Kiongozi Muadhamu Aonana na Wajumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul BaytAS na Muungano wa Redio na Televisheni za Kiislamu

17/08/2015
 Supreme Leader's Speech to Members of Ahlul Bayt World Assembly and Islamic Radio and Television UniAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Asubuhi ya leo (Jumatatu) ameonana na maulama, wananadharia na wageni wa mkutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt AS na mkutano wa Jumuiya ya Redio na Televisheni za Kiislamu na kusema kuwa, mapambano dhidi ya mipango ya Uistikbari katika eneo (Mashariki ya Kati) ni misdaqi dhahiri (ya wazi) ya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mapambano ya dhati (ya nguvu zote) dhidi ya (njama za Marekani za kutumia vibaya natija ya mazungumzo ya nyuklia na satwa ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni nchini Iran) na kuongeza kuwa, mikakati na mipango ya mfumo wa kibeberu katika Mashariki ya Kati zimesimama juu ya misingi miwili ya kuleta hitilafu na kuwa na satwa (upenyaji) ambapo tunapasa kutumia mbinu sahihi za kushambulia na za kiulinzi ili kupambana kwa muono na welewa na bila kusita na mbinu hizo (za maadui).
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria kufanyika kwa kikao cha sita cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (as) na kusema kuwa, kuwafuata Ahlul Bayt wa Mtume (saw) kunalazimiana na kuenezwa maarifa ya Kiislamu, kusimamishwa sheria za Mwenyezi Mungu, kufanya jihadi (jitihada) katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nguvu zetu zote na kupambana na dhulma na dhalimu na akasisitiza kwamba, kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu hakuna maana ya vita vya kijeshi tu, bali kunajumuisha pia mapambano ya kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, leo misdaqi na kielelezo bora zaidi cha jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kutambua vyema mbinu (njama) za Uistikbari katika eneo la Kiislamu na hasa katika eneo la kiistratijia na nyeti la magharibi mwa Asia na kuweka mikakati ya kupambana nazo ambapo mapambano hayo yanapaswa kujumuisha makabiliano ya kiulinzi na kihujuma. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria njama za Uistikbari katika eneo katika kipindi cha miaka mia moja iliyopita na kusema kuwa, hata kama njama za Uistibari katika eneo la Kiislamu zina historia kongwe, lakini mashinikizo na njama ziliongezeka tokea wakati wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ili kuzuia kukaririwa kwa uzoefu huo (Mapinduzi ya Kiislamu) katika nchi nyingine. Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu tokea miaka 35 iliyopita umekuwa mlengwa wa vitisho, vikwazo, mashinikizo ya kiusalama na njama mbalimbali za kisiasa, na taifa la Iran limeyazoea mashinikizo haya.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, tab’ani njama za maadui katika eneo la magharibi mwa Asia zimeongezeka zaidi kutokana na kuchanganyikiwa adui kufuatia Harakati ya Mwamko wa Kiislamu ambao ulianza miaka kadhaa iliyopita kaskazini mwa Afrika. Ayatullah Udhma Khamenei amebainisha kuwa, wanadhani (maadui) kuwa wameweza kukandamiza Mwamko wa Kiislamu lakini harakati hii haiwezi kukandamizwa na bado inaendelea na hivi karibuni au muda usio mrefu ukweli wake utadhihiri. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba, mfumo wa ubeberu ukiongozwa na Marekani ni mfano wa wazi na dhihirisho kamili la fasili ya “uadui” na kusisitiza kuwa, Marekani haijastafidi kabisa na maadili ya kiutu (ubinaadamu) na hutekeleza ukatili na jinai bila kujali lolote na kwa kutumia maneno matamu (ya kuvutia) na kwa uso wa bashasha na tabasamu.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mbinu zinazotumiwa na adui katika mazingira ya hivi sasa na kuongeza kuwa, mbinu hizi zimesimama juu ya misingi miwili ya ‘kuzua hitilafu’ na ‘kujipenyeza.’ Kuhusiana na mpango wa adui wa kuzusha hitilafu na mifarakano, Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, kuzusha hitilafu miongoni mwa serikali na hatari zaidi kuliko hilo, miongoni mwa mataifa, kumewekwa katika ajenda ya Uistikbari. Ameashiria kwamba katika hali ya hivi sasa ibara kama Shia na Suni zinatumika kwa ajili ya kuleta hitilafu miongoni mwa mataifa na kusema kwamba, Waingereza wamebobea katika kuzusha hitilafu nao Wamarekani ni wanafunzi wao na kuongeza kuwa, makundi ya kikatili, yanayovunjia heshima matukufu na ya kijabari ambayo Marekani imekiri kushiriki katika uundwaji wake ni chombo muhimu zaidi kinachotumiwa kuzusha hitilafu ambazo kidhahiri zinaonekana kuwa za kidini miongoni mwa mataifa, njama na mbinu ambazo kwa bahati mbaya mno baadhi ya Waislamu wenye fikra finyu wamehadaika nazo na kutumbukia kwenye mpango wa adui kutokana na kutokuwa kwao na welewa na muono. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mfano wa wazi kuhusiana na maudhui hiyo ni suala la Syria na kuongeza kwamba, wakati tawala za kitaghuti nchini Tunisia na Misri zilipoondolewa madarakani kwa shaari na nara za Kiislamu, Wamarekani na Wazayuni walichukua uamuzi wa kutumia mtindo huo kuzitokomeza nchi za mapambano za Kiislamu na ndio maana waliiendea Syria. Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, baada ya kuanza tukio la Syria, baadhi ya Waislamu wasio na mwamko walitumbukia kwenye njama ya mpango huo na kuanza kujaza jedwali la mafumbo la adui, na hivyo kuifikisha Syria katika hali hii. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, yale yanayojiri leo huko Iraq, Syria, Yemen na maeneo mengine na juhudi zinazofanyika ili kuyadhihirisha kuwa ni ‘vita vya kimadhehebu’ kwa vyovyote vile si vita vya kimadhehebu bali ni vita vya kisiasa. Ayatullah Udhma Khamenei amebainisha kuwa, jukumu muhimu zaidi hii leo ni kufanya juhudi za kuondoa hitilafu hizi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, sisi tumesema wazi na bila kificho kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inazinyooshea mkono wa urafiki serikali zote za Kiislamu za eneo na wala hatuna tatizo lolote na serikali za Kiislamu. Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina uhusiano wa kirafiki na nchi nyingi jirani, bila shaka baadhi ya nchi pia zina hitalifiana na sisi na zinafanya ukaidi na ukhabithi lakini Iran imesimamisha msingi wake juu ya uhusiano mzuri na ujirani mwema na serikali za Kiislamu na hasa mataifa ya eneo (Mashariki ya Kati). Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, msingi wa mwenendo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni misingi ambayo Imam Khomeini (Rahmatullah Alayh) alifungamana nayo na hivyo kufanikiwa kuyaletea ushindi Mapinduzi ya Kiislamu na kuyafikisha katika hatua ya uthabiti.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, ‘wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao’ ni moja ya misingi imara ya mfumo wa Kiislamu na kusisitiza kuwa, sisi kwa msingi wa darsa ya mpendwa Imam (MA) na sera ya wazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hatufanyi mapatano na Uistikbari lakini tuna urafiki na ndugu Waislamu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, sisi hatuzingatii madhehebu katika kutetea na kuunga mkono mtu anayedhulumiwa na uungaji mkono uleule tulioutoa kwa ndugu zetu Mashia nchini Lebanon ndio uleule tulioutoa kwa ndugu zetu Masuni katika Ukanda wa Gaza, na tunalichukulia suala la Palestina kuwa suala la ulimwengu wa Kiislamu.
Katika kutoa jumusho kuhusu suala la “kuzusha hitilafu” Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, suala hilo ndiyo nguzo ya kwanza ya njama za adui katika eneo la Kiislamu la magharibi mwa Asia na kuongeza kwamba, kushadidishwa hitilafu katika ulimwengu wa Kiislamu ni marufuku na sisi tunapinga kila aina ya mwenendo na harakati inayozusha hitilafu hata ikiwa itatoka kwa baadhi ya makundi ya Kishia, na tunalaani kuvunjiwa heshima matukufu ya Ahlu Suna.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema ‘upenyaji’ katika nchi za eneo ni mbinu ya pili ya kikorofi inayotumiwa na Marekani na kusisitiza kwamba, Marekani inataka kuhuisha satwa yake ya makumi ya miaka na heshima yake iliyopotea katika eneo la Mashariki ya Kati. Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameashiria njama zinazofanywa na Washington kwa ajili ya kutumia vibaya matokeo ya mazungumzo ya nyuklia na kuongeza kwamba, Wamarekani wanataka kutumia mapatano ambayo taklifu yake haijajulikana sio Iran tu bali hata Marekani kwenyewe na haijulikani iwapo yatapitishwa au la, kama chombo cha kujipenyeza nchini Iran, lakini sisi tumeifunga kabisa njia hii. Tutatumia nguvu zetu zote kutowaruhusu Wamarekani kuwa na ushawishi wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni au kuwepo kisiasa nchini Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, siasa za kieneo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinagongana moja kwa moja na siasa za kieneo za Marekani na kuongeza kwamba, wao wanataka kuzigawa nchi za eneo na kubuni nchi ndogondogo tegemezi lakini sisi kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu hatutaruhusu hilo kutimia. Kiongozi Muadhamu amekumbusha onyo na tahadhari alizotoa huko nyuma kuhusiana na juhudi zinazofanywa na Marekani kwa ajili ya kuigawa Iraq na kuongeza kuwa, baadhi walikuwa wakishangazwa na maneno hayo, lakini leo Wamarekani wanazungumzia waziwazi suala la kuigawa Iraq.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, kugawanywa Iraq na wakiweza Syria ni lengo lililo wazi la Wamarekani lakini umoja wa ardhi za nchi za eneo zikiwemo Iraq na Syria una umuhimu mkubwa kwetu sisi.
Katika kuendelea kufafanua mkabiliano uliopo kati ya siasa za kieneo za Jamhuri ya Kiislamu na siasa za utawala wa Marekani, Kiongozi Muadhamu ameongeza: Iran inatetea kikamilifu mapambano katika eneo yakiwemo mapambano ya Palestina na itaendelea kumuunga mkono kila mtu anayepambana na Israel na kuuponda utawala wa Kizayuni.
Amesema kuwa kukabiliana na siasa za kuzusha mifarakano za Marekani na vituo vya kuzusha hitilafu ni miongoni mwa siasa za kimsingi za Iran na kuongeza kuwa, Ushia ambako kituo chake cha matangazo kiko London na kazi yake ni kuutayarishia njia ubeberu, sisi hatuutambui kuwa ni Ushia.
Kiongozi wa Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbusha sera za Iran za kutetea watu wote wanaodhulumiwa wakiwemo wananchi wa Bahrain na Yemen na kuongeza kwamba, kinyume na madai yasiyo na msingi, Iran haiingilii masuala ya ndani ya nchi hizo, lakini itaendelea kuwatetea na kuwasaidia wananchi hao wanaodhulumiwa.
Kiongozi Muadhamu amekosoa vikali mauaji yanayoendelea kufanywa dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Yemen na kuharibiwa nchi hiyo na akasema kuwa, kufuatilia baadhi ya malengo ya kisiasa tena kwa kutumia mbinu za kipumbavu ndiyo sababu ya kuendelea kwa jinai zinazofanywa dhidi ya watu wa Yemen.
Ayatullah Udhma Khamenei amekamilisha sehemu hii ya hotuba yake kwa kusema kuwa, katika maeneo mengine ya ulimwengu wa Kiislamu ikiwemo Pakistan na Afghanistan kunajiri matukio ya kuumiza, na Waislamu wanapaswa kutibu matatizo hayo kwa umakini na uangalifu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, Muungano wa Redio na Televisheni za Kiislamu ni kituo chenye umuhimu mkubwa kwa ajili ya kukabiliana na mfumo hatari na umafia tata wa vyombo vya habari vya Kimarekani na Kizayuni. Ameongeza kuwa harakati hiyo inabidi iimarishwe na kupanuliwa zaidi.
Amekumbusha suala la masafa makubwa yaliyopo baina ya vyombo vya habari katika nchi nyingi za Kiislamu na matakwa ya wananchi Waislamu na vilevile suala la vyombo hivyo vya habari kufuata siasa hatari za ubeberu na kusema kuwa, mamlaka kubwa ya vyombo vya habari vya madhalimu ambavyo vinadai kutopendelea upande wowote inahudumia malengo ya madhalimu wa kimataifa kwa kupotosha mambo, kusema uongo na kwa kutumia mbinu tata za aina mbalimbali.
Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, licha ya majigambo ya ubeberu na vibaraka wao, hapana shaka kuwa izza na nguvu ya Uislamu iko wazi na imedhaminiwa kwa baraka za wanaume, vijana na wanawake wapigana jihadi, na mustakbali mwema utakuwa wa eneo la Mashariki ya Kati na mataifa ya Waislamu.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait Hujjatul Islamu Walmuslimin Muhammad Hassan Akhtari alitoa ripoti kuhusu mkutano wa sita wa jumuiya hiyo na kusema kwamba, mkutano huo umehudhuriwa na maulama na shakshia kutoka zaidi ya nchi 30 duniani.
Vilevile Katibu Mkuu wa Muungano wa Redio na Televisheni za Kiislamu, Hujatul Islam Karimiyan alitoa ripoti akisema kuwa, miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na muungano huo ni pamoja na kufanya jitihada za kuanzisha lugha mpya katika medani ya vyombo vya habari kwa kutumia vigezo vya Kiislamu, kuvutia imani ya watu, kulea nguvu kazi inayofaa na kuanzisha mbinu ya kuzalisha, kusambaza na kutangaza habari.

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 20, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: