SAMAHATI SHEIKH JALALA MGENI RASMI: MAULID MADRASAT TAUHIID KINONDON MKWAJUNI.
18/04/2015:
Samati sheikh Hemedi jalala jana Usiku alihudhuria Mualiko wa Mawlid yaliyoandaliwa na uongozi wa Mawlid Tawhiid iliyopo Kinondoni Mkwajuni Dar-es-salaam.
Akihutubia Mamia ya Waumini na Wanafunzi wa Madrasa, Sheikh Jalala alibainisha wazi kuwa Wanao muogopa mungu, ni wale wenye ujuzi, na kwamba kazi ya kuwatengeza watoto ndio kuitengeza jamii, jamii inayowekeza kwa watoto, jamii hiyo ina mustakbali mzuri katika maisha yao.
Watanzania hususani waislamu wanao wajibu wa kutambua Madrasa zetu za dini, ndio zitakazotengeza jamii itakayotambua haki za watu, na kuandaa viongozi wazuri wa taifa hili, kazi hii ni ya kuungwa mkono na taifa, hakuna chombo cha kuwatengeza watu kama Madrasa, aidha aliwaasa wazazi na kuwaambia kuwa “elimu ya madrasa ndio itakayowafundisha watoto kuwatambua wazazi, elimu zingine ni zinafundisha ubinafsi na mtu kushughulikia tumbo lake, mkewe na watoto wake tu,
Aliendelea kusisitiza kuwa kaama wazazi mnataka kuangaliwa na watoto ni kuzienzi na kuziunga mkono madrasa za dini, Mtoto lazima atakujali na kukuombea dua, kwani madrasa kafundishwa pepo ipo chini ya nyayo za kinamama.
Mwisho aliwataka waislamu wote kuwa macho na chokochoko zinazoibuka za kutaka kuzichafua Madrasa za kidini na kuchukua tahadhari na makundi yanayotaka kubadili Vituo vya dini kuwa kambi za kigaidi, chokochoko hizi ni mashambulizi dhidi ya dini na hatua ya kutaka kuzifungia Madrasa ni kusambaratisha kiini cha uislaamu na Malezi bora, kinyume chake ni kutengenezwa jamii ya walevi, Mafisadi, Waporaji na kila Uovu. Aliwataka wazazi na waumini kushirikiana na waalimu na Serekali kunyooshea vidole makundi Maovu yenye nia ya Kuharibu Sura nzuri ya Madrasa zetu ili kuzilinda.
Posted on April 19, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0