IBRA ZA ASHURA KWA MANENO WA IMAM KHAMENEI

ScreenShotHii ni ibra ya ajabu katika historia. Pale ambapo wakubwa huingiwa na khofu; pale ambapo adui anaonyesha sura ya kikatili kabisa; pale ambapo watu wote huhisi kwamba endapo watajitosa kwenye medani ya jihadi watabaki peke yao – hapo ndipo thamani, dhati na batini za watu zinapobainika. Katika ulimwengu mzima wa Kiislamu wa zama hizo ambao ulikuwa ni ulimwengu mkubwa unaojumuisha nchi nyingi za Kiislamu ambazo leo hii kila moja imejitenga na nyingine, nchi zote hizo zilikuwa ardhi moja yenye idadi kubwa mno ya watu. Katika mazingira kama hayo, Husain bin Ali AS ndiye mtu aliyeweza kuchukua uamuzi huo, na kwa azma na ujasiri akawa kukabiliana na adui.

Ni jambo lililo dhahiri kwamba akitokea mtu kama Imam Husain kuanza mapambano, watatokea watu kadhaa kusimama nyuma yake – na hali hivyo ndiyo ilivyotokea kwake. Ingawa watu hao nao ilipodhihirika kwamba jihadi iliyokuwa ikiwakabili mbele yao ilikuwa ni nzito na ngumu mno, mmoja mmoja kati yao walimwacha mkono Imam, kiasi kwamba kati ya watu wapatao elfu na ushei ambao waliandamana na Imam Husain AS alipoondoka Makka, au walijiunga naye huko njiani (kuelekea Karbala), ilipofika usiku wa kuamkia Ashura, ni watu wachache tu ndio waliokuwa wamebaki pamoja naye, ambao ukijumuisha na wale walioungana naye katika siku ya Ashura, idadi yao ilikuwa ni watu 72 tu! Huku ni kufanywa madhulumu (mnyonge)! Dhulma hii maana yake si kudunishwa au kudhalilishwa.

Imam Husain AS ni mujahidi na mwanaharakati mkubwa kabisa katika historia ya Uislamu – kwa sababu alisimama bila khofu na kupigana jihadi katika mazingira kama hayo. Pamoja na hayo, kwa kuzingatia hadhi yake ilivyo, mwanadamu huyu mkubwa alitendewa dhulma. Dhulma aliyofanyiwa ni kubwa kwa kadiri ulivyo ukubwa na adhama ya shakhsia yake, na akauawa shahidi pia katika hali ya ukiwa. Kuna tofauti kati ya yule askari anayejitolea mhanga tu nafsi yake na kwenda kwenye uwanja wa mapambano kwa makeke na hamasa. Askari huyo hushajiishwa na watu huku wakimpigia nara za jina lake ili kumtia hamasa na kumsifia. Pembezoni mwa medani ya vita anakuwa amezungukwa na watu wenye hamasa sawa na yeye. Huwa anajua kwamba endapo atajeruhiwa au kuuawa shahidi namna gani watu watakavyomtukuza kwa hamasa. Kuna tofauti kati ya askari huyu na yule mtu anayesimama na kupambana akiwa ameridhia kadari ya Mwenyezi Mungu na kuwa tayari kufa katika njia yake huku akiwa katika mazingira ya dhulma, ukiwa, upweke, bila ya kuwa na msaidizi wala matumaini ya kupata msaada wowote kutoka kwa watu, huku adui akiwa ameeneza sumu kubwa ya propaganda dhidi yake. Hii ndiyo adhama ya mashahidi wa Karbala! Yaani hawakukhofu ukubwa wa adui pale walipotambua wajibu walionao ambao ni kupigana jihadi kwa ajili ya dini na katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hawakupatwa na kihoro kwa sababu ya upweke wao. Kuwa ndogo idadi yao hawakukitumia kama hoja ya kujuzisha kukimbia na kukwepa kukabiliana na adui. Hili ndilo linalompa adhama mtu, kiongozi na taifa – kutokhofu haiba bandia ya adui.

Bwana wa Mashahidi (‘alayhi ‘s-salatu wa ‘s-salaam) alikuwa anajua kwamba baada ya yeye kuuawa shahidi, adui ataitumia kila fursa aliyonayo katika jamii na ulimwengu wa zama zile kueneza propaganda dhidi yake. Imam Husain AS alikuwa na matumaini kwamba hiyohiyo harakati katika mazingira ya kidhulma na ukiwa, hatimaye itaweza kushinda dhidi ya adui na matunda yake kuonekana katika kipindi cha muda mfupi tu na muda mrefu ujao. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Anakosea mtu kudhani kwamba Imam Husain AS alishindwa. Kuuawa hakuna maana ya kushindwa. Katika medani ya vita aliyeuawa hakushindwa, bali aliyeshindwa ni yule anayeshindwa kufikia lengo lake. Lengo la maadui wa Imam Husain AS lilikuwa ni kuufuta Uislamu na kumbukumbu za Utume. Nao ndio walioshindwa kwa sababu hilo halikujiri. Lengo la Imam Husain AS lilikuwa ni kuuvuruga mkakati wa maadui wa Uislamu ambao ima walikuwa wameshaeneza au walikusudia kuhakikisha wanaeneza kila mahali aina ya Uislamu wautakao wao. Hivyo Imam Husain AS akaweza kufikisha kila mahali ujumbe wa Uislamu, kilio cha haki yake na dhulma aliyotendewa, na mwishowe kupelekea kushindwa kwa adui wa Uislamu. Na ikatokea kuwa hivyo.

Ushindi wa Imam Husain AS uliweza kuonekana baada ya kupita muda mfupi tu na baada ya muda mrefu pia. Baada ya kupita muda mfupi mapambano hayo na kuuawa kwake shahidi pamoja na kuchukuliwa mateka watu wa ukoo wa mtukufu huyo, kuliuteteresha na kuuyumbisha utawala wa Bani Umayya. Ilikuwa ni baada ya tukio hilo ambapo katika ulimwengu wa Kiislamu huko Makka na Madina yalijiri mfululizo wa matukio ambayo hatimaye yalipelekea kutoweka kwa silsila ya ukoo wa Abu Sufyan. Katika kipindi cha miaka mitatu hadi minne, silsila ya ukoo waAbu Sufyan ilisambaratika na kutoweka kabisa. Ni nani angetarajia kwamba adui huyo aliyemwua shahidi kidhulma Imam Husain AS huko Karbala angeweza kushindwa kama hivyo kutokana na athari ya mayowe ya Imam huyo – tena basi katika kipindi cha miaka mitatu minne tu hivi? Katika kipindi kirefu pia Imam Husain AS ndiye aliyekuwa mshindi katika kadhia ya Karbala. Angalieni historia ya Uislamu ili mwone jinsi dini hii ilivyoendelea ulimwenguni! Mweze kuona vipi Uislamu ulivyokita mizizi! Vipi mataifa ya Kiislamu yalivyoamka na kupata nguvu! Elimu za Kiislamu zilipiga hatua. Fikihi ya Kiislamu ikapiga hatua na hatimaye baada ya kupita karne kadhaa bendera ya Uislamu inapepea katika vilele virefu kabisa vya dunia.

Je, Yazid na ukoo wa Yazid walikuwa radhi kuona Uislamu unakua na kustawi kama hivi siku baada ya siku? Wao walitaka kuing’oa mizizi ya Uislamu. Walitaka majina ya Qura’ni na Mtume wa Uislamu yasibakie. Lakini tunachoshuhudia ni kinyume na hivyo. Hivyo, yule mujahidi na mwanamapambano katika njia ya Mwenyezi Mungu ambaye alisimama katika hali ya kuwa madhulumu na kukabiliana na adui na damu yake kumwagwa, na watu wa nyumba yake kufanywa mateka, alimshinda adui wake katika hali zote.

Hili ni funzo kwa mataifa. Na ndiyo maana viongozi mbalimbali wakubwa wa zama hizi wakiwemo hata wale wasiokuwa Waislamu wamenukuliwa wakisema: “Sisi tumejifunza njia ya mapambano kutoka kwa Husain bin Ali AS.” Mapinduzi yetu pia ni mfano mmojawapo. Watu wetu nao pia wamepata funzo kutoka kwa Husain bin Ali AS. Walijifunza kuwa kuuawa hakumaanishi kushindwa. Walifahamu kwamba kusalimu amri mbele ya adui anayeonekana kidhahiri kuwa na nguvu ni kujitumbukiza kwenye nakama tu na maangamizi. Adui hata awe na nguvu kiasi gani, endapo upande wa waumini na kundi la waumini litatawakali kwa Mwenyezi Mungu na kupigana jihadi dhidi yake, mwishowe, adui atashindwa na kundi la waumini litashinda. Wananchi wetu walilifahamu hili pia.

((Hotuba aliyoitoa tarehe 30 Dhulhijja 1412 Hijria mbele ya matabaka mbalimbali ya wananchi kwa mnasaba wa kuwadia mwezi wa Muharram)

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 15, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: