Umuhimu wa Msikiti

ScreenShotAya ya Quraan Kuhusu Msikiti

“Usisimame kwenye msikiti huo kabisa. Msikiti ulio jengwa juu ya msingi wa uchamngu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanao jitakasa”. Quraan (9:108)

Uchambuzi wa Watu hawa:

“Na jengo lao hilo walilo lijenga litakuwa sababu ya kutia wasiwasi nyoyoni mwao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.” Quraan (9:110)

“Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.” Quraan (9:18)

Kwanini tumeamrishwa kuheshimu misikiti

Imesimuliwa na Abu Basir kuwa Imam Jafari Swadiq (as) aliulizwa sababu gani misikiti inatukuzwa. Imam akajibu kuwa “Kwa hakika imeamrishwa kutukuza misikiti kwa kuwa ni nyumba za Mwenyezi Mungu Ardhini”.
Hivyo basi imesimuliwa kuwa Imam Ali (as) amesema kuwa “Kukaa Msikitini ni bora kwangu kuliko kukaa katika pepo. Kwa kuwa matakwa ya nafsi yangu ni kukaa peponi na matakwa ya Mwenyezimungu ni katika Msikiti”.

Kwanini Mazingatio makubwa yawe katika Msikiti?

Imesimuliwa kuwa Imam Jaafari Swadiq (as) amesema kuwa “Mwenyezi Mungu hajawahi kuabudiwa kwa namna sawa na ukimya (kwa upole) na kwa kwenda katika Nyumba (Msikiti) yake.”

Kwa nini kuna msisitizo huu mkubwa kutoacha kwenda Msikitini?

Imesimuliwa pia na Imam Jaafari Swadiq (as) kuwa Amirul Muuminina Ali (as) alipokea habari kuwa baadhi ya watu hawasali katika Msikiti. Ndipo Imam akatoa hutuba na kusema: “Kuna watu ambao hawahudhuri katika Sala pamoja nasi katika msikiti wetu. Hivyo basi watu hawa na wasitoke kula wala kunywa na sisi. Wasitutake Ushauri, Wasioe kwetu na wasichukue chochote katika Mali zetu, isipokuwa tu pale watakapohudhuria sala ya jamaa pamoja nasi”…
Kisha Waislamu wakacha kula, kunywa, na kuoa kwao mpaka pale waliporejea katika sala za Jamaa pamoja na waislamu wengine.

Imesimuliwa kutoka kwa Razeek kuwa Imam Swadiq (as) alisema: “Yeyote atakeyeswali jamaa katika nyumba yake kwa kupuuzia Msikiti, ni kama vile hajaswali kabisa hii ni pamoja na waliosali pamoja nae isipokuwa kama walikuwa na kikwazo kilichowazuia kwenda Msikitini”.

Mtume mtukufu (Rehema na amani ziwe juu yake na kwa watu wa familia yake) amesema: “Hakuna sala ya majirani karibu na Msikiti isipokuwa lazima iswaliwe ndani ya msikiti huo”.

Kwanini kuna fadhila kubwa kiasi hichi kwa kujenga Msikiti?

Imam Jaafari ibn Muhammad Swadiq (as) amesimulia kutoka kwa baba yake kuwa: “Kwa hakika pindi Allah (sw) atakapotaka kuadhibu watu wa ardhini akasema “Kama wasingelikuwepo wale wanaopendana kwa ajili yangu na wanajenga Misikiti yangu na wanatubia kwa wakati kabla hapajakucha, kwa hakika ningeliteremsha chini adhabu yangu”.

Kwanini Misikiti ina hadhi kubwa kwa Mwenyezi Mungu na kwa nini imekokotezwa sana kwenda msikitini?

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesimulia kuwa “Yeyote atakaye uendea Msikiti wa Mwenyezi Mungu kwa hakika atalipwa kwa kila hatua thawabu kumi na atafutiwa Madhambi kumi kutoka kwake na atainuliwa daraja kumi”.

Msikiti utakuwa na Faida, Je ni zipi?

Imesimuliwa na Fadhl ibn Abdul Malik kuwa Imam Jaafari Swadiq (as) amesema “Ewe Fadhl, Hakuna anayekwenda Msikitini kutoka katika kabila isipokuwa ni wa mwanzo wao, na hakuna katika Familia isipokuwa Mtukufu wao. Aendae Msikitini harudi isipokuwa atakuwa na moja ya sifa Tatu (3): Eidha dua (sala) atakayosoma/kusali, Itamuingiza peponi, au dua (sala) atakayosoma/kusali Allah atamlinda kwayo na Mabalaa ya ulimwengu, au atapata ndugu atakayemfaidisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”.

Imam Ali (as) pia alikuwa akisema: “Yeyote atakayekuwa akienda Msikitini mara kwa Mara, atapata moja kati ya mambo nane (8); Ndugu atayemfaidisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Maarifa (elimu) Mazuri, Aya muhimu, au atasikia neno litakalomuongoa, Rehema itarajiwayo, Neno litakalomtoa katika uovu, au kuacha dhambi kwasababu ya kuogopa au aibu”.

Na Mwisho:
Imam Swadiq (as) amesema kuwa: “Matatu hulalamika kwa Mwenyezi Mungu (sw); Msikiti uliopuuzwa ambao watu wake hawaswali ndani yake, Mwanazuoni katikati ya wajinga, na Quraan iliyotundikwa na kupigwa na mavumbi wakati hakuna wa kuisoma”.

 My Address

 

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 20, 2014, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: