KHUTBA YA IJUMAA: UMUHIMU WA MADRASA
Katika khutba ya ijumaaa aliyoitoa Maulana sheikh Hemedi Jalala leo tarehe 1/5/2015 katika masjid Ghadiir, kigogo post Dar e salaam –Tanzania: Maulana aliwataka waumini na waislaam kwa ujumla kuzienzi na kuzithamini maadrasa za watoto kwani zina mchango mkubwa katika malezi ya jamii. Alisema madrasa ni sehemu ya kutoa malezi kwa jamii na panaposomeshwa mtu kumjua mungu, na maadili na tabia nzuri, Maulana alionyesha hatari ya jamii kukosa madrasa ni kuzalisha watu wasio mtambua mungu,na watu wala rushwa na waongo .
Akizungumzia umuhimu wa madrasa katika jamii maulana Aliseama:” elimu katika umri mdogo ni kama mchoro katika jiwe, haufutiki, na amri ya kwanza aliyopewa mtume (s.a.a.w.w,) ni elimu,madrasa watoto wanafundishwa tabia nzuri, kuwasaidia watu wazima , kuwaheshimu wazazi,napia kuja kuwa ni viongozi bora wa jamii na kwa Taifa kwa ujumla.
Akiwaasa waumini na Taifa kwa ujumla, maulana alisema: kama jamii na Taifa linahitaji viongozi na watu wasiwe wala rushwa , waongo, wawe wazalendo,wakusanyaji kodi wazuri ni kuzienzi madrasa.
“Taifa hili kama lina hitajia kuifunga Taasisi ya Takukuru, kupata wakusanyaji kodi wazuri, rai wema na wasio waovu, na wala Rushwa basi ni kuzienzi madrasa, na akaitaka wizara ya elimu kuzienzi madrasa hizo na kuzitia nguvu kwa kuzipa posho kwani kazi zinazofanya zina mchango mkubwa kwa jamii na kwa Taifa kwa ujumla.
Posted on May 1, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0