WAJIBU WA WAUMINI KATIKA KIPINDI CHA GHAIBAT
WAJIBU WETU KATIKA KIPINDI CHA GHAIBAT
Katika kusheherekea mazazi ya imam wa zama Imam MAHDII Muntadhar (a.t.f.s) uongozi wa jamiat Mustafa – upanga Dar es salaam, leo jumatano asubuhi, uliandaa hafla ya mazazi ya imam Mahdii (as). Sambamba na sherehe hizo, kulizinduliwa kitabu kinachomwelezea imam Mahdii (as) kilichotungwa na Sheikh Mulabbah Saleh.
Akizungumza katika hafla hiyo, maulana Sheikh Hemed Jalala, aliwakumbusha waumini wajibu wao katika kipindi hiki cha kumsubiri imam akiwa katika ghaiba, alisema: kuna changamoto kubwa inayowakabili waislaam na watanzania kwa jumla, ambao ufumbuzi wake upo mikononi mwa wafuasi wa Ahlul bayt (as).nayo ni kumsoma na kumtambua Imam vizuri na kuyaeneza mafundisho sahihi kwa watu wote. “ kuweni na malengo ya kuwabadilisha watu kuujua uislaam sahihi wa mtume Muhammad (s.a.w.w)kuweni na yakini kua, mwenyezi Mungu na mtume wake na waumini (Imam Mahdii as) anakuoneni” fanyeni Mwenyezi Mungu ataona, mtume ataona na waumiini wataona.
“angalieni picha ya uislaam inavyooneshwa leo, uislaam wa kuchinjana, anayechinjwa anasema Allahu Akbar na anaechInja anasema Allahu Akbar, fanyeni haraka kuwaokoa watu , kwa kuwafundisha uislaam sahihi wa mtume (s.a.w.w), wajibu wa kukemea mauaji hayo, fikra hizo potofu na kueneza uislaam sahihi wa mtume ni nyinyi wafuasi wa watu wa nyumba ya mtume(s.a.w.w).
“tunauwezo mkubwa wa kuwabadilisha watu kwa sababu yupo anaetufatilia.watanzania wanasubiri wapewe fikra sahihi na nzuri ya uislaam, tusipoitumia nafasi hii, tutakuja kujuta.kipindi hiki cha kuzaliwa imam ni wajibu wetu kuiondoa fikra ya Takfiir na chinja chinja kwa Watanzania.alimalizia Maulana sheikh Jalala.
Posted on June 3, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0