HIJJA NI SULUHISHO LA MATATIZO YA WAISLAAM.

DSC04955

Sheikh Mkuu wa T.I.C, Sheikh Abdallah Seif, Akiwahutubia waumini katika swala ya Eidul Adh-haa

Akitoa khutba ya swala ya  eidul Adh-haa( idd ya kuchinja),  iliyoswaliwa leo alhamis Tarehe 24/9/2015 katika Viwanja vya Pipo- Kigogo , Dar es salaam, Sheikh Mkuu wa T.I.C, Sheikh Abdallah Seif, aliwakumbusha waumini, Tukio kubwa lililoifanya sikuuu  hii kuitwa sikukuu ya kuchinja , kua ni Nabii Ibraahim (as) alipotekeleza  agizo la Mwenyezi Mungu (S.W) la kumchinja mwanae Ismail (as), na alipopewa agizo hilo, hakusita wala kuogopa kutoitekeleza“hijja ni miongoni mwa ibada zilizofaradhishwa  kwa waislaam, ina masharti yake, miongoni mwa masharti hayo ni  uwezo wa pesa, wa kwenda na kurudi,uwezo wa Afya na nguvu za kuitekeleza  ibada hiyo, na usipoenda utakua umeivunja nguzo hiyo na utakua huna Taqwa, Taqwa ni kutekeleza yale aliyokuamrisha Mwenyezi Mungu na kuyaacha yale aliyokukataza, funzo  la kulichukua hapa ni: Tunapokua na jambo la wajibu  tusiwe na woga wa kutotekeleza.

DSC04967

waumini, wakiwa tayari kuitekeleza ibada ya Eidul Adh-haa, katika viwanja vya pipo-Kigogo Post-Dar es salaam.

Hijja kama ingetumika vizuri na waislaam, ingekua ni suluhisho la matatizo yanayotukabili, kusingekua na vita katika dunia na nchi za kiislaam, tunavyovishuhudia leo. wote pale Arafa tungelisimama na kuyatatua matatizo hayo, lakini insikititsha kuona nchi ambayo ni mwenyeji wa ibada ya hijja Saudi Arabia, kua nayo ipo katika vita kuwapiga waislaam wenzao wa Yemeni.

DSC04930

Sheikh Muhammad Abdi, akiwa na Waumini, katika viwanja vya pipo, kwa ajili ya swala ya Eid

“inasikitisha sana kuona baadhi ya waislaam, wanawaita waislaam wenzao kua si waislaam, ni makafiri, hivi hawaoni, juzi walikua pamoja pale katika kuizunguka alkaabat, jana walikua wote pale Arafa na kulala pamoja Muzdalifa, na leo mnatupa pamoja mawe, unamwambia mwenzio kafiri kwa kigezo gani?alihoji sheikh Abdallah Seif.

DSC04902Mwisho aliwaasa waumini, hasa vijana, kutotumika na makundi hayo yanayoeneza  chuki kwa waislaam wenzao kwa kuwaita makafiri,nakuwataka  wakumbuke  nchi ambazo makundi hayo yapo , hakuna amani, hakuna utulivu, kumejaa mayatima, wajane,” vita  haijengi, vita huleta  umasikini,  huzalisha wakimbizi, huwafanya watu wasikae vizuri”, akitolea mfano wa makundi hayo kua ni Boko haram, alshabab na mengineyo.aliwausia kuienzi Amani ya nchi na kuliombea Taifa letu liendelee kua la Amani kuelekea katika uchaguzi mkuu wa nchi.

MUNGU UTUONDOLEE BALAA HILI LA VITA, NASISI UTUWEZESHE KWENDA KUITEKELEZA IBADA HII YA HIJJA MWAKANI, NA WALIOPO HUKO UWAREJESHE MAJUMBANI MWAO KWA USALAMA NA AMANI, AMIIN”.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on September 24, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: