Tukabiliane na hujuma dhidi ya Uislamu kwa kuarifisha Uislamu halisi

(12/03/2015-12:47)

40564_483Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Alkhamisi amekutana na Mwenyekiti na wawakilishi wa Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Iran ambapo amesema kutekelezwa Uislamu kamili ndiyo takwa la Mwenyezi Mungu na lengo kuu la utawala wa Jamhuri ya Kiislamu hapa nchini. Ameashiria udharura wa kuoneshwa Uislamu halisi mbele ya njama za mabeberu za kutaka kueneza hofu kuhusu Uislamu katika mataifa mbalimbali na akasema: Kuna udharura wa kujiepusha na mtazamo wa kijuujuu wakati wa kuchunguza sababu na njia za kukabiliana na changamoto zilizopo na kuchunguza kwa kina sababu za mambo mbalimbali ili kuweza kuyaendesha vyema na kwa njia za kimantiki.

Ayatullah Khamenei amezungumzia pia sifa na huduma za Ayatullah Muhammad Yazdi na kuongeza kuwa, kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wataalamu ni hatua mwafaka. Amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa makini na bila ya makelele na unaweza kuwa kigezo cha kuigwa na taasisi nyingine.

40576_253Akitumia aya za Qur’ani Tukufu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Uislamu unataka kutekelezwa misingi na sheria zote za dini. Amesema kuwa katika mafundisho ya Uislamu hakuna kitu kinachoitwa dini ya kiwango cha chini, kwa msingi huo kuna ulazima wa kutekelezwa vipengee vyote na kamili vya Uislamu na kufanya bidii na harakati ya kudumu katika njia hiyo.

Ayatullah Khamenei amesisitiza udharura wa kulindwa na kuimarishwa pande zote za Uislamu katika “sura” na “sira” yake na kuongeza kuwa: Kulinda sira ya Uislamu kuna maana kwamba Uislamu, malengo na thamani vinapaswa kuwekwa mbele katika mazingira yote ya harakati ya nchi, wananchi na viongozi, na kutayarishwa mipango mizuri ili kuhakikisha jambo hilo linatimia. Amesisitiza kuwa watu wote hapa nchini wanapaswa kufanya harakati katika njia hiyo.

Ayatullah Khamenei amewataja mabeberu wa kimataifa kuwa ndiyo kizuizi kikuu cha harakati ya kuelekea kwenye Uislamu kamili na kuongeza kuwa: Hujuma inayofanywa na vyombo vya kipropaganda na kisiasa vya Wazayuni ili kueneza hofu kuhusu Uislamu ni kielelezo cha woga wao wa kutokemezwa maslahi yao haramu.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia baadhi ya matamshi ya maadui wa utawala wa Kiislamu hapa nchini wanaosema wanataka kubadili mwenendo wa Jamhuri ya Kiislamu na si kubadili utawala huo na kusema: Maana ya kubadili mwenendo wa utawala wa Kiislamu ni kulifanya taifa la Iran lishindwe kufanya harakati ya kuelekea kwenye malengo na thamani zake na kutekeleza Uislamu kamili, na lengo hilo kwa hakika lina maana ya kubadili utawala na kuangamiza sira ya dini katika harakati ya umma ya utawala wa Kiislamu ambako mara hii kunafanyika kwa kutumia njia hiyo.

Amesema kuna udharura wa kujiepusha na misimamo isiyo ya kimantiki katika kukabiliana na hujuma ya kuwatisha watu kuhusu Uislamu na akasema: Propaganda za kueneza hofu baina ya watu kuhusu Uislamu kwa hakika ni tarjumi na kielelezo cha hofu na woga wa madhalimu wa kimataifa mbele ya Uislamu wa kisiasa na Uislamu uliopo hivi sasa katika maisha ya mataifa mbalimbali ambao taifa la Iran ndilo linalobeba bendera ya harakati ya kuuimarisha.

Ayatullah Khamenei amesema inawezekana kubadili hujuma hiyo dhidi ya Uislamu na kuifanya fursa nzuri badala ya kuwa tishio. Ameongeza kuwa jitihada za kudumu za kuyatisha mataifa mbalimbali na vijana kuhusu Uislamu zinazusha swali katika fikra za walimwengu kwamba, ni nini sababu ya hujuma na mashambulizi hayo yote dhidi ya Uislamu?

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kutoa majibu sahihi ya swali hilo kupitia njia ya kuonesha Uislamu halisi kwa mataifa mbalimbali kuna baraka nyingi na kuongeza kuwa: Tunapaswa kufanya bidii na juhudi kubwa katika njia hiyo.

40578_697Akibainisha Uislamu halisi, Ayatullah Ali Khamenei amesema: Kufundisha Uislamu unaotetea watu wanaodhulumiwa na kukabiliana na madhalimu kunawahamasisha vijana na kuwafahamisha kwamba Uislamu una mipango na ratiba ya kivitendo ya kuwatetea watu wanaodhulimiwa na wasio na makimbilio.

Ayatullah Khamenei amesema sifa nyingine za Uislamu halisi ni kutetea akili na mantiki, kukabiliana na mitazamo finyu na fikra mgando na kupambana na hurafa. Ameongeza kuwa tunapaswa kuarifisha Uislamu wa kushikamana na mafundisho ya dini mkabala wa kutojali mafundisho hayo, Uislamu unaokuwa katika maisha ya watu mkabala wa Uislamu wa kisekulari, Uislamu unaokuwa rehema kwa matu dhaifu na Uislamu wa kupigana jihadi dhidi ya mabeberu; kwa njia hiyo tubadili mradi wa kuwatisha watu kuhusu Uislamu na kuufanya fursa ya kulingania Uislamu halisi kwa mataifa mbalimbali.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria changamoto zilizopo kati ya Iran na Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya ikiwemo kadhia ya nyuklia na akasema: Kuna ulazima wa kuchunguza chanzo cha changamoto na matatizo yaliyopo kwa kujiepusha na mitazamo ya kijuujuu, na kwa utaratihu huo tuweze kupata njia ya kimantiki ya ufumbuzi.

Ametolea mfano matatizo yaliyosababishwa na vikwazo na kuongeza kuwa: Upembuzi yakinifu unaonesha kuwa, sababu ya matatizo tuliyosababishiwa na vikwazo ni utegemezi wa nchi kwa mafuta na uchumi unaodhibitiwa na serikali na kutoshirikishwa wananchi katika masuala ya kiuchumi.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 16, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: