KHATIBU WA SWALA YA IJUMAA: USTAWI WA JAMII NA MAISHA BORA YA WATANZANIA NI DHIMA ILIYO MIKONONI MWA KILA RAIA MZALENDO.

image

Na. Abuuzahraa 07/03/2014
Khatibu wa Swala ya ijumaa Msikiti wa Ghadir uliopo kigogo Polisi post Jini Dar es Salam, Samahat Sheikh Hemedi Jalala akiwahutubia Mamia ya waumini waliofurika msikitini hapo, alitambulisha umuhimu wa kila Raia kufahamu jukumu lake kwa nchi yake na kujenga hisia sahihi za Utaifa kwa nchi yake. akifafanua Maudhui ya Aya 48 sura ya Tano (Maida) : Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka angekufanyieni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyokupeni basi shindaneni kwa mambo ya kheri” aliwakumbusha waumini kuwa Mwenyezi Mungu hakumuacha Mwanaadamu bure bure bali aliwaweka Kanuni kuu na Jumla na papo hapo kuruhusu kwa Mataifa na Umma mbalimbali kujitungia kanuni, na Sheria ndgo ndogo Maaalumu za kuendeleza Maisha yao na ustawi wa Nchi zao na haya yanaweza kuthibitishwa kwa kutupia jicho katika Quraan…. kuhusiana na Maisha ya Baba yetu na Nabii Ibrahimu (as) na hata Mtume wetu Muhammad (saw) wote walipewa kanuni kuu za maisha na kuruhusiwa kujiwekea kanuni na sheria maalumu za ustawi wa jamii zao na maisha yao.
Aidha khatibu wa Swala ya Ijumaa alionya kuibuka na kusambaa makundi ya watu wenye kusambaza fikra potofu za madai kuwa kanuni au taratibu mpya zozote ni Bidaa na kuwa hazikuwepo wakati wa Mtume (saw). Sheikh aliyaelezea makundi hayo ya watu kuwa yanaangukia miongoni mwa maeneo Matatu, eidha ni miongoni mwa mambumbu wasiojua falsafa ya Mafundisho ya Quraan  na Sunnah za Mtume, au kwa makusudi wanasambaza Mila potofu uliyoza fikra inayosambaa leo dunia fikra ya Ukufurishanaji na au ni Miongoni mwa Vibaraka wanaotumiwa bila kujua na Maadui ya Kiislamu.
Samahati Sheikh Jalala aliwakumbusha waumini kuwa maneno maarufu kuwa “Miji ni ya Mungu na Watu ni wa mungu” ni udhihirisho kwa watu wote na hasa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutambua kuwa wanalojukumu la kulinda dhamana hii ya Mungu waliyotunukiwa, watailinda kwa kujiwekea kanuni bora zao za maisha yao na kuziheshimu kanuni zilizoweka kwa ustawi bora nchi yao, Sheikh aliashiria kuwa sote tunajifunza kutoka kwa Wanazuoni wetu wakubwa wa Kifiqh wote wanakubaliana kuwa ni Haramu kuchafua Mazingira ni haramu hata kutupa chupa za maji barabarani, ni haramu pia kuvuta sigara mbele za watu endapo moshi unawakera, Mwenyezi Mungu ametupa ruhusa ya kujiwekea kanuni ili maisha yaende. Ni muhimu kuheshimu sheria na kanuni za Barabarani kwani zote hizi ni miongoni mwa kanuni na sheria ndogo ndogo zilizotungwa kwa ajili ya Maisha bora na ustawi wa jamii yetu.
Katika sehemu ya hutuba yake pia amewakumbusha raia wa Tanzania kuwa macho na nchi yao na kutambua kwa yakini kuwa Nchi ya Tanzania ni nchi tajiri na iliyosheheni Mali asili chungu nzima, na akawataka kuipiga vita nadharia inayosambazwa na nchi mabeberu kuwa Nchi yetu ni nchi Maskini wakati kila uchao Matajiri hao wa Magharibi wakifurika ndani ya nchi yetu kuchukua utajiri wetu. Akawataka wananchi kujua kuwa Tanzania imepewa upendeleo mkubwa na Mwenyezi mungu katika maeneo na uga tofauti tofauti, na kuwafungua macho waumini kwa kuwaainisha kuwa Nchi ya Tanzania inayo bahati ya kuruzukiwa Madini ya aina tofauti tofauti yakiwemo mengine yasiopatikana nchi nyingine yeyote, duniani kama vile Madini ya Tanzanite, Dhahabu, Almasi, Rubi, Na hata Mafuta na Gesi.Mbuga kubwa duniani za Wanyama, Mabonde ya Kilimo na Mito na Maziwa makubwa duniani bila kusahau ukanda uliozungukwa na Bahari ya Hindi katika maeneo tofauti tofauti ya Nchi yetu.
Aidha sheikh hakuacha kugusia juu ya mchakato wa Kuandika katiba mpya unaoendelea hivi sasa ndani ya nchi yetu na kuwatanabaisha wabunge wa bunge maalumu la Katibu na vikao vya bunge hilo vinavyoendelea huko Dodoma kutambua na kufanya Marejeo katika maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu … “Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake”… Na kuwataka Wananchi na hasa wabunge hao kutambua ruhusa waliyopewa ya kujiwekea kanuni, sheria na Taratibu za kuendesha maisha sio kwa lengo jingine lolote isipokuwa ni kwa ajili ya kuwezesha mazingira sahihi safi na salama ya kuabudiwa Mwenyezi Mungu. Na Lau angelitaka Mwenyezimungu basi angeliizuia ruhusa hiyo na kutufanya watu wote duniani kuwa ni taifa moja lenye rangi moja, kabila na lugha moja. Katika hilo alisisitiza umuhimu wa wabunge wa bunge maalumu kutunga kanuni na sheria nzuri na bora zitakazowawezesha wananchi kufaidi matunda ya Mali asili zilizopo katika Taifa lao. Katika hali ya mshangao Sheikh Jalala akauliza kulikoni Nchi za Afrika na hususani Tanzania leo ndani ya Karne ya 21 bado wananchi wake ni Maskini tena omba omba wa kutupa? Kuna nini Nchi za ulaya hazikumbwi na Ukame, Njaa, na Majanga haya mengine ya Kibinaadamu? Alishangazwa wako wapi wanasayansi na watafiti wazalendo wa nchi hii? kuinusuru Taifa hili na majanga haya ya kibinaadamu?
Katika kusisitiza umuhimu wa kujiwekea kanuni bora aliwataka wabunge wa bunge la katiba kupitia upya aya ya 48 Na kufahamu maana ya neno “…lakini ni kukujaribuni kwa aliyokupeni basi shindaneni kwa mambo ya kheri”… Kuwa Kushindana juu ya Mambo ya Kheri ni kutunga na kuweka kanuni, sheria na Taratibu sahihi zitakazowawezesha wananchi kufaidi Matunda ya Nchi yao na kubwa zaidi ni kujua kuwa mwisho wao ni kwa Mwenyezi Mungu na kama ilivyo katika usemi maarufu kuwa kila mtu ni mchunga basi kila Mbuge ajue ataulizwa juu ya nafasi ya uwakilishi aliopata Je! amewafanyia nini watanzania?
Khatibu aliwakumbusha wabunge hali ya Amani na utulivu iliyopo leo Tanzania inahitaji kulindwa kwa nguvu zote. Hivyo kanuni na katiba mpya watakayoipitisha iwe ni kwa lengo la kubakisha hali ya usalama na Amani iliyopo nchini. Na kuasa kuwa ni amani ya kweli na utulivu tu ndio njia pekee itakayowawezesha waumini wa Kiislamu wataweza kuingia Misikiti na kuabudu kwa amani, Wakristo nao wataweza kuingia Makanisani na kuabudu kwa amani.
Mwisho wa hutuba yake Sheikh alikemea kwa ukali tabia ya Uhalifu kwa Matumizi ya Tindikali inayowachwa kukua na kushamiri ndani ya taifa la Tanzania. Akasema yeye anaamini kuwa serekali ina nguvu na mamlaka ya kuwatia nguvuni wahalifu hao. Aidha alikwenda mbali kuashiria kuwa ndani ya mkoa wa Arusha pekee yamekariririwa matukio kadhaa ya Masheikh mbalimbali kumwagiwa na Tindikali na kupata majeraha makubwa na hata kuhatarisha maisha yao. Akaisa serikali kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa makundi haya yatashamiri na kuvuruga amani na Utulivu tunaojivunia.
….Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika…

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 7, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: