Kiongozi Muadhamu akutana na Waalimu (07/05/2014)

 

ujumbe kamili

Ayatollah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumatano asubuhi alikutana na maelfu ya walimu. Akizungumza katika mkutano huo, Kiongozi muadhamu alieleza kuwa kupata elimu, mafundisho, na kuimarisha maadili ni mambo makuu matatu matukufu yenye wito. Alisisitiza umuhimu wa utekelezwaji wa mpango wa kubadilisha mfumo wa elimu, na kuongeza kuwa “msaada kamili kwa ajili ya Tasisi (inayoshughulikia Mabadiliko ya mfumo wa elimu) hili kubwa ni uwekezaji endelevu kwa manufaa ya baadaye ya watoto wa Taifa hili na kwa maendeleo ya haraka ya Raia vipenzi wa Taifa la Iran katika maeneo ya kidunia na maisha ya Akhera “.

Akiashiria vipimo vikuu ya ufundishaji, Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alifafanua kuwa: “Kufundisha jinsi ya kupata elimu ni wajibu muhimu, lakini kilicho muhimu zaidi ni kuwafundisha watoto na vijana jinsi ya kufikiri.”

Ayatollah Khamenei alisema kuwa na mtizamo finyu na usomaji wa goigoi unalemaza jamii, akasema: “Kama wanafunzi watajifunza kutoka kwa walimu wao jinsi ya kufikiri katika njia sahihi, mustakabali wa nchi utakuwa umejengwa juu ya msingi wa akili na kufikiri hivyo, walimu wapenzi wana wajibu mzito katika kuhakikisha suala hili.

Kiongozi Muadhamu alielezea kuwa mafundisho ya Maadili mema kivitendo kuwa ni wito na ni kipengele muhimu cha tatu katika ufundishaji, akisisitiza amesema: “kufikia malengo ya fahari na maadili mema inahitaji kuwa na watu wenye subira, busara, dini, ubunifu, ukarimu, ujasiri, Uchamungu, Upole na wenye bidii na kujituma na Walimu wanachukua jukumu la msingi, na muhimu la kudumu katika kujenga watu kama hao.”

Alitoa wito kwa viongozi wenye dhamana ya kulinda mfumo wa elimu kuweka umakini mkubwa katika utekelezaji wa mpango wa kubadilisha mfumo wa elimu, na kuongeza: “ili kutekeleza mpango huu wa msingi na wenye manufaa inahitaji ramani ya kivitendo inayotekelezeka. Ramani hii inahitajika kuandaliwa na kutekelezwa hatua kwa hatua kwa kushirikiana na Baraza kuu la Mapinduzi ya Utamaduni”.

Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria kuwa Nguvu kazi  ni suala jingine muhimu sana katika mfumo wa elimu, na kuongeza kusema: “Taasisi hii aghalabu hukutana na kuwasiliana moja kwa moja na Mamilioni ya watu hivyo, Mameneja wake na viongozi wake wa juu wanapaswa kuwa ni watu wenye sifa maalumu”.

Ayatollah Khamenei akiwaambia waalimu amesema kuwa: “Vipaumbele vyenu lazima vilenge kwa vijana wana mapinduzi, wenye dini, shauku, motisha na vikosi venye bidii. Mnapaswa kuwa makini na kufahamu kwamba kufikia malengo ya mfumo wa elimu ndio jambo pekee ambalo viongozi na mameneja wa taasisi hii wanapaswa kulenga.”

Kiongozi muadhamu alisisitiza umuhimu wa kutegemea nguvu za kimapinduzi na kidini katika mfumo wa elimu, na kutilia mkazo hili alisema: “lengo kuu la watu na viongozi ni kujenga jamii ya kupigiwa mfano na yenye maendeleo ya juu Kimaada, kiroho na katika maeneo ya maadili – chini ya kivuli cha Uislamu na Qur’ani Tukufu. Kuchukua njia ndefu ya kufikia lengo hili inahitaji kujenga jamii bunifu, yenye akili pevu na pana na kizazi chenye Malengo kwa kupitia mfumo wa elimu. Kazi hii inaweza kufanyika vema kwa kupitia makundi ya Mameneja wenye wenye dini na wanamapinduzi.”

Alisema kuwa kuingiza ukereketwa wa vyama vya kisiasa na upendeleo ni sumu kwa mfumo wa elimu, na kuashiria kuwa: “Kwa bahati mbaya, mtizamo kama huu ulikuwa kubwa katika zama fulani na ulisababisha hasara kubwa”.

Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza kwamba mashirika yote hasa kwa Asasi za kiserikali zinazohusika na bajeti, zinapaswa kusaidia mfumo wa elimu.  Alikariri kuwa: “Kadiri tunavyozidi kuwekeza zaidi katika mfumo wa elimu, ndivyo tutakavyopata matokeo mazuri zaidi hii ni kwasababu taasisi hii ni mzizi na msingi wa mafanikio yote katika wakati huu wa sasa na katika siku zijazo”.

Ayatollah Khamenei alifafanua kuwa kuweka kipaumbele katika vitabu vya kiada ni jambo muhimu sana, na kuongeza: “Vitabu vya kiada lazima viboreshwe. Havipaswi kuwa na Maudhui yoyote dhaifu na yenye kupotosha iwe ni kisiasa au kidini – na visipotoshe ukweli. Hivyo basi, viongozi wanaohusika na uandaaji wa vitabu vya kiada wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa usahihi kamili na uaminifu. “

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on May 9, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: