Sheikh Mkuu wa al Azhar: kuwakufurisha Waislamu wa madhehebu ya Shia ni kitendo kisichokubalika

9f9567fb07d84b9c21d3bf3f408fea03_XL

Sheikh Mkuu wa al Azhar nchini Misri amesema, kuwakufurisha Waislamu wa madhehebu ya Shia kunakofanyika kupitia kanali za televisheni za satalaiti ni kitendo kisichokubalika na jambo hilo haliwezi kuhalalishwa au kutetewa kwa kutumia kitabu kitakatifu cha Qur’ani, Suna na mafundisho ya dini.

Sheikh Ahmad al Tayyib amesema Waislamu wa madhehebu ya Suni wanaswali nyuma ya maimamu wa madhehebu ya Shia na kuongeza kuwa: Baina ya Shia na Suni hakuna hitilafu kubwa zinazoufanya upande mmoja uukufurishe na kuutoa katika dini upande mwingine na kwamba kinachoshuhidiwa kwa sasa na kutumiwa vibaya na kwa malengo ya kisiasa baadhi ya hitilafu za kimitazamo. Sheikh al Tayyib amesema wadhifa mkuu wa al Azhar ya Misri ni kufanya jitihada za kuunganisha Umma wa Kiislamu licha ya hitilafu za kimitazamo zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu. Sheikh Mkuu wa al Azhar amesema yuko tayari kusafiri na kwenda eneo lolote lile duniani kwa ajili ya kuimarisha umoja wa Waislamu.

Kwa kutilia maanani hali ya sasa ya nchi za Waislamu, inaonekana kuwa umoja wa Waislamu ndiyo wenzo muhimu zaidi ya kuwawezesha kuvuka salama fitina na njama za ubeberu na maadui wa dini hiyo ya Mwenyezi Mungu. Wakitumia mbinu mbalimbali, maadui hao wa Uislamu wamelifanya suala la kuanzisha vita na mapigano kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni kuwa ndiyo ajenda yao kuu kama njia ya kugawa na kuzusha hitilafu katika Umma. Nyenzo zinazotumiwa na maadui hao kwa ajili ya kupenya baina ya Waislamu ni kutumia wasaliti waliopotoka kutoka madhehebu mbalimbali za Waislamu na kisha kuhubiri tafsiri zisizo sahihi za kisiasa.

Kufasiri na kuhubiri Uislamu wa Kimarekani ni njama ambayo lengo lake ni kuzusha mpasuko na hitilafu katika safu za Waislamu na kuzuia ulimwengu wa Kiislamu kuwa nguvu kubwa katika siasa za kimataifa. Maadui wa Umma wa Kiislamu wanadhamini maslahi yao haramu kwa kuzusha na kukuza hitilafu ndogondogo baina ya Shia na Suni. Kwa njia hiyo maadui wa Umma wanawashughulisha Waislamu na masuala yasiyokuwa na umuhimu na kuwaghafilisha na mauala ya asili ya muhimu sana hususan kadhia ya Quds tukufu. Maadui hao wanaupambanisha Uislamu halisi na sahihi unaosisitiza umoja na mshikamano na ule wa fikra mgando unaowakilisha ujahili na ukatili. Mfano wa uislamu mgando ni ule wa makundi ya kigaidi ya Daesh, al Qaida na Boko Haram ambayo yote yanaungwa mkono kwa njia moja au nyingine na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kama anavyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, katika maktaba na mfumo wa kifikra wa Imam Khomeini, Uislamu wa mashekhe vibaraka wa watawala, Uislamu wa Daesh, Uislamu usijali na unaokaa kimya mbele ya jinai zinazofanywa na Marekani na Israel na kunyoosha mkono wa udugu na urafiki kwa madola ya kibeberu unatokana na chanzo kimoja na hauwezi kukubalika.

Kwa msingi huo Waislamu wanapaswa kuwa macho na wasiruhusu maadui kutumia vibaya hitilafu zao za kimaoni na kimitazamo.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 7, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: