Historia ya Msikiti Mtukufu wa Makka

lvl120140620103546

Maka (Kiarabu Makkah, Zamani Macoraba) Mji Magharibi mwa Saudi Arabia, mji mkuu wa Al-Hijaz katika jimbo la Hijaz karibu na Jiddah. Waislamu waliuita mji huu “Umm al-Qora”, maana yake “Mama wa Miji” jina hili limetokana na utakatifu wake baada ya kuwa sehemu aliyozaliwa Mtume Muhammad (saw). Makka iko katika bonde jembamba, bonde lenye mchanga, iliyozungukwa na vilima tasa.

Hakuna mji katika historia ya Mwanadamu umepewa heshima na utukufu kama heshima iliyopewa mji mtakatifu wa Makkah. Kuna eneo la Al Kaaba tukufu, Hodhi tukufu la Uislamu, umbo mchemraba, chumba kimoja kilichojengwa kwa mawe kaaba ipo Makka Saudi Arabia, ambayo ilikuwa nyumba kwanza kujengwa kwa ajili ya ibada ya Mwenyezi Mungu. Kama ilivyo imarishwa na nabii Ibrahimu na mwanawe Ismael, (Amani ziwe juu yao wote) Kaaba ni hodhi takatifu ambapo waumini hufanya Hija. Utamaduni wa kiislamu ulichukulia kuwa tayari eneo hili lishakuwa eneo kwa ajili ya Hija na hivyo kulifanya patakatifu na muhimu zaidi kabla ya uislamu bara la Arabia. (Kiarabu chake “haram”)

Mlango wa Qaaba una urefu wa futi saba kutoka ardhini, hakuna Madirisha. ndani yake kumepamba na kurembwa sana. Kuna pande nyingi takatifu katika Nyumba ya kaaba tukufu kwa ajili ya kutafakari, mmoja ya kona hizo za kale na kongwe ni eneo alilosimama Nabii Abraham wakati alivyokuwa akiijenga hekalu hilo.

Muda mrefu kabla ya Muhammad (saw) Kaaba ilikuwa ni kitovu cha ibada na hazina ya uwepo wa masanamu yaliyokuwa yakiletwa na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali. Baadhi ya riwaya zinasema kuwa Adam ndiye aliweka misingi wa jingo la Kaaba, Ibrahimu akaja kurekebisha na kukarabati, na Mamia ya manabii wamezikwa kuizunguka kaaba.

Baadhi ya wasomi wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu aliteremsha msingi ya wa nyumba hii kutoka mbinguni na ilikuwa ni nyeupe sana na nyepesi kuliko theluji, lakini baadaye ikawa giza na nyeusi kwa kushikwa na waumini. Kwa ujio wa Uislamu, utakatifu wa Makkah ulithibitishwa rasmi na heshima yake iliongezeka, na ikawa hodhi tukufu na jiwe jeusi katika moja ya kona yake ya kusini-mashariki na Masalio yaliokuwa yakitumika kuabudu masanamu yakabadilishwa na ikawa kitu kitakatifu cha imani.

Mahujaji wakiwasili katika mji wa Makkah, hulibusu jiwe jeusi kama wajibu wao wa kwanza. Nje yake kuna kisima kitakatifu, cha Maji ya Zamzam, ambacho kilitumiwa na Hajar, mama wa mtoto wa Ibrahimu Ismael. umuhimu wa pekee wa Kaaba, jiwe-jeusi na Zamzam ambazo Waislamu wote wachamungu huvitamani, imekuwa labda moja ya sababu kubwa katika kubuni maana ya Umoja kati ya wafuasi waliotawanyika wa Uislamu.

Kwa kuwa mji ambapo Mtume Muhammad (SAW) alizaliwa na ambapo ufunuo (wahy) ulishuka juu yake na na kutumwa na Mwenyezi Mungu kama mjumbe na nabii kwa walimwengu wote kuwaita katika ibada ya Mwenyezi Mungu mmoja bila ya mshirika yoyote. Msikiti mkubwa kuliko yote duniani ni al-Masjid al-Haram (Nyumba Tukufu) katika mji wa Makkah, hili ni uthibitisho wa lile ambalo Mwenyezi Mungu amelitaja katika Qur’an Tukufu: Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote” (3:96)

Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu ameifanya Kaaba, kuwa Qibla au mwelekeo ambayo Waislamu wote huelekea katika kusali Ibada zao, na Kuhiji (Hajj) kwenda Makkah ilisimamishwa kama nguzo ya ibada katika Uislamu. utakatifu na utukufu wa Makkah imehifadhiwa katika historia ya Uislamu.

Kuhiji ni wajibu wa kila mtu mzima Muislamu mwanamke na Mwanaume na mwenye afya ya kuweza kufanya Hijja, Hijja inaweza tu kufanyika mara moja kwa mwaka na hutokea katika mlolongo na tarehe maalum, wakati wake ni wiki mbili za Mwanzo za mwezi wa Kiislamu ya Dhu al-Hijja. Kwa kuwa Mwaka wa Kiislamu unafuata mzunguko wa jua na bila hitilafu, Hijja kama ilivyo kwa sikukuu zote za Kiislamu ni huru na hazitegemei msimu.

Nukuu ya kwanza ya kihistoria kutaja kuhusu kujengwa kwa Kaaba ilikuwa 605 Baada ya Hijira, kabla hata ya Utume wa Muhammad (saw). Mgogoro ulizuka kati ya makabila ya Makka kuhusu wapi pa kuliweka jiwe jeusi, kila kabila waliona kuwa heshima ya kuweka jiwe jeusi lazima wapewe wao. Ili kutatua mzozo, Mtume Muhammad (saw) akaweka jiwe jeusi katika vazi lake (kitambaa) na akwataka  wawakilishi wa kila kabila kushika sehemu ya kitambaa na kunyanya juu jiwe jeusi. Kisha yeye Mtume akalichukua jiwe jeusi na kuliweka katika sehemu yake sahihi katika ukuta wa Kaaba. Kaaba ilibakia katika hali hiyo bila mabadiliko hadi ulipokuja Uislamu ndipo masanamu ambayo yaliokuwa ndani yake na yale yaliokuwa yakiizunguka yaliondolewa.

Kwa Waislamu, Kaaba ni “Nyumba ya Mwenyezi Mungu”, Na huoshwa kila mwaka na kufunikwa na kitambaa cha hariri nyeusi. Kaaba imepanuliwa  sana tangu wakati wa Muhammad (saw), uwa wa msikiti baadaye ulijengwa karibu yake na hivi karibuni lango la dhahabu imara limeongezwa.

My Address

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 20, 2014, in Hotuba na Mawaidha and tagged , , , . Bookmark the permalink. 3 Comments.

  1. Inamaana mwanzo walikuwa wakiswali waabudu masanamu?? Au nmeelewa vibaya

    Like

  2. Ma sha Allah,Allah anijaalie kuiona Kaaba na kufika kuhiji,Amiin

    Like

  3. Ma sha Allah Allah anijalie kuiona kaaba nakufika kuhiji,Amiin

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: