Misikiti na Miezi Mitukufu

ScreenShotMwenyezi Mungu alipendelea baadhi ya maeneo katika ardhi na kuyaita ni nyumba zake na kuwafanya wageni wa nyumba hizo kuwa wageni wake pia. Katika Hadith tukufu anasema, ” Misikiti ni nyumba zangu juu ya Ardhi. Rehema na Amani iwe kwa mtumishi wa Mwenyezi Mungu anayejitakasa nafsi yake katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, basi nitembeleeni katika nyumba yangu. Mwenyeji lazima atamkirimu mgeni. “

Picha ya Ukarimu wa Mwenyezi Mungu

  1. Ukarimu kwa wageni wa nyumba yake huanza pale tu hatua ya kwanza inapopigwa kuelekea msikitini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) anasema, “Mtu anayepiga hatua kuelekea msikitini Mwenyezi Mungu, atamtunza kwa kumpa thawabu kumi, kumsamehe makumi ya Madhambi na kumnyanyua daraja kumi kama malipo kwa kila hatua anayopiga mpaka atakaporudi nyumbani.”
  2. Lakini ukarimu wa Mungu Mwenyezi Mungu unaendelea kwa atakaye kaa msikitini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) anasema kumwambia Abuu Dhar, “Mwenyezi Mungu atawapa daraja ya ziada katika pepo na Malaika watakuwa wakikuombea dua kwa kila pumzi utayopumua huko …”
  3. Aina hii ya ukarimu wa Mwenyezi Mungu huzidi pale utakaposali katika msikiti kwani msikiti utakuwa shahidi mzuri katika siku ya kiyama. Imam Swadiq (AS) anasema, “Mara uwapo katika msikiti, Sali maeneo tofauti tofauti kwani kila eneo litashuhudia hiyo sala yako siku ya kiyama.”

Wajibu wa Msikiti

Baadhi ya ujira mkubwa tulioujadili hapo juu ni kutokana na mchango mkubwa wa msikiti katika maisha ya mtu na jamii. Kwa kweli, msikiti ni:

  1. Nyumba ya Qur’an: Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) anasema, “Misikiti imejengwa kwa ajili ya Qur’an tu.”
  2. Nyumba ya Sala: Imam Swadiq (as) anasema, “Njooni Misikitini: Hizo ni Nyumba za Mwenyezi Mungu juu ya ardhi … hivyo ombeni dua na kusali sana humo.”
  3. Nyumba ya Maarifa: Mtume mtukufu wa Mwenyezi Mungu (SAW) pia alisema, “Yeyote anayekwenda Msikitini kwa nia ya kujifunza au kufundisha atalipwana ujira sawa na ujira wa Hija iliyokamilika.”
  4. Nyumba ya Udugu: Imam Swadiq (as) anasema, “Mwenye kwenda Msikitini mara kwa mara hatorudi mikono mitupu isipokuwa atapata mambo Matatu (miongoni mwa hayo) ni ndugu atakayemfaidisha …”
  5. Nyumba ya Ueledi wa Siasa: Hakika ni kutoka msikiti, Mtume (SAW) alikuza na kuamsha mtazamo wa kisiasa katika roho za Waislamu. Imam Khomeini, Mungu aibariki nafsi yake, pia alisema, “Msikiti ni kitovu cha Mikutano ya kisiasa”
  6. Nyumba ya kutetea Waislamu: Waislamu walikuwa wakitoka msikitini chini ya amri ya Mtume (SAW) kutetea Uislamu. Vivyo Hivyo, Imam Khomeini, Mungu aibariki nafsi yake, pia alisema, “Msikiti ni moja ya mitaro ya kutetea Uislamu na Kibla ni mahali pa vita.”

Matokeo yake, msikiti imekuwa ni hatua ambayo Mujahidina ambao hutetea Uislamu hutokea na ambao hutengeneza njia kuelekea kwa Imam Mahdi. Mashahidi wengi wamepata shahada zao misikitini baada ya kuijenga misikiti ndani ya nyoyo zao.
Hii ndio sababu Imam Khomeini, Siri zake zibaki takatifu, alisisitiza umuhimu wa misikiti na yeye alikuwa akisema, “Kuweka na kutunza Misikiti ni moja ya mambo ambayo uwepo wa Uislamu leo unategemea,” na aliongeza kusema “Msiitenge Misikiti: Kwani ni wajibu na ambao unaowahusu”.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 20, 2014, in Hotuba na Mawaidha and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: