ANAEIHUBIRI AMANI ANAIHUBIRI DINI

DSC01163

      Maulana Sheikh Hemedi Jalala

ANAEIHUBIRI AMANI ANAIHUBIRI DINI
Maulana Sheikh: Hemedi Jalala, imam masjid Ghadiid-Kigogo Post Dar es salaam.
Akihutubia katika swala ya ijumaa iliyoswaliwa katika msikti wa Ghadiir-kigogo Post Dar es salaam, Maulana Sheikh Hemedi Jalala alianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kutupa neema ya uhai na afya ya kuweza kuifikia ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani na kuikamilisha ibada ya Funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa siku ya leo, kwani kuna watu wengi waliotamani kuimaliza funga hii lakini kwa uwezo wa Mungu hawakuafikiwa, wapo ambao hawakumaliza kwa sababu ya maradhi au kwa kutangulia mbele ya hakki. wala hapana hila wala nguvu ispokua kwa kuwezeshwa na mwenyezi mungu mtukufu.
Akizungumzia hatua za kuifikia amani, maulana alianza kwa aya katika Surat anfal :17“kama wasio waislaam watakua wanapenda amani nawe (Muhammad s.a.w.w)usiipinge amani hiyo, elekea katika amani hiyo na mtegemee mwenyezi mungu kwani yeye ndie mwenye kusikia na mjuzi “. maulana alisema mara nyingi tuna hubiri amani kuwa ni tunu na kitu cha kuenziwa, lakini kuna watu wana ufahamu mbaya kwa kudhani kua wanoihubiri amani huenda ni vibaraka au wana tumiwa, hawajui kua amani ndio asili ya dini.”asili ya dini ni amani,maamkizi ya dini amani, anae ihubiri amani ndio anaeihubiri dini si kibaraka.
Akiinukuu hadithi ya mtume Muhammad (s.a.w.w)alisema:”mbora wenu ni Yule anaewalisha watu chakula, aneieneza amani, na anaeswali usiku watu wakiwa wamelala.” Nae imam jaafar swadiq(as) mjukuu wa mtume (s.a.w.w) amesema :muislaam ni Yule watu wamesalimika nae kutokana na mikono yake na ulimi wake” hana tabia ya kuwatukana watu, hana tabia ya kuwagawa watu kwa ulimi wake hana tabia ya kusababisha fitna kwa watu wala hana tabia ya kuwahusudu watu “ ukimpata mtu ana shughulika na hayo ujue si mwislaam, mumtafutie dini nyingine,mwislaam ni Yule watu wamesalimika na mikono yake, hawapigi, hawaibii,haui watu,tukimpata mtu mkono wake haupo salama, huyo bado hajaujua uislaam.mtu anawataka watu kwenda kupigani dini, hivi unajua sharti za jihadi wewe? Alihoji maulana.
Alisisistiza maulana kua uislaam sidini ya kutisha watu, kuwafanyia watu ukatili,uislaam unavutia, muislaam ana haiba muislaam muda wote amebeba amani,Muslaam ni Yule ukimuona hata usiku wa manane unahisi upo katika amani. Akinukuu riwaya ya imam Hasan (as) siku moja aliingia bedui mmoja katika mji wa madina akaanza kumtukana baba yake Amiir muunina Alii bin Abii Twalib (as) baada ya kumaliza imam Hassan (as)alimuuliza umemeliza? Nakuona ni mgeni hapa madina, karibu nyumbani, ukiwa na njaa tutakulisha, kama huna pakulala tutakupa malazi, baada ya kuka siku kadhaa Yule bedui akasema hakukua na nyumba niliyokua nikiichukia kama nyumba hii, lakini kuanzia sasa hakuna nyumba ninayoipenda kama nyumba hii.
DSC01373
Akielezealezea hatua za kuifikia amani, Maulana alisema “tukitaka Tanzania iendelee kua kisiwa cha amani, tukitaka Dunia iwe ya Amani, hatua ya kwanza ni kumuheshimu binaadam mwenzio .” kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe, kupeana adabu (ambazo mtume s.a.w.w amesisitiza kua ni darsa katika mwezi huu wa Ramadhani) mkishikamana itaondoka dharau na kuja amani, ukijihisi una kitabia cha ufirauni, kujiona wewe ni mkubwa, basi sifa ya amani inaondoka.
Hivyo basi mataifa yanayojiita makubwa ya ulimwengu wa kwanza, lazima waondoe dharau na kubri kwa watu wa ulimwengu wa tatu,inapasa wawaheshimu ili amani iweze kuendelea na kudumu duniani. Mwisho maulana aliwataka waislaam kutokubezana na kuitana kwa majina yasiyofaa, kwani kufanya hivyo ni kuingiza mizozo na mifarakano, na matokeo yake ni kukosekana kwa amani katika jamii na kwa Taifa kwa ujumla.DSC01375

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on July 17, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: