BAKWATA SEHEMU YA PILI

Na Mohamed Said
Sehemu ya Pili

Katika hali ya kawaida, uongozi wa EAMWS pale makao makuu Dar es Salaam ungelikasirishwa kidogo na kitendo cha Adam Nasibu cha ushabiki wa siasa. Lakini uongozi wa EAMWS haukumuonya kiongozi wake wa Bukoba kuhusu jambo lile ambalo dhahiri halikuwa la kupendeza katika jumuiya. Bila shaka uongozi wa EAMWS ulichelea kuwa kwa kufanya hivyo wangelionekana si uzalendo, hasa ukiichukulia jinsi wananchi walivyohamasika na Azimio la Arusha. Hata hivyo Waislam siku zote ndiyo waliokuwa mbele katika kuongoza siasa. Makao Makuu walibaki kimya kama vile hakuna kilichotokea. Funika kombe mwana haramu apite.

Tofauti na mwaka wa 1963 wakati Nyerere alipojaribu kufanya mapinduzi dhidi ya uongozi wa EAMWS, mwaka wa 1967 hali ya mambo yalikuwa yamebadilika sana yakimwendea Nyerere vyema. Serikali ilikuwa imedhibiti vyombo vyote vya habari ukiondoa gazeti la The Tanganyika Standard ambalo bado lilikuwa chini ya Lonrho. Nyerere alikuwa amemuweka Martin Kiama kama mkurugenzi wa radio ya taifa, na Benjamin Mkapa kama mhariri wa magazeti mawili ya TANU, The Nationalist na Uhuru. Adam Nasibu aliandikwa katika magazeti na habari zake kutangazwa katika radio kwa ajili ya kitendo chake, hasa kuhusu yale maneno aliyosema kuwa ujamaa ni sawa na mafundisho ya Qurían. Katika hali ya mambo kama yalivyokuwa wakati ule hasa jinsi uhasama ilivyokuwapo baina ya serikali na Waislam, baadhi ya Waislam walimuona Adam Nasibu kama kibaraka anaetafuta umaarufu wa bure kwa kujipendekeza kwa TANU, Nyerere na serikali yake. Juu ya haya yote kile kitendo cha katibu wa Bukoba wa EAMWS kitakuja kuwaathiri vibaya jumuiya hiyo na uongozi wake wote pamoja na Mufti Sheikh Hassan Bin Amir.

Kwa wengine Adam Nasibu alionekana kama mzalendo na Muislam mwenye ëuoni wa mbalií. Kwa ajili hii basi serikali ikamuoana kama kiongozi wa baadae ambayo ingeweza kumtegemea wakati wa shida. Uongozi wa EAMWS makao makuu ukaonekana haupo pamoja na wananchi, wala haujali shida zao na uko mbali sana na sera za serikali. Lakini kwa hakika EAMWS kama taasisi ya dini isingeliweza kujitokeza na kuunga mkono Azimio la Arusha kwa kuwa hayo yalikuwa mambo ya siasa. Kwa kufanya hivyo ingelikuwa inakwenda kinyume na msimamo wake wa kutojiingiza katika siasa. Kwa zaidi ya robo karne toka iasisiwe EAMWS ilikuwa imejiweka mbali sana na mambo ya siasa ikishughulika na masuala ya Uislam tu. Hata hivyo kuwa nje ya Azimio la Arusha kukaonekana kama kitendo cha kukosa uzalendo na kutoa picha kuwa jumuiya hiyo ilikuwa haijali maendeleo na ustawi wa watu wa Tanzania. Mambo yakawa yamevurugika zaidi kwa kuwa rais wa EAMWS, Tewa Said na makamo wake Bibi Titi Mohamed walikuwa katika baraza la mawaziri la Nyerere na wakapoteza nyadhifa zao za ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1965. Kwa ajili hii basi serikali ikawa inaeneza propaganda kuwa kwa kuwa Tewa na Bibi Titi walikuwa katika uongozi wa juu wa EAMWS, walikuwa wanatumia nafasi zao kujijengea himaya mpya kutoka kwa Waislam dhidi ya Nyerere. Viongozi hawa ikawa lazima washughulikiwe na kuangamizwa. Mtu wa kufanya kazi hii hakuwa mwingine ila Adam Nasibu katibu wa EAMWS Bukoba, mwalimu wa shule ya msingi ambae elimu yake wala haikuwa kubwa. Adam Nasibu alikuwa tayari keshafanikiwa kufanya mapinduzi dhidi ya rais wa EAMWS, Tewa Said Tewa. Kutokana na vitendo vyake alikuwa ameidhihirishia serikali kuwa yeye angeweza kuwa mtumishi bora kwa dola kuliko ule uongozi wa EAMWS uliokuwa pale makao makuu Dar es Salaam ambao ulikuwa ukionekana umechoka.

Wakazi wa Dar es Salaam kila mwaka walikuwa wakifanya maulidi katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW). Huu ndiyo toka asili ulikuwa uwanja ambao TANU ilifanya mikutano yake yote wakati wa kupigani uhuru. Mwezi Juni 1968 maulidi mbili katika usiku mmoja zilisomwa kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume (SAW). Maulidi moja ilisomwa Mnazi Mmoja na nyingine Ilala. Chanzo cha haya yote ni kuwepo kwa kutoelewana kati ya viongozi wa Waislam waliokuwa wanajiona kuwa ni ëwazalendoí wafuasi wa TANU na wale na wale viongozi wa EAMWS ambao kambi nyingine ilikuwa ikiwaona kama wapinzani wa TANU. Yale maulidi yaliyosomwa Ilala yalihudhuriwa na viongozi wa EAMWS na yalipata watu wengi na yakafana sana ukilinganisha na yale maulidi ya Mnazi Mmoja, ya wafuasi wa TANU. Uongozi wa TANU ulitishika na hali hii iliyokuwa ikijitokeza kwa maana ilikuwa inaonyesha kuwa chama kilikuwa kinapoteza wafuasi ambao walikuwa wakijiunga na kambi ya Tewa na Titi iliyokuwa ikisemekana ipo dhidi ya Nyerere.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on February 17, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. 1 Comment.

  1. Hello admin, i see your page needs fresh articles.
    Daily updates will rank your blog in google higher, content is king nowadays.
    If you are to lazy to write unique posts everyday you should search in google for:
    Ightsero’s Essential Tool

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: