MKUTANO WA AHLULBAYT WORLD ASSEMBLY UMEHITISHWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
Na mwandishi wetu Mohamed Juma Khatibu.
Dar es salaam Tanzania,
Taasisi ya Ahlulbayt World Assembly yenye makao makuu yake mjini Tehran imefanya kikao chake cha maandalizi ya mkutano mkuu wa Mwaka utakaofanyika nchi Iran Mwezi Augusti mwaka huu.
Katika kikao chake kilichofanyika jijini Dar es salaam ukumbi wa khoja-mtaa wa Indira gandi kiliwakusanya wanazuoni, Masheikh na Wanaharakati kutoka nchi takriban 15 za Afrika, baadhi ya nchi hizo ni Tanzania, Kenya, Uganda, kongo DRC, Kongo brazavile, Madagaska, Nigeria, Benin, Sierleon na nyunginezo.
Lengo likiwa, kukutana pamoja kujali njia za Tabligh na vikwazo vinavyo ikumba nchi za Afrika.
Akizungumza katika Mkutano huo Maulana Sheikh Jalala kama katika kufungua kikao alitoa ripoti ya jumla ya hali ya Tabligh kwa nchi ya Tanzania ambapo alisema Tabligh ilipitia hatua kadhaa, na kukumbana na changamoto nyingi lakini alimshukuru Mwenyezu Mungu na kusema kuwa kwa sasa Tabligh ndani ya nchi ipo ktk uhai, kwani Tabligh inafanyika katika hali ya kuridhisha sana na kupitia harakati ya Imamswadiq leo Waislamu Mashia na ndugu zao Ahlu suna ni kitu kimoja, leo Masuni kwa Mashia wanahudhuria Maulid kwa pamoja. Waislamu na Wakristo wanakaa vikao vya pamoja vya Amani na dini, Leo harakati inajivunia mahusiano mazuri na Serekali.
Baada ya Hotuba yake ambayo iliwasisimua wengi, washiriki wakatamani kutembelea hawza Imam swadiq anapofanyia kazi kujionea wenyewe,
Mawlana akiwafahamisha wageni wake kuhusu shughuli mbalimvali zinazofanywa na hawza Imamswadiq na msikiti wa kigogo.
Mmoja wa wageni waliotembelea Masjid Ghadir ni Mtoto wa Kiume wa Sheikh Ibrahim Zakyzak. Akiwa amesimama akiwashukuru vijana wa kigogo kwa ukaribisho wao na kutoa furaha yake kwa kuona jinsi imam khamenei anavyotambulika.
na wakati wa Magharib walifika hawza Imam swadiq na kuswali Masjid Ghadir swala ya jamaa na kutembelea madarasa na ofisi ya Mawlana walifurahi na kupongeza juhudi zinayofanywa na hawza imam swadiq.
Posted on June 14, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0