HATARI YA KUKUFURISHANA

DSC01163

Imam wa Masjid Ghadiir-Maulana Sheikh Hemed                                      Jalala

HATARI YA KUKUFURISHANA

Akihutubia waumini katika swala ya ijumaa leo masjid Ghadiir-Kigogo Post –ar es salaam, Maulana Sheikh Hemedi Jalala alisema ,kitendo cha kumwita mwenzako kua ni kafiri ni kusema kua damu Yake ni halali kumwagwa,na mali yake ni halali, nahii ni hatari jamii kuitana majina mabaya, majina ambayo yatasababisha damu ya mwenzio kumwagwa, na kumuhukumu kuingia motoni. Maulana alihoji: hiki kibali cha kuwaingiza watu motoni wamekitoa wapi? Ni mwenendo wa mtume kweli hata wale wasio waislaam kuwaita makafiri? Laa hapana bali mtume (s.a.w.w) alikua akiwaita kwa majina mazuri, ndio maana hata katika mjadala na wakristo wa Najran, mungu aliwaita ya Ahlal kitab, iweje mwislaam mwenzio umuite kafiri?
DSC02030Maulana aliwaasa waumini kua kuitana majina mabaya ni kuigawa jamii, naa akasema hakuna sababu ya kuitana majina mabaya wakati waislaam wote wanasema Laailaha Illa Allah, Muhammada Rasuulu llah,”kitendo cha mtu kumkiri mungu na mtume wake ni Heshima kubwa anapasa apewe, ni kigezo gani cha kumtoa katika dini wakati mtume (s.a.w.w.) amesema anaesema Laa illaha Illa Llah ameingia peponi damu yake imehifadhiwa, hivi hawa hawasomi riwaya katika bukhari na muslim?”
Akilifafanua zaidi hilo, maulana aliwakumbusha waislaam ,tukio lililo mtokea Sahaba wa Mtume (s.a.w.w) Bw Usama bin Zaid, alipo kua katika vita akapambana na mushrikina, mushrik akaomba amani, usama akamuua, mtume(s.a.w.w) akamuhoji Usama vipi unamuua mtu alie sema laailaha illa llah,? Utajitetea vipi na laa ilaha llla llah, siku ya qiyamat?uliingia katika moyo wake kua alikua hasemi kweli?
Maulana aliwataka waislaam na watanzania kwa ujumla,kuyaona yale yanayotendeka katika nchi za kiislaam, na Afrika, kua mtu anaejita muislaam, mwenye jina zuri la kiislaam kuingia katika msikiti na kujiripua na kuwaua waislaam, au kukamatwa mateka kwa wanawake na kuuzwa sokoni, kua huo si uislaam na wala uislaam hauelekezi hayo, “ni uislaam upi unaoruhusu wanawake kuuzwa? Tunasoma katika vita ya jamali, uhudi, hivi ni vita gani wanawake waliuzwa? Uislaam gani wanaouonyesha hawa? alihoji maulana.
Mwisho Maulana aliwausia waumini kuuusoma uislaam halisi wa mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuuhubiri kwa watu, na kuachana na huu uislaam wa chinja chinja na wa kuleta farka kwa watu na jamii,pia aliwataka katika kipindi hiki cha uandikishaji wa daftari la kupigia kura, waumini wajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuja kuitumia hakki yao ya msingi ya kumchagu mtu wamtakae” Kipindi hiki kinahitajia lugha za busara,na maelewano,ni wajibu wa waislaam kisheria kujiandikisha na kupiga kura, “ni sauti yako ya kuwachagua watu watakao leta maelewanao. MUNGU IJAALIE TANZANIA IBAKIE NI KISIWE CHA AMANI”.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on July 24, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: