WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA JAMII

DSC02408

Maulana, Sheikh Hemed Jalala, Mkuu wa Harakati ya Kislaam, na mkuu wa chuo cha Hawzat Imam Swadiq- kigogo Post-Dar es saalaam.

WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA JAMII
“ENYI WATU HAKIKA TUMEKUUMBENI KUTOKANA NA MWANAMUME MMOJA NA MWANAMKE MMOJA NA TUKAWAFANYA NI MATAIFA NA MAKABILA TOFAUTI ILI MJUANE, HAKAIAKAK MBORA WENU NI MCHAJI MUNGU” SURAT HUJURAT: 49:13
Akizungumzi Katika semina ya Wajibu wa vyombo vya Habari katika kuielimisha jamii,iliyofanyika leo jumapili ya Tarehe 9/8/2015,Mkuu wa chuo na Imam wa msikiti wa Ghadiir uliopo Kigogo Post-Dar es salaam, Maulana Sheikh Hemed Jalala aliwataka wanasemina kwanza kufahamu vyanzo na viashiria vya uvunjifu wa amani katika jamii, kisha ndio ufuatie wajibu wao. alisema ni lazima watu kwanza waufahamu uislaam,Uislaam uliofunzwa na mtume (s.a.w.w) na uliozungumwa na maimam wa nyumba ya mtume(s.a.w.w) haukufundisha uvunjifu wa amani,muislam wa kisawasawa niyule anae eneza amani, maelewano,mshikamano katika jamii, amesema mtume (s.a.w.w.)” muislam ni Yule mungu anampenda anaeeneza amani, “muislaam wa kweli ni Yule waliosalimika watu kutokana na ulimi wake na mikono yake.”
Mafunzo aliyofundisha mtume (s.a.w.w) ni watu kukaa pamoja, kukubali rai ya mwenzako, kama a livyoishi mtume (s.a.w.w)na mushrikna wa makka, na kujenga mahusiano nao, hata kuweka amana zao kwake na kumwita mkweli na muaminifu. Na hata mtume alipo kua madina alikaa kwa amani na wakristo na mayuhudi na kuwekeana nao makubaliano ya amani.Akitokea mtu katika jamii kumkataa mwenzake kwa kua si katika dini yake , huyo amekuja na dini mpya.
Akielezea falsafa ya jihadi katika uislaam, Maulana alisema Falasafa ya jihadi ni kuwalinda na kuwatunza wasio waislaam,sio kuwashambulia, aliwataka watu kusoma historia ya mtume alipokua makka, kua mtume (s.a.w.w) hakupigana na mushrikina mpaka walipomzuia kutangaza neno la mwenyezi mungu, ndipo mungu akampa ruhusa ya kujitetea, “na katika sheria za vita jihadi, mwana mke , mtoto, mtu wa dini ,askofu au Padre, hawapigwi, na miti pia haikatwi, kuonyesha uhifadhi war oho za watu na mazingira.”
Maulana aliwastaajabu hawa wanaotangaza jihadi leo, mbona hawafuati maelekezo haya ya mtume (s.a.w.w.)? kwa kuwateka wanawake, kuwauza, na kuwadhalilisha, kubomomoa vituo na athari za kiibada za dini nyingine, ni mafundisha ya dini gani wanayoyafuata? Alihoji maulana.DSC02376
Maulana pia, alataja viashiria vya uvunjifu wa amani, amabapo alitaja kiashiria cha kwanza ni tafsiri mbaya ya vitabu vitakatifu.” Jamii yetu imekumbwa natabia ya kukufurishana , jamii ikiachwa na tabia hii, jamii itasamabaratika.
Ukimwambia mwenzio ni kafiri, maana yake umemtoa katika dini,umemuondolea hakki ya kuishi, mali yake na nafsi yake ni umeifanya halali. ,”leo katika familia zetu tunaishi ndani ya familia, kuna waislaam, nawakristo, jamii imechanaganyikana sana, leo kuja kuwabagua wenzako kwa udini na kuwagawa kwa misikngi ya ukafiri, jambo hili ni la kukemewa sana,na kupingwa kwa njia zote.
Kiashiria kingine maulana alisema ni kutokuamainana, “jamii ya watu wasio aminiana haiwezi kukaa kwa amani.
Aliwataka viongozi wa dini kuwepo na juhudi ya dhati ya kuwa navikao vya viongozi wa dini mbalimbali, kukaa pamoja, kubadilishana mawazo,fikra,kitendo cha viongozi wa dini , masheikh, maaskofu, maimam Aliwataka viongozi wa dini kuwepo na juhudi ya dhati ya kuwa navikao vya viongozi wa dini mbalimbali, kukaa pamoja, kubadilishana mawazo,fikra,kitendo cha viongozi wa dini , masheikh, maaskofu, maimam mapadre kukaa pamoja kutaiathiri jamii, na kutawafanya waumini wetu kuiga mfumo huo wa kujenga umoja katika jamii.

DSC02391

baadhi ya wanahabari walioshiriki katika semina hiyo ya leo

DSC02408

Mkuu wa chuo Harakati ya Kislaam na mkuu wa chuo cha kidini cha Hawzat Imam swadiq- Kigogo Post-Dar es salaam, akiongea na waandishi wa habari- leo.

Kiashiria kingine Maulana alisema, ni mauaji ya ndugu zetu Albino, kunawafanya wenzetu, watanzania wenzetu waishi bila ya amani katika nchi yao,alitaka vitendo hivyo kupingwa kwanguvu zote, na waandishi wa habari kuyaripo matukio hayo na kuyafuatilia ili jamii hiyo iweze kua salama, kwani nao wana hakii ya kuishi kama binaadamu wengine. Ni wajibu wa vyombo vya habari kuihabarisha na kuielimisha jamii, wala si kupendelea upande mmoja.
Mwisho maulana aliwataka wanahabari, na waandishi kwa ujumla,kuifunza jamii ya kitanzania juu ya swala zima ya uchaguzi mkuu wa nchi na aliwaasa watu wasiwe wavunjifu wa amani, na kuwataka waandishi wasiwe ni sababu ya uvunjifu wa amani kwa kupendelea upande mmoja, watoe habari zakweli zisizo na viashiria vya uvunjifu wa Amani, kubwa ni kuwaelimisha Wanzania waje kuchagua watu makini wanaoweza kutatua kero za wananchi.
Naye Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Bw Charles Kayoka, akizungumzia dhima ya waandishi wa habari, alisema: miongoni mwa dhimma kubwa ya waandishi wa habari ni: taarifa wanazotoa ziwe za kweli, kufanya uchunguzi juu ya habari kujenga jamii, kuanzisha agenda maalum kwa ajili ya kujenga maslahi ya Taifa, kupanua fikra, mawazo zaidi ya mahala tulipo, kufikiri nje ya boksi,kuiunganisha jamii, kuonyesha sauti zote za watu zinasikika, kuwajengea watu uwezo wa kuchuja pumba na mchele, na kuwa na uwezo wa kuuliza maswali.
,Bw Charles Kayoka alizungumzia changamoto zina zowakabili waandishi kua: elimu ndogo, mazingira ya kiuchumi,mgongano wa kimaslahi, na mashinikizo kutoka kwa wamiliki na maafisa.aliwataka waandishi na wanahabari kuzishinda changamoto hizo ili kuielimisha jamii mamabo yatakayowaletea tija katika Taifa.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 9, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: