KHUTBA YA SALA YA IJUMAA 02/10/2015 Sehemu 01
Maulana Smahat Sheikh Hemed Jalala Khatib wa sala ya ijumaa, Mudeer na kiongozi wa Chuo cha theolojia ya dini ya kiislamu cha Imam Swadiq a.s kilicho na makao makuu yake jijini Dar es Salaam alianza kwa kutaja matukio mawili makubwa, tukio kubwa kabisa ni tukio la ghadeer na uteuzi wa kiongozi wa waumini Ali abi Talib, tukio la pili ambalo ndio msingi wa mazungumzo wa ijumaa hii ni tukio la Hija kwa kuwa limegubikwa na msiba mzito wa vifo vya mahujaji katika Ardhi ya Minna, jamarat na katika msikiti wa mtume.
Maulana Sheikh Hemed jalala alianza kwa kuzungumzia Hijja na utukufu wa ardhi ya makka na historia fupi juu upatikanaji wa Alkaaba na tukio la kuamrishwa Ibrahim kumchinja mwanae Ismail, Maulana Sheikh Hemed Jalala alielezea kuwa moja ya Majina ya makka na kusema “Wanahistoria wameandika majina mengi kuhusu makka na yote hii ni kuonyesha utukufu wa ardhi hiyo, moja ya majina yake ni “AL-ISLAH” ikimaanisha kutengeneza na kufanya vizuri, HIVYO M/MUNGU AMEWAWEKEA WAISLAMU MJI MAALUMU AMBAO NDIO MJI WA KUTENGENEZA MAMBO YAO, KWA MAANA NYINGINE NI KUWA WAISLA MU WAMEWEKEWA OFISI YA AMBAYO NI MAKKATAL MUKARRAMA, ambayo makka hiyo ikiwekewa msikiti ambao ndio nyumba ya kwanza ya Allah ya kwanza kujengwa duniani, Mji huu ni mako makuu ya waislamu, malengo makuu ya kuwekewa makao makuu waislamu ni kutengeneza mambo yao na ndipo mafundisho ya Mtume na maimamu yanasema “Uislamu utabaki maadamu Alkaaba itabakia” ikimaanisha ya kwamba UISLAMU UTABAKI IKIWA UTAKUA NA MAKAO MAKUU YA KUENDESHA MAMBO YAO”
Maulana Sheikh Hemed jalala aliendelea kusema kuwa Moja ya falsafa ya hija ni watu kuonana na kukutana katika makao yao makuu wakabadilishana mawazo, fikra na mitazamo. Waliokua na hali mbaya ya maisha katika nchi zao wakafaidika na wale waliokua na hali nzuri ya maisha wakiwa katika ofisi yao hiyo kama anavyofundisha Imam wetu wa nane Imam Ridhwa a.s ya kwamba Moja ya falsa ya mkusanyiko wa ibada ya hija ni kubadilishana manufaa yao ya duniani.
Maulana Sheikh Hemed jalala katika kutolea mfano hilo anasema “ Ndugu zetu wa Pakistan kwa mfano wako juu katika maswala ya sayansi na technolojia, lakini watanzania tuna ardhi nzuri ya kilimo. Wapakistani wafaidike na ardhi yetu na sisi tufaidike na technoligia yao, Wairani wanavyuo vikuu vingi na vina nafasi, kwetu Tanzania tuna miti mingi na Irani hakuna miti kwa mfano, Sisi watanzania tufaidike na vyuo vikuu vya iran na wao wafaidike na miti yetu hali watoto wetu wapate nafasi za masomo”
Aliongeza na kusema kuwa “Mtume Ibrahim a.s alipafanya Makka kuwa ni Haram (mahali patukufu na amani), mahali ambapo mtu haruhusiwi kukata mti na hata kuwinda mnyama, na Zaidi ya hivyo hata mnyama aliyewindwa nje ya maka haifai kuja kumchinjia pale (katika mwezi wa hijja) lakini mtume s.a.w.w haukuishia na kupafanya maka tu kuwa ndio mahali pa Amani bali aliifanya madina pia kuwa ni haram na mahala paa Amani na mtakatifu, hivyo maka na madina ni sehemu mbili za makao makuu yenu kwaajili ya kutengeneza mambo yenu. Leo wacha tuseme pasina ya kufichaficha ya kwamba BALAA KUBWA LILILOWAKUMBA WAISLAMU NI KUPATA WASIMAMIZI WA SEHEMU HIZI KUWA NI FAMILIA YA AL SAUDI ILIYOUNGANA NA WAFUASI NA SHEIKH MUHAMMAD BIN ABDUL WAHAB NA WAKAWA SAMBAMBA KATIKA KUTENGENEZA SERIKALI YA SAUDI ARABIA. HIVYO NI SERIKALI YA KIWAHABI, YENYE AKIDA (ITIKADI ZA KIWAHABI) INAYOENDESHWA KIFALME NA KIKUNDI CHA WATU FULANI, HAWA NDIO WASIMAMIZI WA MIJI HII MITAKATIFU ”.
Posted on October 2, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0