TAMKO: KUPINGA KUDHALILISHWA MTUME MUHAMMAD (SAWW) KULIKOFANYWA NA JARIDA LA CHARLIE HEBDO NCHINI UFARANSA

TAARIFA KWA UMMA

image

Harakati ya hawza Imam Swadiq chini ya Uongozi wa Samahat Sheikh Hemedi Jalala inaungana na Waislamu wote duniani na Wapenzi wa Amani kokote walipo kupinga kwa Kauli thabiti hatua zozote zinazochukulia na Serikali za nchi za Magharibi na Marekani kuchochea vitendo venye lengo la kuamsha chuki na machafuko ya Kidini ulimwenguni.
Tunatamka wazi kuwa kitendo cha Jarida La Charlie Hebdo kuchapisha picha za Katuni zenye kumdhalilisha Mtume Muhammad (saww) ni kitendo cha Kifedhuli, ni Kashfa na Matusi ya wazi kwa Mtume wetu Kipenzi chetu Muhammad (saww) Waislamu wote bali na wapenda Amani duniani kote. Ni kitendo kisichovumilika na hakuna Muislamu awezae kustahamili ghadhabu zake kwa kitendo hichi.
Aidha tunatambua kuwa vitendo hivi vinafanywa na makundi ya Watu waovu, wasio na Imani ya Dini wala Ubinaadamu, wanaopata kinga ya kulindwa na ufadhili wa Idara za Kijasusi za Mataifa na dola za Magharibi kwa lengo lao ovu la kutaka kuupaka Matope Uislamu na Waislamu duniani, ili kuzusha na kuchochea hasira miongoni mwa waumini wa dini tofauti tofauti na hatimaye kuzalisha Makundi ya Waumini wenye misimamo mikali na yenye kuvuka mipaka kwa lengo la kuzusha fitina, Machafuko na Mauaji baina ya waumini wa dini tofauti tofauti duniani.
Kuheshimu Imani, Mila, Tamaduni na Matukufu ya Imani za Dini tofauti tofauti ni kanuni ya Msingi ya Umoja wa Kimataifa, tunawataka wakuu wa Dola za Magharibi na Amerika kuwa Vinara kuziheshimu na kutekeleza kwa vitendo kanuni na Haki hizi. Haitoshi tu kwa Viongozi hao kukiri makosa ya ubovu wa sera za nchi zao, bali wanapaswa kuchukua Maamuzi sahihi na kwa wakati Muafaka kuleta Utengamano na Mahusiano mema baina ya Imani za dini tofauti tofauti katika Mataifa yao. Maamuzi yasio na Upendeleo wa kiimani na yenye Maslahi sawa kwa raia wa Imani tofauti wa Mataifa yao. Kwani ni kwa Maamuzi wanayofanywa yenye upendeleo wa Makusudi kwa Upande mmoja wa Imani ya Dini na kukandamiza upande mwingine ndio chanzo cha kuzuka makundi yenye misimamo mikali na yenye mikakati ya kulipiza kisasi na kufanya vitendo vya Kigaidi. Mfano “Kama mauaji  ya idadi fulani ya watu Katika Jengo la Gazeti la Uchochezi na Udhalilishaji wa Matukufu ya Dini Uislamu Charlie Hebdo, ni tukio baya na kupelekea Maandamano ya kitaifa kuitishwa nchi mbalimbali za Magharibi, Kwanini basi Mauji ya Wapalestina 2,000 wakiwemo watoto 578 yaliyofanywa na Taifa hasimu la Israel isionekane ni kitendo Kiovu  cha Kigaidi na Kishetani? Kwanini viongozi wa Magharibi na Amerika wanatumia gharama kubwa kukandamiza maandamano ya Amani yanayoitishwa katika nchi zao kulaani Vitendo viovu na vya kigaidi vinavyofanywa na Taifa ghasibu la Israel?
Sambamba na hili tunaungana na Ulimwengu mzima kupinga Vitendo vyovyote vya kigaidi vinavyofanyika duniani kote dhidi ya Nchi na au binaadamu yeyote asiye na hatia.
Hakuna uhuru usio na Mipaka, Matumizi mabaya ya Vyombo vya habari na Mawasiliano, Imani na Misimamo inayokiuka mipaka ya Dini na Sheria za Nchi, Mauaji na Udhalilishaji wa Viongozi wenye kuheshimiwa wa Dini na Nchi, Kukashifu na kutakana Matukufu ya Dini na uvunjaji wa Alama za dini zinazoheshiwa na waumini wa Dini hizo, ni Vitendo Viovu visivyokubalika na vya kukemewa na kupigwa vita na kila Mwanaadamu mpenda Amani.
Tuungane wananchi wote na walimwengu Mzima kupinga Propaganda na kampeni chafu zinazofanywa na Makundi ya Wapinga Mungu, wenye lengo la kumaliza kizazi cha Mwanaadamu mwenye Imani ya Dini. Tushikamane kuwaumbua na Mbinu zao ili tuifanye dunia yetu kuwa Mahala salama na Amani kwa Wanaadamu wote.
Mwisho.

Imetolewa na:
Leo Tarehe 14/01/2015 na
Ofisi ya Habari Hawza Imam Swadiq
Kigogo, Dar es Salaam, Tanzania.
Tanzania.
asadiqmedi@gmail.com

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on January 15, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: