BAKWATA SEHEMU YA KWANZA

Na Mohammed Said

Sehemu ya Kwanza

Mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) wa Mwaka wa 1968

Kutokana na katiba ya mwaka wa 1957 lengo kuu la EAMWS ilikuwa ni kuutangaza Uislam katika Afrika ya Masharikií. EAMWS yenyewe ilikuwa ikijigamba kuwa uti wake wa mgongo ilikuwa ni tabligh, yaani utangazaji wa dini.  Jumuiya hii iliyoanzishwa mwaka 1933 ilikuwa ya Waislam wa mataifa yote katika uanachama na katika uongozi wake. Katika uhai wake wa miaka thelathini na tano EAMWS ilijiweka mbali sana na siasa. Jumuiya hii ilishughulikia kuutetea na kuueneza Uislam katika Afrika ya Mashariki. Lakini baada ya kutokea maasi ya Tanganyika Rifles mwaka 1964 yaliyopelekea viongozi wengi wa Kiislam kuwekwa kizuizini, EAMWS ikawa imepoteza mwelekeo wake na kudhoofika. Baadhi ya matawi yaliyokuwa katika majimbo yakafungwa kwa woga na kukosa viongozi thabiti na kwa matawi mengine yalifungwa kwa sababu viongozi wake walkuwa wakichimbwa chinichini na serikali. Waislam wengi walihisi vitisho vya serikali kwa hiyo waliogopa kuchukua uongozi wa EAMWS. Wengi waliogopa kuitumikia EAMWS kwa kuwa walihisi ofisi za jumuiya hiyo zilikuwa zikichukuliwa na serikali kama vituo vya upinzani dhidi yake. Kwa zaidi ya miaka mitatu toka ule mkutano wa mwaka 1963, EAMWS haikuweza kufanya mkutano wowote.

EAMWS ilipokuja kuitisha mkutano wake wa mwaka mjini Arusha mwaka 1966 kikajitokeza kikundi kutoka upande wa Tanzania kikidai EAMWS ijigawe, kila nchi iwe na mamlaka yake na ijitegemee yenyewe, yaani Tanzania, Kenya na Uganda zote ziwe mbalimbali. Kikundi hiki kilichokuwa kikidai utengano vilevile kikadai kuwa katiba ya EAMWS nayo iwe ya ëkizalendoí Hii ilikuwa na maana kuwa uongozi itabidi iifanyie katiba marekebisho ili kuiwezesha Tanzania kuwa huru ndani ya EAMWS. Wajumbe waliokuwa wanaona mbali kutoka Tanzania na wengine kutoka Kenya na Uganda, na kwa hakiaka mkutano mzima kwa ujumla walipinga kitendo hicho, wakidai kuwa kwa kufanya hivyo Waislam wa Tanzania watakuwa wametengwa na umma wa Kiislam wa Afrika ya Mashariki. Jambo hili likitokea, si tu litakuwa limewadhoofisha Waislam wa Tanzania peke yao, bali Waislam wa Afrika ya Mashariki nzima. Wajumbe wa Kenya na Uganda walikuwa wanatambua kuwa kulikuwa na shinikizo kubwa kutoka serikali ya Tanzania kwa Watanzania kujitoa kutoka EAMWS. Halikadhalika ilikuwa inafahamika kuwa wajumbe wa Tanzania walikuwa wakifanya kazi chini ya shinikizo kali kutoka serikali ya Nyerere.

Haikuwa siri sana kuwa baadhi ya viongozi wa EAMWS walikuwa kisirisiri wakiandamwa na serikali. Lakini mkutano ule haukuzungumzia matatizo haya kwa kuwa hayo yalichukuwaliwa kama matatizo ya ndani ya nchi. Hata hivyo kwa ule moyo wa Kiislam wa kuhurumiana, wajumbe wa Kenya na Uganda kwa faragha walionyesha masikitiko yao kwa Tewa kuhusu ile hali iliyokuwa ikiwakabili Waislam wa Tanzania. Wajumbe walipokuwa wakiondoka kurejea makwao, ilikuwa wazi kuwa serikali ya Tanzania ilikuwa ikiingilia kati EAMWS kiasi cha kuifanya jumuiya hiyo ishindwe kufanya kazi yake vyema na kupitisha maamuzi yake. Hali hii ilijidhihirisha wazi pale kwa kipindi kizima cha mkutano, makachero wa serikali walikuwa wamejitokeza kwa wingi mjini Arusha.

Haukupita muda ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia Waislam wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo. Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru. Ieleweke hapa kuwa kama tulivyokwisha eleza hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzani ilikuwa mikononi mwa Wakristo na watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa. Hii ilikuwa na maana kuwa kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislam ambayo Kanisa itaweza kuiamuru. Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislam kama nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa. Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa mgogoro wa EAMWS ambao ulidumu kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.

Ilituweze kuuelewa vyema kisa kizima cha ëmgogoroí ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika ëmgogoroí ule. BAKWATA SEHEMU YA KWANZA
BAKWATA

Ilituweze kuuelewa vyema kisa kizima cha ëmgogoroí ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika mgogoro ule.
Mwisho, ni muhimu kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha TANU na vyombo vya dola katika ëmgogoroí ule. Hii itasaidia kuelewa kama kweli ulikuwepo ëmgogoroí katika EAMWS, au ëmgogoroí ulibambikizwa na watu katika TANU, serikali na ndani ya Waislam wenyewe ili kuwadhoofisha Waislam kwa nia ya kuwa usije Uislam ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislam kushika madaraka ya nchi.

Mwaka wa 1967 Mwalimu Julius Nyerere alitangaza Azimio la Arusha hatua ambayo iliitia Tanzania katika siasa ya ujamaa. Sera hii mpya ya uchumi ilipokelewa vyema na wananchi. Mtu ambae hata alikuwa hajulikani, tena mwalimu wa shule ya msingi akijulikana kwa jina la Adam Nasibu ambae alikuwa katibu wa Bukoba wa EAMWS, alichukua nafasi hii kwa kuongoza maandamano hadi ofisi ya TANU ya Mkoa kumuunga mkono Mwalimu Nyerere na sera yake mpya ya uchumi ya Azimio la Arusha. Adam Nasibu inasemekana kuwa alisema ujamaa ni sawa na mafundisho ya Qurían Tukufu. Adam Nasibu hakuishia hapo alikwenda mbele zaidi na kutoa ëmiongozo kwa viongozi wote wa Kiislam wa Bukoba akifafanua Azimio la Arushaí.  Wasiokuwa Waislam walimuona Adam Nasibu kama Muislam mwenye mwamko mzuri wa kimaendeleo, na kwa kuwa yeye alikuwa ni kiongozi wa EAMWS, kuunga kwake mkono Azimio la Arusha kulionekana kama kitendo rasmi cha jumuiya hiyo kuunga mkono sera hiyo. Lakini kabla ya yeye kufanya haya, hakuna mtu aliyemjua mwalimu huyu wa shule kama mwanasiasa licha ya kuwa msomi mwenye uwezo wa kuchambua mambo.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on February 16, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: