakiwa na shaka kuwa, kuwepo makundi hayo na uungaji mkono wa kifedha na kisilaha yanayopata makundi hayo si kazi ya mashirika ya kiusalama na khabithi ya madola ya kibeberu na vibaraka wao?
Ayatullah Udhma Khamenei kwa kuzingatia uhakika huo ameitaja mirengo na mkundi ya kitakfiri kuwa ni hatari kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na ameziusia nchi za Kiislamu kuwa macho sana mbele ya makundi hayo.
Ameongeza kwa kusema: Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya tawala za Waislamu hazishughulishwi na madhara ya kuyaunga mkono makundi hayo na hazielewi kuwa kuna siku moto waliouwasha utawageukia wao wenyewe na kuwateketeza.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezitaja njama za kuchochoa na kushadidisha mivutano na hitilafu kati ya Waislamu wa Kisuni na Kishia na kuchochea mapigano ya wenyewe kwa wenywe kwenye mataifa ya Waislamu katika kipindi cha miaka mitatu minne iliyopita, kuwa ni radiamali ya mabeberu wa dunia ya kukabiliana na suala la kuongezeka mwamko wa Kiislamu katika baadhi ya nchi.
Ameongeza kuwa: Mabeberu wanafanya njama za kujaribu kufifiliza na kuufunika mwamko wa Kiislamu kwa kuwagombanisha Waislamu wa madhehebu tofauti na baadaye kuvikuza kupinduka vitendo viovu na vichafu vinavyofanywa na magenge ya kitakfiri kama vile kutafuna tafuna maini mabichi ya watu waliouawa ili kupotosha mafundisho matukufu na ya asili ya Kiislamu katika fikra za walimwengu, na kujaribu kuionesha dini hii ya Mwenyezi Mungu kuwa inafundisha ukatili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Ni jambo lisilo na shaka hata kidogo kuwa, mambo haya hayakuzuka kwa ghafla moja bali madola ya kibeberu duniani yamechukua muda mrefu kuyaandalia mazingira na mikakati ya kutokea kwake.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kupambana na jambo lolote lililo dhidi ya umoja na mshikamano wa Kiislamu kuwa ni jukumu kubwa na zito kwa Waislamu wote wa Kishia na Kisuni na wa madhehebu mengine ya Kiislamu na kusisitiza kwamba: Watu wenye ushawishi na vipaji vya kisiasa na kielimu na kidini wana jukumu zito la kuleta umoja na mshikamano katika jamii za Waislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka Maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu kuwatahadharisha Waislamu kuhusu hatari za hitilafu na mizozo ya kimadhehebu. Amewataka wasomi wa Vyuo Vikuu kubainisha umuhimu wa malengo ya Kiislamu kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kama ambavyo amewahimiza watu wenye ushawishi wa kisiasa katika umma wa Kiislamu kutegemea uungaji mkono wa wananchi na kujiweka mbali na mabeberu na maadui wa Uislamu akisisitiza kuwa: Leo hii jambo muhimu zaidi kuliko yote katika ulimwengu wa Kiislamu ni mshikamano na kuwa kitu kimoja.
Vile vile ameashiria namna mataifa ya Waislamu yanavyotoka pole pole chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa wakoloni na kutahadharisha kuwa: Waistikbari na mabeberu wamekusudia kulinda manufaa yao ya kipindi cha ukoloni na ubeberu wa moja kwa moja kupitia ubeberu usio wa moja kwa moja wa kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi. Ayatullah Udhma Khamenei amekutaja kuwa macho na kuwa na welewa wa kina wa mambo kuwa ndiyo njia pekee ya kuweza kupata saada na ufanisi umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Kuwa na suhula nyingi sana, kuwa katika eneo bora la kijiografia, urithi mwingi wa kihistoria na wenye thamani kubwa sana pamoja na vyanzo visivyo na kifani vya kiuchumi vilivyoko katika nchi za Kiislamu vinaweza kutumiwa kuwaletea heshima, utukufu na hadhi ya kipekee Waislamu chini ya kivuli cha mshikamano na kuwa kitu kimoja.
Vile vile ameutaja ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuzidi kupata nguvu sifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuwa kigezo bora kwa mataifa mengine licha ya kupita miaka 35 ya njama mbali mbali za mabeberu kuwa ni katika dalili za bishara njema kwa umma wa Kiislamu na kusisitiza kuwa: Kwa baraka na msaada wa Mwenyezi Mungu, taifa la Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unazidi kupata nguvu siku baada ya siku, unazidi kuimarika na unazidi kuwa madhubuti.
Mwishoni mwa mkutano huo, Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonana kwa na kuzungumza kwa karibu na wageni waalikwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Kiislamu.
Kabla ya hotuba hiyo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Hasan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa maadhimishio ya Maulidi ya Mtume wa Mwisho SAW na Imam Jafar Sadiq AS na ameashiria kiza totoro cha kiutamaduni, kijamii na kisiasa kilichokuwa kimetanda katika kipindi cha ujahilia na kuongeza kuwa: Ni katika kipindi hicho kilichojaa masaibu mengi ndipo Nabii wa rehma alipozaliwa na kuijaza historia ya mwanadamu nuru ya uongofu na usafi na ukweli.
Rais Rouhani amegusia pia matatizo na hitilafu zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema kuwa, ni jambo lisilo na shaka kuwa hivi sasa Mtume wa Uislamu anateseka kutokana na watu wapotofu na watu walioamua kufuata njia ya misimamo mikali ya kitakfiri ya kuwakufurisha Waislamu wengine na kwamba jamii za Kiislamu zinapaswa kwa mara nyingine kusimama imara kumsaidia Nabii wao wa rehma.
Rais Rouhani amekutaja kufuata mwito wa umoja na mshikamano uliotolewa na Imam Khomeini (quddisa sirruh) kuwa ndiyo njia pekee ya kuuokoa umma wa Kiislamu na kuongeza kkuwa: Dini moja, Mtume mmoja, manufaa ya pamoja, maadui wa pamoja na malengo kama vile Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni pamoja na Quds azizi ni mambo ambayo yanaweza kuwaunganisha Waislamu.
Rais Rouhani ameongeza kuwa: Umma wa Kiislamu unapaswa kushikamana na Qur’ani Tukufu chini ya kivuli cha tadibiri, busara, misimamo ya wastani, matumaini na kufanya juhudi bila ya kuchoka ili kuufufua tena ustaarabu wa Kiislamu.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on January 26, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: