Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Waziri Mkuu wa Uturuki

29/01/2014
20140129Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, leo jioni (Jumatano) ameonana na Waziri Mkuu wa Uturuki na kusisitiza kuwa, uhusiano wa kiudugu, kimapenzi na kiurafiki ulioimarika zaidi katika karne za hivi karibuni baina ya Iran na Uturuki ni uhusiano wa aina yake kabisa na kuongeza kuwa: Nchi hizi mbili zina maeneo mengi sana ya kuweza kuimarisha ushirikiano baina yao na kwamba jambo hilo limezidi kuandaa uwanja mzuri wa kuweza kutia nguvu na kupanua ushirikiano wa pande hizo mbili kwa kiwango kikubwa sana.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa, ni jambo la dharura sana kwa Tehran na Ankara kulipa uzito wa hali ya juu suala la utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika safari ya Bwana Ordogan mjini Tehran na kusisitiza kuwa: Kupewa uzito wa aina hiyo jambo hilo kutapelekea kuimarika zaidi uhusiano na kuongezeka kasi ya ushirikiano baina ya pande mbili.
Vile vile amekumbushia mielekeo na mfungamano wa ndani ya nyoyo uliopo baina ya mataifa mawili ya Iran na Uturuki na kuongeza kuwa: Inabidi fursa na nafasi muhimu zinazotokea mara kwa mara zitumike vizuri na kwa njia sahihi.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Uturuki, Bw. Recep Tayyip Erdogan sambamba na kuwasilisha salamu nyingi za Rais na wananchi wa Uturuki amesema kuwa, anaihesabu Iran kuwa ni nyumbani kwake kwa pili.
Aidha Waziri Mkuu wa Uturuki amesema kuwa, mazungumzo yake ya leo na Rais Hassan Rouhani na viongozi wengine wa Iran yalikuwa mazuri na yenye faida nyingi na huku akiashiria kutiwa saini hati kadhaa za maelewano baina ya nchi mbili amesema: Ni matumaini yangu kuwa uhusiano wa nchi hizi mbili utazidi kustawi na kuimarika na kuwa kigezo kizuri kwa ajili ya eneo hili na dunia nzima kiujumla.
Vile vile Bw. Ordogan amelitaja suala la kutiwa saini hati ya Baraza Kuu la Ushirikiano wa Iran na Uturuki kuwa ni hatua muhimu sana na kuongeza kwa kusema kuwa: Tutatumia vikao vya mara kwa mara vya pande mbili kuimarisha uhusiano wetu na kuufikisha katika kiwango ambacho itaonekana kana kwamba mawaziri wa nchi hizo mbili wanafanya kazi na kujadiliana mambo yao katika baraza moja la pamoja la mawaziri.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on February 5, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: