KHUTBA YA SALA YA IJUMAA 7/8/2015

Samahat Sheikh Hemed Jalala khatib wa sala ya ijumaa MASJID ALGHADEER na kiongozi mkuu wa chuo cha dini cha Imam Swadiq katika Khutba ya sala ya ijumaa August 7, 2015 katika kuzungumzia HATARI YA WATU KUKUFURISHANA Alisema yafuatayo:
Uchaguzi wa mada hii ambayo ni muendelezo wa mada tuliyoianza siku za nyuma ni kwa sababu ya mazingizra halisi tunayoishi, ninaamini ya kuwa dunia inahitaji mazungumzo kama haya yanayowatahadharisha watu juu ya hatari kubwa za watu kukufurishana. Kitendo cha kumkufurisha mtu ni kumtoa katika dini yake, kumnyang’anya mtu haki ya ubinadamu na kumuweka katika hatari ya kuuawa, kunyongwa na kusambaratishwa.
Kutokana na uislam kutambua hatari kubwa ya watu kukufurrishana uliweka nembo ya kuwakusanya watu katika mwamvuli mmoja ambao LAAILAHA ILLALAH.
Katika historia watu waliwahi kukufurishana, mahala pa msingi pa kuangalia (kulingana na mazingira yetu) ni kuwa HAWA WANAOKUFURISHA WATU WANATOKA WAPI NA NI NANI ANAWATENGENEZA.
Allah katika Quraan anasema “Amewaahidi mwenyezimungu wale ambao wameamini katika ninyi na wakatenda mambo mema atawaweka wasimamizi wake katika ardhi kama alivyoweka wasimamizi wale waliokua kabla yao na atawamakinishia dini yao amabayo amewaridhia na atawabadilishia wao badala ya khofu na wasiwasi Amani wananiabudu mimi na wala hawanishirikishi, na wenye kukufuru baada ya hilo basi wao ni mafasiq” Surat Noor 55
Sasa ikiwa sisi ni makhalifa wa Allah katika ardhi vinapatikana wapi vikundi vya kukufurishana ambavyo vimeibuka na maradhi sugu ya KUGAWA PEPO NA MOTO,” Jambo la kushangaza ni kuwa sikuizi hata daraja za pepo huwa zinagawiwa hapa duniani na mtu anapewe Firdausi na mwingine anapewa Jahannam.
Akizungumzia athari za watu kukufurishana Maulana alisema Katika athari za KUKUFURISHANA ni kugawanya watu na kuwasambaratisha kiasi watu hawawezi kukaa pamoja na pia inabomoa misingi ya adabu, ndipo utawapata watu wanadiriki kusema katika mijadala yao kuwa HATA AKINA IMAM SHAFII NA MAALIK HAWAKUFANYA KITU BALI WALIGAWANYA WAISLAMU NA KILA KITU KILIKUA NI KWA RAI ZAO.
NDUGU ZANGU HII MIZANI YA KUWA WEWE NDIE WA KWENDA PEPONI UMEITOA WAPI?
Maulana sheikh hemed Jalala aliwaasa watu akisema:
“Ndugu zangu masheikh, maulamaa na wasomi mbalimbali kuweni makini na vikundi hivi vinavyofanya kazi ya kukufurisha watu kwani ni vikundi vya shetani, Kukufurishana ni fitna kubwa iliyoikumba umma wa kiislamu na inawagawanya waislamu na ule mwili mmoja wa uislamu unagawanywa kwa sababu ya kukufurishana, hivyo fitna ya kukufurishana ni fitna hatari sana”
Moja ya madhara ya kukufurishana yaliyoikumba jamii ya waislamu ni kung’ang’ania hata itikadi mbovu (na kutosoma upande mwingine) kwa sababu tumeshaitana makafiri na hatuwezi kukaa meza moja, hivi ni sawa kweli mpaka sasa kukapatikana mtu anaamini kuwa mungu ana uso na mikono na eti anakaa huko juu? Kwanini watu hawamuulizi imam Ali a.s huyu mungu yuko wapi?…

Maulana Sheikh Hemed Jalala akanukuu maneno ya imam Ali a.s kutoka katika Nahjulbagha khutba ya kwanza inayomzungumzia Allah, imam anasema:
“…na atakaesema yuko juu basi maana yake chini hayupo,( na akiwa chini basi juu hayupo), atakaesema yuko ndani ya ..basi atakua amemdhibiti nje ya kitu hayupo” Allah haihitaji mahali ili awepo kwa kuwa yeye ndie amepaumba mahali alikuwepo kabla yake,
Sheikh Hemed Jalala akaendelea kusema kwa kuuliza akitumia mfano wa swali lilitumiwa na DR. Tijani Samawi alipomuuliza mtu kuhusu aya za Quraan kukosa taawili na kuwa kila mahala palipozungumzwa mkono na uso panatafsiriwa kama ilivyo, sheikh kwa msisitizo akauliza huku akiisoma aya ya Quraani inayelezea ya kuwa kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa uso wake ( Allah), JE HII INAMAANISHA KUWA MIKONO YA ALAAH NA MIGUU PIA ITAANGAMIA NA UTABAKI USO?
Maulana Sheikh akaendelea kusema “hizi itikadi zisizokuwa za sawa haziwezi kubadilishwa kwa kuwa moja ya athari ya watu kukufurishana ni kukosa adabu na kutokukaa meza moja”
Sheikh aliongeza na kusema:
“vita baina ya waislamu na mauaji ya kikatili katika jamii ya kiislamu ni ya kutisha , yote haya yanatokana na fitna za watu kukufurishana, hili linawafanya waislamu wawe dhaifu wasioweza kumiliki hata Nursery nzuri kwa ajili ya watoto wao, na kila ishara za umaskini zinadhihirika kwa waislamu , hii leo ukienda makanisani ukaangalia magari yaliyoegeshwa utayapata ni mengi na yenye thamani lakini misikiti utapata pikipiki na baiskeli”.
Hivi ndugu zangu mnadhani hizi nguvu za waislamu duniani mashie, masuni na Ibadhi zikiunganishwa uislamu utakua wapi? Hakika uislamu ndio utakua SUPER POWER, Akili za watu kama Imam Khomein na Sayed Ali Khamenei zikiwekwa meza moja na maulamaa wa Misri na Khalij unadhani nini kitazalika?
Maulana Sheikh Hemed Jalala alimaliza kwa kutoa pongezi kwa kongamano kubwa liliofanyika huko senegali ambalo malengo yake ni kuzungumzia ugaidi na amani, ambapo Raisi wan chi hiyo alishiriki na kutoa nasaha za watu kushikamana na kuheshimiana.
Pia Sheikh alisema TUNAUNGANA NA WATU WOTE DUNIANI KUPINGA NA KULAANI TUKIO LA KUCHOMWA MOTO KWA MTOTO MCHANGA HUKO PALESTINE, KULIKO SABABISHWA NA MAZAYUNI, yote haya yanatuonyesha kuwa kadhia ya Palestine ikinyamaziwa basi Amani itazidi kuvurugika duniani.
Mwisho kabisa Sheikh alimaliza na kutoa nasaha juu ya swala zima ya uchaguzi mkuu wa nchi na kuwaasa watu wasiwe wavunjifu wa Amani na kuwa wachague watu makini wanaweza kutatua kero za wananchi.
Imetolea na kitengo cha Habari Hawzatul Imam Swadiq (a.s)

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 7, 2015, in Hotuba na Mawaidha. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: