Sayyid Hassan: Tutashinda Mapambano haya dhidi ya Makundi ya Kukufurisha (Takfiri)

Na Abuu Hassanain

Sayyed_martyr_leaders (1)Katibu mkuu wa Hizbullah Sayyed Hasan Nasrallah ametoa hotuba ya Televisheni Jumapili ya Tarehe 16/02/2017 iliyorushwa moja kwa moja na Televisheni ya Almanar, katika kilele cha maadhimisho ya kila Mwaka ya “Viongozi Mashahidi” na katika hutuba yake amezungumzia hali ya Maendeleo inayojiri ya ndani na ya kikanda, na kwa kuanzia aliainisha vitisho vinavyoendelea vya Israel.

Sayyed Nasrallah katika kilee cha kumbukumbu ya Viongozi Mashahidi  aligawanya hotuba yake katika sehemu tatu, ya kwanza ilikuwa juu ya Adui Israel na tishio lake linaloendelea dhidi ya Lebanon, Pili ni kuhusu mapambano ya Hezbollah awamu ya sasa, na Tatu ilikuwa kuhusu changamoto za harakati ya Mapambano katika masuala mbalimbali.

Baada ya kutoa Salamu na kuzitakia Rehema Roho za viongozi Mashahidi, Na Mashahidi katika harakati ya mapambano, Mashahidi katika Jeshi, na wananchi waliouawa katika milipuko ya mabomu ya kutegwa ya Kigaidi hivi karibuni, Nasrallah aliashiria kuwa “tumefikia hali ambayo watu hawataki kabisa kutanzua mgogoro wa Palestina na na kumshughulikia Adui,” na akasema kuwa” hapo ndipo hamu ya Marekani ilipo.”

Sayyed Nasrallah alisema kuwa “Utawala Marekani kwa kushirikiana pamoja utawala ghasibu ya Wazayuni wanataka, kukomesha kabisa sababu za kutetea mapambano ya  Palestina, na wanaona kuwa huu ndio wakati muafaka kwa kuwa kwa Mataifa ya Kiarabu na Kiislamu dunia leo hayapo macho, kila nchi imegubikwa na matatizo yake yenyewe. “

Sayyed Nasrallah aliwakumbusha Walebanoni kwa umuhimu wa pekee juu ya tishio la adui huyu ambae amekua aghalabu akitishia mustakbali wa kisiasa, Kijeshi, Kiuchumi, na Nishati ngazi zote, na alisisitiza kuwa “Wajibu wetu ni kuilinda Lebanon, Matukufu na uwezo wake, na si kuicha ikabiliane na hatima yake …”

Aliashiria kuwa “Laiti kama si harakati ya Mapambano ya Hizbullah, Lebanon ingebakia ikikaliwa kwa mabavu na Israel, Na kusisitiza kuwaa “tunapaswa kufahamu kuwa Israel bado ni adui na tishio,” na kwamba “katika wiki chache zilizopita Israel imejaribu kutumia fursa hiyo kuanzisha mapambano na uhalifu dhidi ya harakati ya Mapambano na katika Makaazi  yetu … Kwani bado macho yao yangali katika nchi na mafuta yetu na bado Israeli inaiona Hezbollah kama hatari kubwa katika kanda.”

Katibu mkuu wa Hezbollah alikiri kwamba “Israel haitutishi na haiathiri Ari yetu, na ni lazima wajue kwamba harakati ya mapambano ya Hizbullah ipo katika utayari wa hali ya juu na wakati wote.”

Alizidi kusema kuwa ana matumaini  ya “kuwa na Serikali yenye uwezo na  Jeshi lenye nguvu ambalo litakuwa ndio tegemeo la pekee kuilinda lebanon,” na kuthibitisha kuwa “itakapofikia hapo ndipo tutapumzika.”

Kitishio cha Makundi ya Kukufurisha…

Sayyed Nasrallah alisisitiza kuwa tishio la Pili baada ya hili la Adui Israel, ni hofu ya Ugaidi wa Makundi ya Kukufurisha (Takfiri), na la kuzingatiwa ni kwamba “Mfumo huu wa Ukufurishaji (Takfiri) wenyewe kama mfumo sio tishio na kama utaendelea kubakia katika mawanda ya Akili, lakini tatizo lipo katika dhana ya kumpinga na kumkataa kila mtu, wao wanapinga kila itikadi, Siasa, au akili, hivyo hutaka kumuondoa na kumuangamiza kila asiye katika mfumo wako.”

Alisema kuwa “tishio hili la Wakufurishaji (Takfiri) lipo katika eneo la kanda nzima katika mfumo wa makundi ya waasi ambao hutumia kanuni ya kimantiki ya kumuangamiza kila asiye katika mfumo wao, hutumia kanuni hiyo hata katika hata ndani ya uga za Kiislamu, Iwe ni dhidi ya Madhehebu mengine au dhidi ya Madhahebu ya Sunnis ambao hawakubaliani nao.” Sayyed Nasrallah aliashiria kile kinachoendelea katika  vita ya sasa kati ya “Daesh” na “Al- Nusra Front” kama mfano, unaonyesha kwamba “zaidi ya wapiganaji 2,000 kutoka sehemu zote mbili wameuawa, na mashambulizi kadhaa ya kujitoa Muhanga yamefanywa  na Magari ya kutegwa bomu yamelipuliwa… fahamu kuwa makundi yote mawili yana itikadi moja, lakini kwa kuwa hawakukubaliana kisiasa, hivyo ruhusa kuuana.”

“Je, makundi haya yenye silaha yamefanya nini kwa watu Algeria na “Wafalme” wa harakati zao wenyewe?” Aliuliza, na kuongeza: “Hebu na tutizame uzoefu wa Afghanistan Makundi ya Waafghani walimpiga mvamizi Msoviet na jeshi lake kubwa lenye nguvu, kisha baada ya Msovieti kuondoka, baadhi ya vikundi vya kukufurisha (Takfiri) vikajingiza katika vita ya wenyewe kwa wenyewe na kuuawa watu zaidi ya wale waliouwawa na Jeshi la Urusi…”

Katibu mkuu huyo alisisitiza kwamba “Lebanon ni shabaha ya makundi ya kukufurishana (Takfiri) na ni sehemu ya mradi wao, na kipaumbele chao ilikuwa ni kuja Lebanon baada ya kumaliza Syria, hii ndio sababu kwa nini waliamua kutumia mkakati wa kudhibiti mipaka ya Lebanon na Syria. Hii ndio itikadi yao, na kwa kuwa  Wamarekani na Israel ni washirika wa makundi haya, hivyo shabaha yao ni kuilenga Lebanon na ni jambo la uhakika kwa sababu ya uwepo wa harakati ya Mapambano ya Hizbullah, ambayo ni tishio kubwa kwa  Israeli.”

Alisema kuwa “kulikuwa na majadiliano hapa Lebanon kuhusiana na milipuko na mashambulizi ya kujitoa Muhanga, na baadhi walisema kwamba hili lisingetokea kama si kwa ushiriki Hizbullah huko Syria. Wao wamechagua mantiki hii ya utetezi ambayo itaendelea hata baada ya sisi kuwa washirika katika serikali hiyo.”

Sayyed Nasrallah katika kilele cha kukumbuka Viongozi Mashahidi katika hatua hii, Sayyed Nasrallah alionyesha mshangao wake na kusema: “Kabla ya kwenda Syria, hivi Lebanon haikushuhudia vita vya kulazimishwa na wale walio kaskazini na katika makambi ya wakimbizi?, na Je hawakulenga kwa Magari yalifungwa Mabomu ya kulipuka? katika Mikoa ya Wakristo na maeneo ya kambi za Jeshi? haya yote yalitokea kabla ya matukio ya Syria kuanza.”

sayed-out-475-2Alisema kuwa “habari za hivi karibuni zimebaini kuwa wengi katika nchi ambazo zilizokuwa zikifadhili na kuwezeshwa wapiganaji wa kigeni kuingia Syria wameanza kuonyesha hofu yao kutokana vitisho vya usalama wao kwa ushindi wa Syria,” na ameashiria baadhi ya hatua mpya kadhaa zinazochukuliwa na nchi hizi ili kuzuia wananchi wao kusafiri kwenda Syria kushiriki katika mapambano yanayoendelea huko,” na kutoa kama mifano nchi za Tunisia na Saudi Arabia juu ya hilo.

Aidha, akiwahutubia Walebanoni alisema: “Kwa nini nchi hizi zote zinaruhusiwa kuwa na wasiwasi juu ya uwepo wa vijana wao katika safu za makundi ya waasi huko Syria?, na sisi majirani wa Syria, ambao maisha na hatima yetu vinahusiana na yanayoendele huko Syria, haturuhusiwi kuchukua hatua za tahadhari kwa hilo? Ni kitu gani mpaka leo Serikali ya Lebanon imekifanya zaidi ya kujiengua binafsi jambo ambalo ni sawa na kuzika kichwa chake chenyewe katika mchanga? Je, hatuna haki ya kuingilia kati kuzuia mauaji, wizi na kubakwa Wanawake ambapo Lebanon ina zaidi ya raia 30,000 wamekuwa wakiteseka huko Al-Qusayr? Itakuwaje laiti kama wale Wakufurishaji (Takfir) ambayo walishindwa huko Qusayr watakuja Lebanon? Je, itakuwaje, Mungu aepushie mbali, kama wataweza kuidhibiti Syria yote? Ni picha gani itakuwa wakati huo?”

Aidha, Kiogozi huyo Muadhamu aliuliza zaidi: “Kwa nini wanaogopa uchaguzi usifanyike huko Syria? Ni kwa sababu wanajua maoni ya umma yapo upande gani kwa sasa.”

Kutokana na nukta hizo, Sayyed Nasrallah akathibitishia kuwa “na tutashinda katika Mapambano haya na ni suala tu la wakati.  Kile ambacho kilihitaji kwa mapambano haya kwa ngazi mbalimbali kinapatikana, haya ni mapambano muhimu, lakini hatima yake ni ushindi.”

Hata hivyo, alisisitiza umuhimu wa kuzuia malengo yoyote ya Makundi ya kukufurisha (Takfiri) na muhimu ni mapambano kuzuia fitina za kimadhehebu.

“Matamshi yao huko Syria na Lebanon ni kuhusu madhehebu ni kama wanataka kuchochea chuki za Kimadhehebu. Wanataka sisi kama Mashia ambao Wanawake na Watoto wetu ni wanalengwa katika milipuko ya mabomu tujibu kwa chuki za Madhehebu, lakini hili halikutokea katika siku za nyuma na kamwe halitotokea katika siku zijazo. Majibu hayo yatawafaa tu Makundi ya Kukufurisha (Takfiris), “alisema, akisifu Jeshi la Lebanon na mafanikio yake ya kiintelijensia hasa ya hivi karibuni.

Serikali Lebanon…

Kuhusu Serikali ya Lebanon ambayo iliundwa Siku ya Jumamosi, Sayyed Nasrallah amewahakikishia kuwa Hizbullah iliridhia makubaliano mengi ili kuundwa serikali hii, kwa kuzingatia zaidi “maslahi ya kitaifa “au    Serikali ya “Maridhiano” badala ya serikali ya muungano.

Kiongozi huyo Muadhamu alisisitiza kwamba “Hizbullah wakati wote daima ilikuwa wakitafuta ushirikiano na haijawahi kusema kamwe inakataa kuunda Serikali ya ushirikiano pamoja na Future Party, au Jeshi la Lebanon au kikundi chochote cha March 14 … hatujawahi kamwe kusema tunakataa mazungumzo na Machi 14, tumekuwa tukisistiza kuwa tunataka Serikali ya Umoja wa kitaifa na Majadiliano, na hili halimaanishi kulazimisha maoni ya mtu yeyote kwa upande mwingine.”

Sayyed Nasrallah aliwahakikishia kwamba “wale waliochelewesha  kuundwa kwa serikali kwa muda wa miezi kumi hawatokani na Mikoba ya Mawaziri bali ni kutoka ule pande ambao ulikataa kuunda serikali ya kisiasa na kutoa wito wa kuunda Serikali isiyofungamana na upande wowote (Neutral) na kuwatenga Hizbullah,” na akasema kuwa “Uimara wa Hizbullah leo ni thabiti zaidi na wenye nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote, iwe ni kwa Siasa za ndani, Kikanda au Kimataifa…”

Akitoa maoni yake juu ya hofu na wasiwasi wa baadhi ya watu kwa baadhi ya mawaziri waliochaguliwa katika Serikali mpya, Sayyed Nasrallah alisema: “Mimi ninawaambia  haijalishi ni nani atateuliwa kushika wadifa wa Waziri wa Sheria, lakini Omar Al- Atrash au Naim Abbas hawataachiliwa kamwe kwa sababu wamekiri kuhusika katika hujuma ya Gari lilifungwa Mabomu … “

kwa kumalizia…

Muadhamu alitoa saluti Salamu ya heshima kwa Wananchi wanaodhulumiwa wa Bahraini kwa kupitisha miaka Mitatu wakiwa katika mapinduzi yao ya Amani na ya kiistaarabu licha ya ukandamizaji wote na kamatakamata inayofanywa na serikali.

Pia alitoa salamu za heshima kwa Walebanoni wote, Wapalestina, na raia watukufu wote katika kanda, akisema: “Kama unataka Israel ipoteza nafasi yoyote iliyonayo, na kama unataka kuzuia fitna katika ukanda huu, Sitisheni vita dhidi ya Syria na waondoeni wapiganaji huko, na bila shaka na sisi tutaondoka wakati huo. Kwa pamoja lazima tuzuie Vita hivi dhidi ya Syria ili kulinda Lebanon, Palestina, Syria, na taifa.

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on February 17, 2014, in Habari na Matukio and tagged , , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings