KIONGOZI MUADHAMU WA MAPINDUZI YA KIISLAMU AONANA NA WANANCHI WA MKOA WA AZERBAIJAN

KIONGOZI MUADHAMU WA MAPINDUZI YA KIISLAMU AONANA NA WANANCHI WA MKOA WA AZERBAIJAN

17/02/2014

13921128000485_PhotoIAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na maelfu ya wananchi wa Tabriz na miji mingine tofauti ya mkoa wa Azerbaijan Mashariki na sambamba na kutoa shukrani zake za dhati kwa matabaka ya wananchi wote wa taifa kubwa la Iran kutokana na kuwaonyesha walimwengu tena kwa sura nzuri kabisa nguvu na utukufu wao kupitia maandamano ya Bahman 22 (Februari 11) na kupitia sherehe za kuadhimisha miaka 35 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ameitaja istikama na mshikamano kuwa ni ujumbe mkuu wa aina mbili uliotawala katika maandamano ya mwaka huu ya maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Katika maandamano ya mwaka huu ya Bahman 22 taifa la Iran lilitoa majibu makali; kwa jeuri na ufedhuli, kupenda makuu, utovu wa heshima, ujuvi na usafihi wa viongozi wa Marekani. Wananchi wa Iran walijitokeza kwa wingi mno katika maadhimisho hayo na kutangaza kuwa, kamwe hawawezi kusalimu amri wala kupiga magoti mbele ya ubeberu, usaliti na ulaghai wa Marekani.

Katika mkutano huo ambao umeitishwa wakati wa kukaribia maadhimisho ya miaka 36 ya harakati ya kihistoria ya wananchi wa Azerbaijan, yaani Bahman 29, 1356 (Hijria Shamsia sawa na Februari 18, 1978) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameanza hotuba yake kwa kuwashukuru wananchi wa Iran kwa kushiriki kwa wingi mno katika maandamano ya Bahman 22 ya mwaka huu (Februari 11 wakati zilipofikia kileleni sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran).

Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Ulimi hauna uwezo wa kusifu na kushukuru vile linavyopasa kushukuriwa taifa kubwa la Iran lakini kabla ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu Ambaye ndiye mlainishaji na mbadilishaji wa Roho na nyoyo na nia na azma. Aidha amesema: Ninamsujudia Mwenyezi Mungu kumshukuru kwa neema zake hizi na halafu ninatoa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya moyo wangu kwa wananchi wa matabaka yote wa Iran kote nchini kutokana na kuwaonyesha walimwengu sura iliyotukuka, iliyostawi, na iliyo hai ya Mapinduzi ya Kiislamu wakati wa maadhimisho ya Bahman 22.

Baada ya hapo ameashiria harakati ya kihistoria iliyofanywa na wananchi wa mji wa Tabriz tarehe 18 Februari 1978 na kusema kuwa tukio hilo lilitoa mafunzo na ibra nyingi na kuongeza kwamba: Funzo la kwanza kabisa linalopatikana katika harakati hiyo ya Bahman 29 (Februari 18) lilikuwa ni kutoa taswira ya sifa maalumu na kubwa za wananchi wa Tabriz na wa Azerbaijan.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Imani thabiti na kubwa ya kidini, ghera ya kidini, ushujaa, kuelewa vizuri nyakati na kuchukua hatua kwa wakati unaofaa, kuwa mstari wa mbele na kufungua njia na kufanya ubunifu wa hali ya juu katika njia ya kufikia malengo ni miongoni mwa sifa maalumu za kipekee za wananchi wa Tabriz na Azerbaijan ambazo taswira yake ilitolewa na harakati ya wananchi hao ya Bahman 29 (Februari 18, 1978).

Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja somo la pili lililotolewa na harakati ya Bahman 29 ya wananchi wa Tabriz na Azerbaijan kuwa ni kuonesha mshikamano na uhusiano madhubuti na wa kina uliopo baina ya watu wa kaumu na makabila tofauti ya Iran.

Amesema: Watu wa kaumu mbali mbali nchini Iran kutokana na kukita mizizi imani ya dini ya Kiislamu katika nyoyo zao, wote wanaungana pamoja chini ya bendera ya Uislamu na jina linalovutia la Iran na kuwafanya wote kuwa na mfungamano wa karibu mno na jambo hilo ndiyo ile nukta ambayo watu wanaolitakia mabaya taifa la Iran wanailenga kwa nguvu zao zote na wanataka kuwachonganisha Wairani wa kaumu na makabila mbali mbali wazozane na wapigane wao kwa wao.

13921128125800379_PhotoLVile vile ametoa mwito kwa wananchi na viongozi wote nchini Iran kuwa macho mbele ya suala hilo na kusisitiza kuwa: Haipasi kusahauliwa hata kwa sekunde moja ujumbe wa mshikamano, umoja na ushirikiano uliokuwemo kwenye harakati ya Bahman 29.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja “muujiza wa irada ya taifa” kuwa ni ujumbe wa tatu uliokuwemo kwenye harakati ya Bahman 29 ya wananchi wa Tabriz na mkoa wa Azerbaijan na kuongeza kuwa: Harakati hiyo ilionesha kuwa, hakuna kitu chochote na wala nguvu yoyote hata yenye ukubwa kiasi gani inayoweza kukabiliana na irada na nia thabiti ya taifa lililosimama imara na lisilotetereka.

Akiendelea na hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amechambua sababu zilizowafanya wananchi wa Iran wajitokeze kwa wingi zaidi na kwa hamasa kubwa zaidi katika maadhimisho ya mwaka huu ya Bahman 22 na ujumbe uliotolewa na wananchi katika maandamano ya siku hiyo.

Vile vile ameashiria mahesabu na ripoti takriban za kina za watu weledi na watambuzi wa mambo kuhusiana na idadi ya watu walioshiriki kwenye maandamano ya Bahman 22 katika miaka tofauti na kusema: Kwa mujibu wa ripoti za kina na za kitaalamu, idadi ya watu walioshiriki katika maandamano ya mwaka huu ilikuwa kubwa zaidi ikilinganishwa na ya mwaka uliopita na jambo hilo ni udhibitisho wa uhakika kuwa, sherehe za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kama yalivyo mapinduzi yenyewe, ni tukio la aina yake na la kipekee kabisa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja hatua ya wananchi ya kufanya sherehe katika nukta mbali mbali za Iran kwa ajili ya kuadhimisha Mapinduzi yao ya Kiislamu tena baada ya kupita miaka 35 ya ushindi wa mapinduzi hayo kuwa ni jambo la kustaajabisha na la kuvutia sana kwani sherehe hizo zinafanyika kwa sura ya kipekee na ya kuvutia na kutia moyo tofauti na sherehe chapwa na zilizojaa urasmi za nchi nyinginezo na kuongeza kuwa: Tofauti kabisa na zinavyojaribu kuonyesha propaganda na uchambuzi usiotegemea ukweli wa vyombo vya habari vya kibeberu, uhakika wa mambo ni kuwa wanafikra na watungaji sera wa nchi hizo za kibeberu wanaupata kwa vizuri sana ujumbe wa wananchi wa Iran wanaoshiriki kwa hamasa na imani ya hali ya juu katika matukio kama hayo na ujumbe unaobebwa na kaulimbiu za taifa la Iran.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Kauli mbiu za wananchi katika maandamano ya Bahman 22 zilibeba ujumbe wa aina mbili, ujumbe wa istikama na kusimama kidete na ujumbe wa umoja na mshikamano.

13921128125758273_PhotoLAmetoa ufafanuzi zaidi kuhusu ujumbe wa istikama na kusimama imara katika kulinda na kutekeleza malengo matukufu akisema: Mapinduzi ya Kiislamu yana malengo chanya na malengo yanayofuatiliwa kwa njia hasi. Amefafanua kwa kusema: Malengo yake chanya ni kutekeleza kivitendo mafundisho ya Uislamu, kusimamisha uadilifu wa kijamii, kushiriki vilivyo wananchi katika nyuga na matukio tofauti, kuwa na uchumi huru, utamaduni wa asili wa Iran – Kiislamu usiopandikizwa kutoka nje, kuwasaidia na kuwapa hifadhi wanyonge na watu wanaodhulumu sambamba na kupambana na dhulma, kuiletea nchi maendeleo, kupiga hatua kubwa za kielimu na kuwa mstari wa mbele katika masuala ya kimaanawi, kiakhlaki na maadili bora.

Ayatullah Udhma Khamenei amekutaja kutosalimu amri na kutokuwa tayari kuupigia magoti ubeberu, ulaghai na usaliti wa madola ya kibeberu ambayo dhihirisho lake la wazi kabisa ni Marekani, kuwa ni malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu yanayofuatiliwa kwa njia hasi na kusisitiza kuwa: Katika maadhimisho ya Bahman 22 mwaka huu, taifa la Iran lilitangaza wazi kuwa , ulaghai na usaliti wa Marekani.

Vile vile amewakosoa watu wanaojaribu kuwaonyesha wananchi wa Iran sura isiyo halisi ya Marekani na kusema: Kuna baadhi ya watu wanajaribu kuipamba na kuiremba sura ya Marekani ili kuficha na kufifiliza sura chafu, ya ukatili na ya kutisha ya dola hilo na wanajaribu kuonesha kuwa serikali ya Marekani inawapenda wananchi wa Iran, na eti ni serikali inayowapenda watu wengine, lakini ni jambo lisilo na shaka kwamba juhudi za watu hao zitashindwa kuzaa matunda wanayoyataka.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria historia chafu ya watawala na serikali za Marekani katika kipindi kisichopungua miaka 80 iliyopita na kuongeza kuwa: Hatua ya Marekani ya kuanzisha vita vya umwagaji damu na kuua watu watu wasio na hatia katika kona mbali mbali za dunia, kitendo chake cha kuwasaidia na kuwaunga mkono Madikteta madhalimu katika nukta tofauti duniani, kuunga mkono ugaidi wa kimataifa, kuunga mkono ugaidi wa kiserikali ambao dhihirisho lake la wazi ni utawala pandikizi, ghasibu na unaotenda jinai wa Kizayuni, kuivamia kijeshi Iraq na kuua kwa uchache makumi ya maelfu ya watu nchini humo, kuivamia Afghanistan, kuanzisha mashirika ya kuua watu na ya kigaidi kama vile shirika la Black Water na kuasisi makundi yenye misimamo mikali ya kitakfiri yanayokufurisha Waislamu wengine na kuyaunga mkono kwa kila hali, ni sehemu ndogo tu ya vitendo vichafu na viovu vya Marekani. Ayatullah Udhma Khamenei pia amehoji kwa kusema: Vipi inawezekana kuiremba na kuipamba sura ya mtenda jinai kama huyo mbele ya wananchi wa taifa la Iran?

Aidha amegusia historia ya uadui wa Marekani dhidi ya wananchi wa Iran na kuongeza kuwa: Tangu wakati wa mapinduzi ya tarehe 28 Mordad 1332 (August 19, 1953) hadi mwaka 1357 (1979) na tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo hii taifa la Iran limekumbwa na kila aina ya jinai, usumbufu, maudhi, kero, njama na vikwazo vya Marekani ambapo suala la karibuni kabisa ni kitendo cha kifedhuli cha Rais wa Marekani cha kuwaunga mkono watu waliofanya fitna ya mwaka 88 (2009 nchini Iran na hasa mjini Tehran) na hadi hivi karibuni kabisa ametangaza kuwa anaendelea kuwaunga mkono wafanya fitna hao.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa: Orodha hiyo ni sehemu ndogo tu ya vitendo viovu vya watawala wa Marekani dhidi ya taifa la Iran na hadi hivi sasa vingali vinaendelea.

Ayatullah Udhma khamenei amekumbushia pia hotuba aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka huu (wa Hijria Shamsia) huko Mash’had (kaskazini mashariki mwa Iran) na kuongeza kuwa: Kuna baadhi ya watu ndani ya serikali iliyopita na hata ndani ya serikali ya hivi sasa wanadhani kuwa kama sisi tutafanya mazungumzo na Marekani katika kadhia ya nyuklia, basi masuala yote yatatatuka. Nami pia kutokana na kusisitiza kwao sana kuhusu mazungumzo hayo ya nyuklia nimesema kuwa sina pingamizi lakini tangu mapema kabisa nilisisitiza kuwa, mimi sina matumaini na wala sina mtazamo mzuri kuhusu mazungumzo hayo.

Ameongeza kuwa: Hivi sasa ishara zinazotufanya tusiwe na matumaini na mazungumzo hayo zimeanza kujitokeza na ishara ya wazi kabisa ni matamshi ya kifedhuli na ya kijeuri ya Maseneta na viongozi wa Marekani dhidi ya taifa la Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwa kusisitiza kwamba: Tab’an katika maandamano ya Bahman 22 mwaka huu, taifa la Iran lilitoa majibu makali kwa ufedhuli, usafihi na jeuri hizo za viongozi wa Marekani.

13921128125802500_PhotoLAyatullah Udhma Khamenei amesema: Moja ya sababu zilizowafanya wananchi wa Iran washiriki kwa wingi zaidi na kwa hamasa kubwa zaidi katika maandamano ya Bahman 22 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ni jeuri, kupenda makuu ufedhuli na usafihi wa viongozi wa Marekani ambao umeamsha ghera ya kidini ya wananchi wa Iran na kuwafanya wajitokeze kwa wingi na kwa hamasa kubwa ili kuipa somo na kuitangazia serikali ya Marekani kuwa isifanye makosa katika mahesabu yake kwani wananchi wa Iran wako imara katikati ya medani.

Ameongeza kuwa: Ujumbe wa wananchi wa Iran katika maandamano ya Bahman 22 mwaka huu kwa viongozi wote nchini na kila mtu anayehudumu katika Wizara za Mambo na Ndani na Nje za nchi ni kwamba, taifa la Iran liko imara na limesimama kidete na kwamba viongozi nao hawapaswi kuhisi udhaifu wa aina yoyote ile katika kukabiliana na adui.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia himizo na sisitizo ambalo amekuwa akilitoa mara kwa mara kwamba kadhia ya nyuklia ni kisingizio tu kinachotumiwa na madola ya kibeberu hususan Marekani na kuongeza kuwa: Kama itatokezea siku moja – kwa mfano ambao taba’an hauwezekani – kadhia ya nyuklia ya Iran ikatatuliwa kwa namna inayotaka Marekani; basi ni wazi kuwa Wamarekani watazusha kitu kingine na hata hivi sasa watu wote tayari wanaona namna wasemaji wa serikali ya Marekani wanavyozungumzia masuala ya haki za binadamu na uwezo wa makombora na wa kujilinda wa Iran.

Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Hivi hawa Marekani hawaoni haya kweli kuzungumzia suala la haki za binadamu?Kwani kama kila mtu duniani ana haki ya kuzungumzia suala la haki binadamu, mtu huyo hapaswi kuwa Mmarekani ambaye ana faili kubwa sana la uvunjaji wa haki za binadamu. Marekani haina haki hata ya kutamka tu neno haki za binadamu.

Ameashiria vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinavyotendwa na Marekani ikiwa ni pamoja na jinai zake katika jela za Guantanamo na Abou Ghuraib, misaada ya Marekani kwa magaidi maarufu duniani, kuvunja kwake ahadi na uongo wa kila namna wa Marekani na kuongeza kuwa: Wamarekani ambao wana faili hilo kubwa na jeusi, wanapaswa waone haya hata kutamka jina tu la haki za binadamu lakini cha kustaajabisha ni kuwa wanadai kwa ufedhuli mkubwa kwamba eti wanapigania haki za binadamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile amesema kuhusu mazungumzo ya nyuklia kwamba: Kazi iliyoanzishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na viongozi wa serikali kuhusu mazungumzo ya nyuklia itaendelea na Iran haitakuwa ndiyo nchi itakayojitoa na kuachana na kazi hiyo iliyoianzisha yenyewe lakini kila mtu atambue kuwa,Uadui wa Marekani ni dhidi ya asili ya Mapinduzi ya Kiislamu, Uadui wa Marekani ni dhidi ya Dini yenyewe ya Kiislamu na kwamba Uadui huo kamwe hauwezi kwisha kwa mazungumzo.

Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Njia pekee ya kuweza kuponya na kukabiliana na uadui huo ni kutegemea uwezo wa ndani na wa taifa na kuzidi kuimarisha muundo wa ndani ya nchi.

Vile vile ameashiria kuwasilishwa siasa kuu za uchumi wa kimuqawama karibuni sana hivi, na ameongeza kusema: Njia ya kuweza kutatua matatizo ya nchi ni kutekelezwa siasa za uchumi wa kimapambano na kimuqawama na kutegemea nguvu za ndani ya nchi na kutokodolea macho msaada kutoka nje.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile ameashiria utajiri mkubwa na wa kipekee wa maliasili na nguvu kazi iliyonao Iran hususan akiba kubwa ya mafuta na gesi inayohitajika sana duniani na kuongeza kuwa: Kila mtu ameona namna nchi za kigeni zilivyomiminika kwa wingi nchini Iran baada ya kuona tabasamu tu la Iran hivyo Marekani haiwezi kubakia milele na siasa zake za kiukaidi na kiubishi na kama sisi tutasimama imara na kutegemea uwezo wetu wenyewe, bila ya shaka yoyote tutaushinda ukaidi na ubishi wa Marekani.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Kamwe hatutaweza kufika popote kama macho yetu yatakuwa yanakodolea misaada ya wengine, au tutakaa na kusubiri kupunguzwa vikwazo au tutakaa na kungalia viongozi wa Marekani wanasema nini.

Ameongeza kuwa: Ninapenda kusisitiza tena na tena kuwa, viongozi wetu nchini wategemee uwezo wetu wa ndani, wawaamini wananchi ili chemchemu hii ya ndani ya nchi inayochemka kwa nguvu na isiyo na mwisho izidi kuchemka na kutoa matunda mazuri yanayotakiwa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Kama hilo litatendeka, basi bila ya shaka yoyote milango iliyofungwa itafunguka na inabidi tuendelee kivitendo na njia ya harakati hiyo.

Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, malengo ya Marekani na mabeberu wa dunia dhidi ya taifa la Iran yatashindwa tu na taifa hili litashinda na kusherehekea ushindi wake huo mbele ya macho ya wanaolitakia mabaya taifa la Iran.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Ayatullah Mujtahid Shabestari, Mwakilishi wa Fakihi Mtawala mkoani Azerbaijani Mashariki ambaye pia ni Imam wa Sala ya Ijumaa wa mji wa Tabriz ametoa hotuba fupi na sambamba na kuwakumbuka na kuwataja kwa wema mashahidi wa harakati ya Bahman 29, 1356 (Februari 18, 1978) wa huko Tabriz amesisitiza kuwa: Harakati ya Bahman 29 ya wananchi wa Tabriz ilikuwa ni hamasa kubwa iliyobakia milele na iliyokuwa na taathira za kipekee na ilipelekea kufedheheka zaidi utawala wa kifalme wa Shah na kuimarika na kuzidi kupata nguvu Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.

Imam wa Sala ya Ijumaa wa Tabriz vile vile amewashukuru wananchi wote wa Iran kwa kushiriki kwa wingi mno na kwa hamasa kubwa katika maandamano ya Bahman 22 na kuongeza kuwa, hatua ya wananchi wa Iran ya kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo ya miaka 35 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu imethibitisha kivitendo msimamo wao wa kupinga na kupambana na ubeberu na vile vile uaminifu na imani yao kwa Mapinduzi ya Kiislamu na kwa Fakihi Mtawala na wametoa jibu kali sana kwa matamshi ya kifedhuli na kisafihi ya viongozi wa Marekani.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on February 19, 2014, in Habari na Matukio and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings