SHEIKH JALALA: WAISLAMU TUUNGANE KUPIGA VITA MAKUNDI YENYE TABIA YA KUKUFURISHA WENZAO.

Akihutubia mamia wa waislamu waliokusanyika katika viwanja vya Peoples Kigogo polisi post baada ya swala ya iddi Jana, Mawlana Sheikh Hemedi Jalala aliwatahadharisha juu ya hatari ya Tabia iliyozuka ya baadhi ya watu au Vikundi viinavyozuka na Tabia ovu ya kukufurisha waislamu wenzao na akasema kuwa “Kitendo cha mtu kumuita mtu mwingine kafiri ajue kwa tamko hilo atakuwa amemtoa Muislamu katika dini bali pia amehalalisha damu yake kumwagwa na Mali yake kutaifishwa”, na akawataka waislamu kuitizama hatari hii kwa jicho la tahadhari sana.

image

Akifafanua hatari ya kitendo cha mtu kumuita mwenzake kafiri alisema “kumuita mtu kafiri kwa lugha nyingine umemthibitishia mtu huyo kuwa atadumu katika Moto wa Jahannamu milele.
Katika sehemu nyingine ya hutuba yake Mawlana Sheikh Jalala aliwataka waislamu na hususan wafuasi wa Nyumba tukufu ya Mtume (saw) kuyachukua kwa mikono miwili na kuyatumia mafunzo waliyoyapata kwa kozi ya Siku Thelathini za Mfungo wa Ramadhani na mafunzo hayo yawe dawa ya kukomesha tabia hii ovu ya kukufurishana baina ya waislamu au hata watu wenye vitabu kama vile wakristo na Mayahudi.

image

Akisisitiza juu ya Ubaya wa Tabia ya kukufurishana na kuitana majina Mabaya alisema “Tufahamu kuwa jamii yoyote yenye tabia ya kupeana majina mabaya kwa kuitana Makafiri, Wanafiki, Waovu, Watu wa Motoni, Makhurafi, na Majina mengine tunayoyasikia kila uchao, jamii hiyo ni jamii isiyoheshimu na kuenzi haki za Binaadamu wengine. Kwani kwa kitendo hicho wanawanyang’anya wanaadamu wenzao haki ya kuishi, Haki ya Usalama, haki ya Kuheshimiwa na haki ya kumiliki Mali hii ni misingi muhimu kuliko yote katika haki za binaadamu duniani.
Kwani kitendo cha kumuita Mtu kafiri ni sawa na kuitangaza jamii kuwa wale wenye uwezo wa kubeba Silaha na wabebe, wale wa Mapanga na wayanyanyue na hata kujifunga mabumu basi wafanye hivyo na kujitoa muhanga kuangamiza nafsi za wale wanaoitwa Makafiri kwani kwa kuwaita Makafiri Damu yao ni halali kumwagwa, na hata Mali zao ni halali kuporwa bila idhini yao, Je kuna unyama na ukatili kushinda huu akawataka waislamu kuungana kuupiga vita tabia hii.
Akielezea madhara yanayopatikana kijamii kwa kuitana majina Mabaya na Maovu alisema “Tabia ya watu kukufurishana au kuitana majina mabaya huzua mpasuko katika yao na jamii hiyo huanza kugawanyika katika Matabaka na makundi tofauti tofauti, kundi moja likiwatuhumu wenzao kuwa hawa ni makafiri, Wanafiki au kuwaita hata Makafiri au watu watu wa motoni. Akauliza kwa mshangao Vipi basi utaweza kuwaweka katika meza moja makundi hayo yenye kuhasimiana kiasi hichi? vipi watakaa meza moja kafiri na mwenye dini? Akatanabaisha kuwa jamii isiyokaa meza moja na kujadili changamoto zinazowakabili jamii hiyo ni jamii Mfu.

image

Akawaasa waislamu kuwa Uislamu Tanzania unakabiliwa na changamoto lukuki, Haiwezekani kukaa meza moja ikiwa baina yenu hakuna Mapenzi na Kuheshimiana, kamwe hamuezi kufikia Maendeleo yenu ikiwa wasomi na Wataalamu wenu wamekalia kugaiana pepo na Moto, huyu wa pepo huyiu kafiri wa Motoni, hawakai pamoja meza moja kuratibu maendeleo yenu katika Nyanja za Elimu, Tiba, Uchumi, na Ustawi wa jamii. Changamoto hizi zote zinahitajia waislamu bali watanzania kwa ujumla wao kukaa pamoja wakiheshimiana na kutafuta njia muafaka ya kukabiliana nazo.
Akiwakumbusha Waumini historia ya kudai Uhuru wa Tanganyika alisema kuwa historia ya kale ya Watanganyika imedhihirisha Babu zetu walikuwa ni jamii iliyolelewa kukaa pamoja, Watanzania hawajui kukufurishana, hata zama za kudai na kutafuta uhuru wa nchi yetu Mapenzi na kuheshimiana baina ya watanganyika ilikuwa ndio silaha pekee waliyompiga nayo Adui mkoloni, huku akiwauliza kwa mshangao alisema, “ni nani asiyemjua Sheikh Taqadiri, Sheikh Ramia, Bibi Titi Mohammed, Tewa Said Tewa, Abduliwahid Sykes, Chief Abdallah Said Fundikira, Mufti Sheikh Hassan Bin Ameir, hawa walikuwa Waislamu tena wenye msimamo na dini yao lakini ni hawa hawa waliotoka mstari wa mbele na Mwalimu Julius Nyerere Mkiristo tena Mkatoliki, hawakumbagua kwa dini yake wala kumuita majina mabaya na kwa pamoja wakatuletea uhuru ambao mpaka leo tunajivunia na kutoka kifua mbele. Akawataka waislamu kujua kuwa Wazee wetu hawa waliasisi sunna (Tabia) hii nzuri ambayo leo imetuletea Amani ya kweli Uhuru, Kuheshimiana, Ushirikiano na Busara baina ya Watanzania bila kujali dini zao. Lazima Sunna hii ienziwe iendelezwe na ilindwe. Fikra za kukufurishana, fikra zinazozuka za kupeana majina mabaya na Maovu baina ya Waislamu na Watanzania kwa ujumla tutambue kuwa fikra hizo hazina nia njema kwa waislamu bali hata kwa taifa letu kwa ujumla, fikra hizo ni adui wa Maendeleo yetu kama taifa ni mpango kabambe uliosukwa kuwafanya waislamu kushindwa kupanga mikakati ya Maendeleo yao kwani hakuna kazi inayoweza kufanywa  ndani ya jamii ikiwa jamii hiyo imegawanyika, hata wahenga walisema “Umoja ni nguvu utengano ni Udhaifu. Akinukuu Aya ya Mwenyezi Mungu juu ya umuhimu wa kufanya kazi na kuachana na Majungu na vitendo vya kuitana majina mabaya alisoma: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda (9:105)
Akihitimisha sehemu ya Khutba yake ya Iddi al-Fitra Mawlana Sheikh Hemedi Jalala aliwasema “Sisi kama waislamu lazima tuunganishe nguvu zetu pamoja kupigana vita na mtu yeyote au kikundi chochote chenye malengo ya kuigawa jamii ya Waislamu, kwani mtu au kikundi hicho hakiwatakii mema waislamu bali hata wakristo na Taifa letu kwa ujumla.

image

Tushikamane pamoja katika kamba wala tusifarikiana. Swala ya Iddi iliswali jana katika viwanja vya Peoples Vilivyopo eneo la Kigogo Dar es salaam,  ikiwa ni ibada ya kuhitimisha mfungo wa Ramadhani ambapo waislamu walikuwa katika Ibada ya Funga kwa muda wa Siku thelathini.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on July 19, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: