Kuzaliwa Sayyeda Zainab (sa)

Kuna tofauti ya maoni kuhusu Tarehe rasmi ya kuzaliwa kwa Sayyeda Zainab (sa). Wengine wanasema ilikuwa katika Mji wa Madina Tarehe 5 ya Jamadi Al-Awwal, na wengine wanasema ni Tarehe 1 mwezi wa Shabaan, katika mwaka 6 Hijria.
Ilikuwa ni miaka mitano baada ya Waislamu kushiriki pamoja na Mtume (SAW) katika Safari ya kuhamia (Hijrah) Madina, ndicho kipindi Binti Mtakatifu wa Mtume, Sayyeda Fatima (sa), alijifungua msichana mdogo.
Wakati baba yake, Imamu Ali (AS), alipomuona binti yake huyo mchanga kwa mara ya kwanza alikuwa amekuja pamoja na Imam Hussain (as), ambaye wakati huo alikuwa na umri wa karibu miaka mitatu, Kijana (Imam Hussein) akasema kwa furaha, “Oh! Baba, Mwenyezi Mungu amenipa Dada.” Kwa maneno hayo Imam Ali (as) alianza kulia, na pindi Hussain (as) alipomuliza kwa nini alikuwa analia hivyo, baba yake alijibu kwamba hivi karibuni utakuja kujua.
Sayyeda Fatima (sa) na Imam Ali (as) hawakumpa jina mtoto wao mpaka siku chache baada ya kuzaliwa kwake, kwani wao walikuwa wakimsubiria Mtume kurudi kutoka safari yake ili aweze kupendekeza jina .
hatimaye wakati mtoto wa kike alipoletwa mbele ya mtume alimpakata katika mapaja yake na kumbusu. Ndipo Malaika Jibril alimshukia, na kutoa jina ambalo atapaswa kupewa mtoto huyo, na kisha akaanza kulia.
Mtume (SAW) akamuuliza Jibril kwa nini analia naye akajibu, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Tangu mapema katika maisha ya msichana huyu ataingia na kubakia katika mateso na majaribu katika dunia hii, Majaribu ya kwanza yeye atakulilia wewe utakapotengana (kutoka katika dunia hii); baada ya hapo ni yeye atakayelia kwa ajili kuondokewa na mama yake, kisha baba yake, na kisha kaka yake Hassan. Baada ya hayo yote atakabiliwa na majaribu ya ardhi ya Karbala na mateso ya jangwa la upweke, Kwa sababu ya mateso hayo utafika wakati hata nywele zake zitabadilika na kuwa za kijivu na mgongo wake Kuinama.”
Wakati jamaa katika familia ya Mtume waliposikia utabiri huu wa Wahyi kwa mtume wote waliangusha kilio kikubwa. Hapo Imam Hussain (as) sasa akaelewa kwa nini mapema baba yake alikuwa pia akilia. Kisha Mtume (SAW) akampa jina lake kuwa ni Zainab (sa).
Siku moja, wakati Zainab (sa) akiwa na umri wa miaka mitano, aliota ndoto ya ajabu na kutisha. Upepo mkali ulikuwa ukivuma katika Mji na kutia Giza zito katika Dunia na Anga. Msichana mdogo akipepesuka huku na huko, ghafla mschana huyo akijikuta amekwama katika Matawi ya Mti mkubwa. Lakini upepo ulikuwa ni mkubwa kiasi ambacho Mti ule uling’olewa. Zainab (sa) akayashika wa Matawi yake lakini nayo yakakatika. Kwa woga akayakumbatia Mashina mawili lakini mashina nayo yakakatika na kumuacha akidondoka bila msaada. Kisha kwa mshtuko akaamka. Wakati alipomsimulia babu yake, Mtume (SAW), kuhusu ndoto hiyo Mtume akalia sana kwa uchungu na akasema, “Ewe binti yangu. Kuhusu Mti huo ni mimi ambaye nina muda mfupi nitaondoka na kuiacha hii dunia. Matawi ni baba yako Ali na mama yako Fatima Zahra, na Mashina ni ndugu zako Hassan na Hussain. Wote hao wataondoka dunia hii kabla yako, na utateseka kwa kutengana nao.”
Alipotimiza umri wa miaka saba ndio wakati mama yake mpendwa aliaga dunia. Kifo cha mama yake kwa ukaribu kilifuatana na kifo cha babu yake mpendwa Mtume Muhammad (saw). Baada ya muda fulani Imam Ali (as) alimuoa Bi Ummul- Banin, ambaye ibada na ucha Mungu wake ulimpa moyo na msukumo Zainab ( sa) katika kujifunza kwake.
Wakati bado angali msichana alikuwa na uwezo kamili wa kutunza na kuwajibika katika utunzaji na uendeshaji wa nyumba ya baba yake. Kama vile kujali na kuhakikisha ndugu na dada zake wanakaa kwa utulivu, starehe, Kwa mahitaji yake mwenyewe alikuwa akiyatoa kwa ukarimu na kusaidia maskini, wasio na makazi na Mayatima. Baada ya ndoa yake imeripotiwa kuwa mumewe alikuwa akisema, “Zainab ni Mama bora wa nyumbani.”
Tangu mapema sana alijenga na kuyalewa mahusiano yasiovunjika na nduguye Imam Hussain (as). Mara kwa mara wakati akiwa mtoto mchanga katika mikono ya mama yake hakuweza kumbembeleza na akaacha kulia, alikuwa akinyamaza tu pale anaposhikiliwa na kaka yake, na hapo hukakaa kimya akaiushangaa sana uso wake imam Hussein. Kabla ya kuanza ibada ya Swala alikuwa kwanza akiutizama uso wa kaka yake mpendwa.
Siku moja Bi Fatima (sa) alimuelezea Mtume (SAW) juu undani wa mapenzi ya binti yake kwa Imam Hussain (as). Mtume akashusha pumzi kwa nguvu na akasema kwa macho laini, “Mtoto wangu mpendwa, hakika huyu mwanangu Zainab atakabiliwa na majanga elfu na moja na atakabiliwa na shida kubwa huko Karbala.”
Zainab (sa) alikuwa mwanamke mwenye umbo zuri kuhusiana na muonekano wa umbile lake ni machache yanayojulikana. Wakati wa janga la Karbala lilipomkumba akiwa na miaka Hamsini alilazimishwa kutoka nje akiwa bila hijabu. Ni wakati huo baadhi ya watu walisema kuwa alionekana kama “Jua linalong’aa ” na “kipande cha Mwezi

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 6, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: