Kiongozi Muadhamu Aonana na Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu

03/06/2014
20140603Anga ya Husainia ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) mjini Tehran imehinikiza uturi wa kutuliza nyoyo wa maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu, katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kutukufu Imam Zaynul Abidin, Aliyyu bnil Husain maarufu kwa lakabu ya Imam Sajjad AS. Wahadhiri, maqarii na “mahufadh” bora wa mashindano ya thelathini na moja ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu, wamefanya mahafali ya kuwa na mapenzi na kuwa karibu na Qur’ani Takatifu, mahafali ambayo yamehudhuriwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika mkutano huo, Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja lengo la mwisho na kuu la kuhifadhi na kusoma Qur’ani kuwa ni kuelewa na kutendea kazi mafundisho yake pamoja na kuwa na ukuruba na mapenzi makubwa kwa maneno ya Mwenyezi Mungu.
Aidha amebainisha kuwa, uongofu wa Mwenyezi Mungu na kufahamu vigezo vikuu vya Qur’ani katika masuala nyeti kama vile kumtambua adui, ni mambo ambayo yanapatikana kupitia kuwa na ukuruba na mapenzi na Qur’ani Takatifu.
13_5389852b4637cAmesisitiza kuwa: Kuwa karibu na Qur’ani Tukufu, kuwa na tadibiri na kuzama ndani ya maana na mafundisho ya Kitabu hicho kitukufu, ndiko kutakakouletea umma wa Kiislamu heshima uliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, hatua ya mabarobaro na vijana wa Iran ya kuipokea vizuri harakati ya Qur’ani nchini Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni neema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Ameongeza kuwa: Mapenzi na kuwa karibu na Qur’ani, kunaifanya jamii izidi kuwa karibu na utekelezaji wa mafundisho muhimu sana ya kitabu hicho na kwamba hilo ndilo lengo bora zaidi na la juu kabisa la kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.
Vile vile amesema, kuwa karibu na Qur’ani Takatifu ni ishara ya kuwa tayari moyo wa mwanadamu kwa ajili ya kupokea uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuongeza kuwa: Matatizo makubwa yanayoukumba ulimwengu wa Kiislamu leo hii yanatokana na ulimwengu huo kujiweka mbali na mafundisho ya Qur’ani na matokeo yake ni Waislamu kughafilika na njama na ukhabithi wa maadui wa Uislamu.
6_5389850ba07dfAyatullah Udhma Khamenei ameitaja njia ya kufidia mapungufu hayo makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu kwamba ni kuwa na welewa wa kina kuhusiana na vigezo vya Qur’ani Tukufu na kufafanua zaidi kwa kusema: Baada ya kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, maadui wa Uislamu walizidisha njama zao dhidi ya Uislamu na kuzifanya tata zaidi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kusema: Siasa za maadui wa Uislamu ni kuzusha vita vya ndani vya kupokezana, na kuwafanya ndugu kuuana wao kwa wao katika jamii za Waislamu, na kwamba kitu kinachosikitisha zaidi ni kuwa, kuna baadhi ya watu katika umma wa Kiislamu hawazioni siasa hizo za maadui na wako tayari kushirikiana na mashetani kuendesha vita dhidi ya ndugu zao Waislamu, bali wako tayari hata kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Waislamu wenzao.

4_538984fe98179Vile vile amewashukuru wote walioendesha na walioshiriki mashindano hayo ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu na kuongeza kuwa: Umma wa Kiislamu unaweza kufikia kwenye heshima uliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa baraka za kuwa na mapenzi na kuwa karibu na Qur’ani Tukufu.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammadi, Mwakilishi wa Faqihi Mtawala ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Wakfu na Mambo ya Kheri ya Iran, ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa sikuu za mwezi wa Shaaban hususan sikukuu ya kukumbuka siku ya kuzaliwa Imam Sajjad Alayhis Salaam na huku akiashiria kiwango cha juu cha mashindano hayo na jinsi mashindano ya mwaka huu ya 31 ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu yalivyopokewa na washiriki wengi kutoka mataifa tofauti amesema: Katika mashindano ya mwaka huu, nchi 71 za mabara tofauti duniani zimetuma wawakilishi wao ambapo mashindano hayo yalisimamiwa na majaji 10 kutoka nje na watano kutoka Iran huku wajumbe watatu wakiwa ni watazamaji.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 4, 2014, in Habari and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: