IMAM WA SWALA YA IJUMAA: ITIKADI YA UTAKATIFU (UMAASUMU) WA MITUME SILAHA PEKEE YA KULINDA UJUMBE WA ALLAH (SW).

 UntitledHatibu na Imam wa Swala ya ijumaa Msikiti wa Ghadir Kigogo, Dar es Salaam Sheikh Mohamed Abdi Mbwana akiwahutumia mamia ya waumini katika ibada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa msikitini hapo leo amewaasa Waislamu kutumia Akili zao kubainisha utukufu na Utakatifu (Umaasumu) wa Mitume na ndipo waegeukia Aya za Mwenyezimungu na kuasa kuwa Allah (sw) ameahidi kwa kupitia akili atawatia watu peponi na kwa akili hiyo hiyo pia atawaingiza Motoni.

Katika sehemu ya kwanza ya hutuba yake amesema maana ya neno Mtume ni Mtu aliyeteuliwa Makhsus na Allah (sw) kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu pasina na kiunganishi chochocte cha kibainaadamu, Aidha akabainisha kuwa tafsiri hiyo ndiyo inayomtoa Imamu kuwa mtume kwani imam hufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kupitia kiunganishi cha Mtume kwa maneno mengine Imamu hutufikishia ujumbe alioupata kutoka kwa Mtume, vile vile tafsiri hiyo pia humuondoa Malaika kuwa Mtume kwani mteule lazima awe binaadamu. Katika kauli yake akawaasa waumini akisema Imani ya uwepo wa Mitume kama moja ya nguzo ya Imani ya Uislamu haiwezi kukamilika mpaka kuamini kuwa mitume kamwe hawawezi kufanya Makosa na akabainisha kuwa kuitakidi kuwa Mitume hawawezi kufanya makosa (Maasum) ni itikadi inayopatikana kwenye madhehebu ya Kishia pekee.

Sheikh Mohamed Abdi ametanabaisha waumini kuwa yeyote asiyeamini juu ya Umaasum wa Mitume atakuwa amejiingiza katika itikadi potofu ya kuamini kuwa mitume ni kama binaadamu wengine wanafanya makosa, na akawataka wote wenye itikadi hiyo kutambua kuwa sio tu imani hiyo hutumika mara zote kuwa msingi wa kuwadhalilisha mitume bali pia imewatumbukiza wenye imani hiyo katika changamoto na au chaguzi tatu  kuu, Eidha kuchagua baadhi ya ujumbe wa Mtume (saww) kuufuata na kuacha baadhi kwa dhana kuwa zipo nyakati huwenda mtume alipitiwa na kufanya makosa hivyo kushindwa kufikisha ipasavyo ujumbe wa Mwenyezi Mungu na au ukubali kuwa mitume walikuwa wakikosea na ikawepo haja ya kumpata mtu wa kuwakosoa wanapokosea, katika sintofahamu hii ndipo msingi wa kuwatukuza watu wengine wa kawaida na kumdhalilisha na kumshusha cheo mtume ulipopata Mashiko yake.

Imamu wa Swala ya Ijumaa akaongeza kuwa changamoto ya tatu ni kwa yeyeote asiye amini Umaasumu wa Mtume, kimantiki anaitakidi kuwa Allah alifanya makosa (Allah atuepusha na uzushi huo) katika uteuzi wake kwa kumteua mtume mtu ambaye hajakamilika na ni mwenye kufanya makosa. Mwisho ameashiria mbali ya vigezo hivi vya kiakili na Kiman

Untitled2

tiki ambavyo kila muumini anapaswa kuvitumia katika akili yake pia ndani ya Quraan zipo aya Chungu nzima zinazoainisha kuwa mitume wote walikuwa Maasumu. Na kuzianisha aya husika Mosi ni Surat S’aad: Aya 82-83 kupitia Ulimi wa Ibilisi alipochukuwa kiapo cha kuwapotosha binaadamu wote aliposema…” naapa kwa nguvu zako nitawapoteza waja wako wote ispokuwa wale miongoni mwa waja wako waliotakaswa (waliokingwa kufanya Madhambi na makosa) na pili ni katika Surat (Nisaa Aya ya 64) Kwa hakika hatukumtuma Mtume isipokuwa atiiwe kwa Idhini ya Mwenyezimungu. Kwa dalili hizi yatosha kujua kuwa kuteuliwa na kutumwa kwa mitume kumeambata na wajibu wa kutiiwa, na hawezi kutiiwa yule ambaye anafanya makosa na Madhambi. Mwisho aliwataadharisha waumini kuwa Uislamu na ujumbe wa uislamu utabakia Milele mbali ya vita vinavyopiganwa dhidi ya uislamu na kuwataka wote kujua kuwa Itikadi ya Utakatifu (Umaasumu) wa Mitume ndio silaha pekee ya kulinda Ujumbe wa Allah (sw).

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on February 21, 2014, in Hotuba na Mawaidha and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: