KHUTBA YA SALA YA IJUMAA NA MNASABA WA MUBAHALA 09/10/2015.

Maulana Samahat Sheikh Hemed jalala Imam na Khatibu wa sala ya ijumaa, alizungumzia tukio la kihistoria la MUBAHALA, katika khutba yake alielezea falsafa na mafunzo ya tukio hilo la ushindi wa waislamu katika historia baina yao na Manaswara wa Najran.

Maulana sheikh Hemed jalala

Maulana Sheikh Hemed Jalala alianza kwa kusema “Moja ya kazi kubwa aliyoifanya mtume Muhammad s.a.w.w alipokuwa madina ilikua ni kuwaandikia barua viongozi wa makabila , wakiristo, mayahudi na wapagani ili kuwaalika katika uislam. Moja ya watu walioandikiwa barua walikua ni wakiristo wa sehemu ya Najran, Watu hawa walivutana na mtume juu ya ujumbe wake na hatimae walifunga safari ili kuja kujadiliana nae juu ya msingi wa uislamu na kuhusu Nabii Issa a.s, Mtume aliwakaribisha katika eneo la msikiti na pia aliwapa sehemu ya kufanya ibada yao.Moja ya mafunzo makubwa tunayoyapata ni kuwa mtume ni alikua akikaa na wasiokuwa waislamu na hata kuwakaribisha msikitini na kujadiliana nao”.

Maulana Sheikh Hemed Jalala aliendelea kuelezea tukio hilo la mubahala ambalo linazungumziwa na historia  ya uislam kuwa wale wakiristo walipopewa kila dalili za kuonyesha Nabii Issa si mwana wa Mungu na wala si Mungu bali ni nabii kama manabii wengine, walikataa na kupinga. Hivyo Allah akateremsha aya ya Quraan iliyoko Surat Imran aya 61 akisema:

”IKIWA WATAKUJADILI JUU YA ISSA BAADA YA WEWE KUWAJIA NA ELIMU, BASI SEMA NJOONI TUWAITE WATOTO ZENU NA WATOTO ZETU, WANAWAKE ZENU NA WANAWAKE ZETU NA NAFSI ZENU NA NAFSI ZETU KISHA TUOMBEANE LAANA IWASHUKIE WAONGO” Imran 61

Maulana Sheikh Hemed jalala alifafanua kuwa mtume alitoka na Hassan na Hussein kama watoto zetu, Fatima zahraa kama wanawake zetu na Ali bin Abi Talib kama Nafsi zetu, Walipokwenda katika sehemu ya maagano wale Wakiristo wa Najran wakasema “Hakika tunaona nyuso ambazo lau kama zitamuomba Mungu ahamishe mlima mahala pake Mungu atauhamisha mlima huo”. Hivyo wakakubali kuishi katika dola ya kiislamu kwa kulipa kodi ili wasiombeane hiyo laana na ushindi ukawa ni wa waislamu. Katika kufafanua hili maulana Sheikh Hemed Jalala alisema:

“Kitendo cha mtume kuwatanguliza watu hawa watukufu katiko tukio hilo la mubahala ni darasa ya kwamba wao ndio viongozi na ikiwa yeyote atashikamana nao basi atashinda dhidi ya yeyote kama vile mtume na uislamu ulivyowashinda Wakristo wa Najran”.

Sheikh Aliendelea na kusema:

“Mtume amesema katika maneno yake marufu ya kwamba anatuachia vizito viwili ikiwa tutashikamana navyo hatutopotea milele, KITABU CHA ALLAH, NA WATU WA NYUMBA YAKE (Ahlulbayt) hawa watu wa nyumba yake ni pamoja na hawa watu watano walioshiriki hilo tukio la maapizano, Hilo ni darasa ya kwamba mtume anatutaka tusiwatangulie kwani tutaangamia na pia tusiwafundishe kwani wao wanajua Zaidi yetu. Maneno ya mtume juu ya vizito viwili yamewaweka Ahlulbayt katika mizani moja na Quraan na ndipo unaona wakiristo wa Najran walisema nyuso za ahlulbayt ni nyuso ambazo lau zitamuomba Allah ahamishe mlima kutoka mahala pake mlima utahama, Quraan inasema lau kama hii Quraan ingeshushwa juu ya mlima basi huo mlima ungepasuka kutokana na hofu juu ya mungu, Hawa Ahlulbayt ni watu waliobeba Quraan ambayo milima haiwezi kuibeba hivyo wanaweza kuhamisha mlima kutoka mahala pake kwa uwezo wa M/mungu, Hao ni viongozi ambao ikiwa waislamu watashikamana nao na kuwatanguliza katika mambo yao watashinda kwa sababu walikua sehemu muhimu ya kuubakiza uislamu, kwani lau waislamu na mtume wangeshindwa katika mdahalo huo na maapizano basi pasingekua na uislamu, Hawa ndio watu twahara Zaidi ya watu wote waliokuwepo na ndio sababu ya mtume kutoka nao na asitoke na wengine na ndipo Quraan inasema “HAKIKA MWENYEZIMUNGU ANATAKA KUWATAKASENI NA KUWAONDOLEENI UCHAFU NA KUWATAKASENI KABISA KABISA”.

Maulana Sheikh Hemed Jalala aliendelea kusema huku akitoa mfano juu wale ambao hawajakamatana na Ahlulbayt jinsi gani wanafeli, huku akitoa mfano alisema:

“Nyote mnajua nguvu kubwa iliyotumika katika bara la Afrika juu ya kukakataza kile walichokiita BIDAA, mfano KHITMA, MAULIDI, TALAQINI na MIKUSANYIKO ya kumtaja mtume, na  badala yake walituletea mikusanyiko mingine kwa jina la kongamano na semina, watu hawa wamefeli kwa kuwa hawana msingi wa uongozi na hawajawatanguliza Ahlulbayt a.s. WATU HAWA WENYE UISLAMU WA BIDAA WAMETULETEA ALLAHU AKBAR AMBAYO INAHALALISHA MTU BADALA YA KUMCHINJA MNYAMA KWAAJILI YA KULA. DUNIA IJUE YA KWAMBA WAISLAMU PEKEE WANAOWEZA KUKAA NA WATU WENGINE MIONGONI MWA WAKIRISTO, MAYAHUDI NA WAPAGANI KAMA MTUME ALIVYOKAA NAO NI WAFUATA AHLULBAYT a.s.”

Maulana Sheikh Hemed jalala aliendelea kusema:

“Leo utawaona hawa watu (Wa kupingana na bidaa) walipoikamata Libya waliwachinja watu na wakiristo kwa kigezo cha wao kutokua waislamu. Utawaona hata pale KENYA walikua wakikamata watu na kuwataka wasome surat Alfatiha ili kujua ni muislamu lasivyo wanakuchinja, Nani kawaambia hicho ni kipimo cha uislamu? Ukitaka kuwaona wameshindwa (Baada ya kutoshikamana na Ahlulbayt) ni pale walipoikamata Aghanistan na kushindwa kufanya chochote cha maana Zaidi YA KUKUSANYA REDIO NA TV NA KUCHAMA KWA KUWA NI BIDAA.”

Hivi mnakwenda wapi? Na kwa nini hamuoni na kuzingatia hali dalili ziko wazi? Tuna mafunzo mengi katika tukio la mubahala na muda hauwezi kuruhusu kuyataja yote

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 10, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: