MJUE IMAMU IMAM HUSEINI BIN ‘ALI (A.S.)

The_Birth_Of_Imam_Hussain

Jina:          Huseini.

Kuniyah:    Abu ‘Abdillah.

Lakabu:    Sayyidu ‘sh-Shuhadã.

Baba:         ‘Ali bin Abi Tãlib

Mama:      Fatimah bint wa Mtume.

Kuzaliwa:   3 Shabani 4 A.H. Madina

Kufariki:     10 Muharram 61 A.H. Karbala, Iraq.

1.  Kuzaliwa na maisha yake ya mwanzo:

Imamu Huseini (Sayyidu ‘sh-Shuhadã / Bwana miongoni mwa mashahidi), mtoto wa pili wa’Ali na Fatimah, alizaliwa mwaka wa 4 A.H., na baada ya kaka yake Imamu Hasani kuuliwa shahidi  akawa Imamu kwa amri ya Allah (kupitia kwa Mtukufu Mtume) na wosia wa kaka yake.

Imamu Huseini siku zote alikuwa na kaka yake wakati wa uhai wa mtume na Imamu ‘Ali; alichangia katika matukio muhimu zaidi ya kipindi hicho. Alikuwa bega kwa bega na kaka yake wakati wa kipindi kigumu cha Uimamu wa kaka yake. Uimamu wake mwenyewe ulikuwa wa kipindi cha miaka kumi

2.  Utawala wa Mu’awiyah:

Imamu Huseini aliishi chini ya masharti magumu ya uonevu na mateso. Hii ilitokana na ukweli kwamba awali ya yote sheria za dini na kanuni zimepoteza uzito na sifa zake nyingi na sheria za serekari ya Bani Umayya zimepata mamlaka kamili na uwezo. Pili, muawiyah na wasaidizi wake walitumia kila njia inyowezekana kuwaweka kando na kuwaondoa nje ya njia Ahlul Bayit wa Mtume na Shi’ah, na hivyo, kufutilia mbali jina la ‘Ali  na familia yake. Na juu ya yote, Mu’awiyah alitaka kuimarisha msingi wa ukhalifa wa mtoto wake, Yazidi, ambaye kwa sababu ya ukosefu wake wa kanuni na aibu alipingwa na kundi kubwa la Waislam. Kwahiyo, ili kuzima upinzani wote, Mu’awiyah alichukuwa njia mpya na kali zaidi, kwa nguvu na kulazimika, Imamu Huseini aliishi siku hizo na kuvumlia kila aina ya uchungu wa akili na kiroho na mateso kutoka kwa Mu’awiyah na wasaidizi wake – mpaka katikati ya mwaka wa 60 A.H. Mu’awiyah alifaliki na mtoto wake Yazidi akachukua nafasi yake.                                   

3.  Yazid Adai Bay’ah

Kiapo cha utii (bay’ah) ilikuwa ni desturi ya zamani ya Kiarabu ambayo ilikuwa ikifanywa katika mambo muhimu sana kama yale ya ufalme na utawala. Wale ambao walikuwa wakitawaliwa, na hususani wale wanaojulikana sana miongoni mwao, watatoa mkono wa kiapo, makubaliano na utii kwa mfalme au malikia wao na kwa njia hii wataonyesha kuunga kwao mkono vitendo vyake. Kutokubaliana na hayo baada ya kula kiapo cha utii kulichukuliwa kama aibu na kujivunjia heshima kwa mtu, ni kama kuvunja mkataba baada ya kuwa umekwisha sainiwa rasimi, ilikuwa ikuchukuliwa kama jinai ya wazi kabisa. Kwa kufuata mfano wa Mtukufu Mtume, watu waliamini kwamba kiapo cha utii kama kikitolewa kwa utashi na sio kwa nguvu, hubeba uzito na mamlaka.

Mu’awiyah aliwataka watu wanaojulikana sana miongoni mwa watu kula kiapo cha utii kwa mwanae Yazid, lakini hakuliweka ombi hili juu ya Imamu Huseini. Alimuambia Yazid katika wosia wake wa mwisho kwamba kama Huseini akikataa kula kiapo cha utii kwako, basi aliache hilo lipite kimya kimya, na habari yenyewe aipuuze, kwani alielewa kwa usahihi kabisa majanga ambayo yangetokea kama suala hili lingelazimishwa kwa nguvu. Lakini kwa utovu wake wa dini na ukatili  wake, Yazid alipuuza ashauri wa baba yake na punde tu baada ya kifo cha baba yake alimuamrisha gavana wa Madina mambo mawili, amma amlazimishe Imamu Huseini kula kiapo cha utii au apeleke kichwa chake Damascus.

Baada ya gavana wa Madimna kumjulisha Imamu kuhusu matakwa haya ya Yazid, Imamu alikataa kukubaliana na matakwa hayo ya Yazid, na ilipofika usiku wa manane aliondoka yeye na familia yake kuelekea Makka. Alichukua hifadhi katika sehemu takatifu ya Mungu ambayo katika Uislamu ni sehemu rasimi ya kukimbilia na usalama. Kadhia hii ilitokea mwishoni mwa mwezi wa Rajabu na mwanzoni mwa mwezi wa Shabani mwaka wa 60 A.H. Imamu Huseini alikaa uhamishoni mjini Makka karibu miezi minne. Habari hizi zilienea pote katika ulimwengu wa ki-Islamu. Kwa upande mwingine watu wengi ambao walikuwa wamechoshwa na dhulma za utawala wa Mu’awiyah na zaidi kutoridhishwa wakati Yazid atakapokuwa Khalifa, waliwasiliana na Imamu na kumuelezea imani yao kwake. Kwa upande mwingine mafuriko ya barua yalianza kufurika, hususani kutoka Iraq na haswa kutoka mji wa Kufa, wakimkaribisha Imamu aende Iraq na akubali utawala wa wengi kule pamoja na lengo la kuanzisha harakati za kukabiliana na dhulma na unevu. Kwa namna ilivyo, hali kama hiyo ilikuwa hatari mno kwa Yazid.

Imamu Huseini aliendelea kukaa mjini Makka mpaka wakati wa msimu wa hijja wakati Waislamu kutoka ulimwenguni pote wlipoanza kumiminika kuingia mji Makka kwa makundi kwa ajili ya kutekeleza ibada ya hijja. Imamu aligundua kwamba baadhi ya wafuasi wa Yazid wameingia Makka kama mahujaji wakiwa wamepewa amri ya kumuua Imamu wakati wa ibada ya hijja na huku wakiwa wamebeba silaha ambazo wamezificha ndani ya ihram zao.

Imamu alifupisha ibada ya hijja na kuamua kuondoka. Katikati ya mkusanyiko mkubwa wa watu, alisimama na katika hutuba fupi alitamka kwamba anaondoka kuelekea Iraq. Katika hotuba hii fupi, vile vile alitangaza kwamba angeuliwa shahidi na akawataka Waislamu kumsaidia katika kulifikia lengo ambalo analo katika mawazo yake na kutoa maisha yao katika njia ya Allah (swt). Siku iliyofuatia aliondoka yeye na familia yake na kikundi cha masahaba zake kuelekea Iraq.

Imamu huseini alikuwa ameamua kutokula kiapo cha utii kwa Yazid na alielewa vizuri sana kwamba tauawa. Alikuwa anafahamu ya kwamba kifo kilikuwa hakiepukiki mbele ya jeshi lenye nidhamu ya woga la utawla wa Bani Umayyah, ukiungwa mkono kama ilivyo na baadhi ya sekta, uporomokaji wa kiroho, na ukosefu wa utashi miongoni mwa watu, haswa katika nchi ya Iraq. Baadhi ya watu maarufu wa Makka walisimama upande wa Imamu Huseini na wakamuonya juu ya hatua ambayo anataka kuichukuwa. Lakini alijibu kwamba alikataa kula kiapo cha utii na kutoa uthibitisho wake kwa serikali ya dhulma na madhalimu. Aliongeza kusema kwamba alijua kwamba popote atakapoelekea au kwenda angeuliwa. Ataondoka ili kulinda heshima ya nyumba ya Allah (swt) na kutoruhusu heshima hii kuharibiwa kwa damu yake kumwangwa pale.

4.  Kuelekea Karbala

Wakati akiwa njiani kuelekea Kufa na ikiwa ni siku chache tu toka aondoke Makka, alipokea habari kwamba wakala wa Yazid katika Kufa amemuua muwakilishi wa Imamu katika mji huo na ambaye vile vile alikuwa mmoja wa watu walioamua kumuunga mkono, mtu anayejulikana sana mjini Kufa. Baada ya vifo vyao, miguu yao ilifungwa na kuburuzwa mitaani. Mji pamoja na vitongoji vyake uliwekwa chini ya uangalizi mkali, na wanajeshi wasio idadi wa adui waliwekwa tayari kumsubiri Imamu wamshike. Ilikuwa hakuna njia nyingine kwake isipokwa kuendelea mbele na kukikabili kifo. Hapa ndio sehemu ambapo Imamu alielezea uamuzi wake imara wa kuendelea mbele akauawe shahid; na hivyo aliendelea na safari yake.

Takriban kilometa sabini kutoka Kufa, katika jangwa linaloitwa Karbala, Imamu na msafarea wake walizunguukwa na jeshi la Yazid. Kwa muda wa siku nane walikaa katika hali hii wakati ambapo ukawa mwembamba na idadi ya jeshi la adui iliongezeka. Hatimaye Imamu pamoja na familia yake na idadi ndogo ya masahaba wake walizunguukwa na jeshi la askari sabini elfu. Wakati wa siku hizo Imamu aliimarisha msimamo wake na akafanya uchanguzi wa mwisho wa masahaba zake. Ulipoingia usiku aliwaita masahaba zake na katika hotuba fupi alieleza kwamba hakuna chochote mbele yetu isipokuwa kifo na shahada. Aliendelea kusema kwamba kwa vile maadui walikuwa na haja na yeye tu binafsi, angewatoa katika majukumu yote haya hivyo kwamba mtu yeyote anayetaka anaweza kutoroka katika giza hili na kuokoa mnaisha yake. Kisha aliamrisha taa zizimwe na wengi wa wale waliojiunga kwa manufaa yao walitawanyika na kuondoka. Ni wale wachache tu ambao waliipenda haki na Banu Hashim walibaki.

Kwa mara nyingine tena Imamu aliwakusanya wale ambao wamebaki na akawaweka katika mtihani. Waliwahutubia masahaba zake na jamaa wa Banu Hashim, akisema tena, maadui wanamtaka yeye tu binafsi. Kila mmoja anaweza kunufaika na giza hili la usiku na kujiepusha na hatari. Lakini safari hii masahaba waaminifu wa Imamu kila mmoja alijbu kwa njia yake kwamba hata mara moja hawtapotoka kutoka njia ya haki ambayo Imamu alikuwa kiongozi na kamwe hawatamuacha peke yake. Walisema watailinda familia yake mpaka tone la mwisho la damu yao, na ilimradi muda wanaweza kubeba panga zao.

Katika siku ya tisa ya mwezi wa Muhrram maadui walimfanyia Imamu changamoto ya mwisho ya kuchagua kati ya “kiapo cha utii au vita”. Imamu aliomba kuahirishwa hilo lli kwamba aweze kufanya ibada usiku ule na kuwa katika uwamuzi imara wa kuingia katika vita siku inayofuata.

Katika siku ya kumi ya Muharram mwaka wa 61/680 Imamu alijipanga mbele ya maadui pamoja na kundi dogo la wafuasi wake, watu si chini ya tisini ambao ni masahaba zake, thalathini ambao ni baadhi ya asikari wa jeshi la maadui ambao walijiunga naye wakati wa usiku na siku ya vita, na watoto wa familia ya Banu Hashim, ndugu zake, wapwa, na binamu zake. Siku ile walipigana kuanzia asubuhi mpaka pumzi yao ya mwisho, na Imamu na vijana wa kibanu Hashim na masahaba wote waliuawa mashahidi. Mwiongoni mwa wale waliuliwa ni watoto wawili wa Imamu Hasani ambao mkubwa alikuwa na miaka kumi na tatu na mdago alikuwa na miaka kumi na moja; na mtoto wa miaka mitano na mtoto mchanga anaye nyonya wote wa Imamu Huseini.

Baada ya vita kwisha, jeshi la adui liliteka nyara familia ya Imamu na kuchoma mahema yake. Waliikatakata miili ya mashahidi. Waiiacha uchi na kuiacha bila kuizika. Kisha wakaondoka na jamaa ya familia yake, wote walikuwa ni wanawake na wasichana wsiojiweza, sambamba na vichwa vya mashahidi, mpaka Kufa. Miongoni mwa wafungwa alikuwepo jamaa watatu wa kiume; mtoto wa miaka ishirini wa Imamu Huseini ambaye alikuwa anaumwa sana na hawezi kutembea, aitwaye ‘Ali bin Huseini, Imamu wa nne; mtoto wake wa miaka minne, Muhammad ibn ‘Ali, ambaye alikuja kuwa Imamu wa tano. Maadui waliwachukuwa wafungwa mpaka na kutoka pale mpaka Damascus mbele ya Yazid.

5.   Matokeo ya Karbala:

Matekeo ya Karbala, kutekwa kwa wanawake na watoto wa Ahlu ‘l-Bayit wa Mtukufu Mtume, kuchukuliwa kwao wafungwa kutoka mji mwingine mpaka mji mwingine na hotuba zilizotolewa na binti wa ‘Ali, Zainabu, na Imamu wa nne ambaye alikuwa miongoni mwa wafungwa, iliwaabisha Banu Umayya. Unyanyasaji huu wa familia ya Mtume ulitangua propaganda ambayo Mu’awiyah aliifanya kwa miaka mingi. Suala hili lilifikia ukubwa kiasi kwamba Yazid alilazimika kukana hadharani na kulaani vitendo vya mawakala wake.

Tukio la Karbala lilikuwa ni kipengele kikubwa katika kupinduliwa kwa utawala wa Banu Umayah ingawa matokeo yake yalicheleweshwa. Miongoni mwa matokeo yake ya mara moja ilikuwa ni maasi na vurugu zilizo changanyika na umwagaji damu ambao uliendelea kwa muda wa miaka kumi na mbili. Miongoni mwa wale ambao walikuwa ni wahusika katika kifo cha Imamu, hakuna hata mmoja ambaye aliweza kuepuka kisasi na adhabu.

Mtu ambaye anachunguza kwa ukaribu historia ya maisha ya Imamu Huseini na Yazid na hahi ambayo ilikuwepo wakati ule, na akachambua sura hii ya historia ya ki-Islamu, atakua hana shaka yoyote kwamba katika mazingira hayo kulikuwa hakuna hiari mbele ya Imamu Huseini bali kuuliwa tu. Kula kiapo cha utii kwa Yazid kungelimaanisha kuonyesha hadharani kuutweza Uislamu, kitu ambacho kilikuwa hakiwezikani kwa Imamu, kwani Yazid hakuonyesha kutokuuheshimu Uislamu tu na maamrisho yake bali vile vile alionyesha kwa vitendo hadharani usafihi. Akikanyaga chini ya miguu yake misingi yake na sheria zake. Wale waliokuwa kabla yake, ingawa walipinga sheria za dini, siku zote walifanya hivyo kwa kutumia pazia la dini, na angalau mwanzoni waliheshimu dini. Walijifaharisha kwa kuwa masahaba wa Mtukufu Mtume (saw) na watu wengine wa dini ambao watu waliwaamini.

Kutokana na hili inaweza kuhitimishwa kwamba, madai ya baadhi ya wafasiri wa matukio haya ni ya uwongo wakati wakisema kwamba ndugu hawa wawili, Hasani na Huseini walikuwa na ladha mbili tofauti na kwamba mmoja alichangua njia ya amani na mwingine njia ya vita, hivyo kwamba ndugu mmoja alifanya amani na Mu’awiyah ingawa alikuwa na jeshi la watu arubaini elfu, ambapo mwingine alikwenda vitani dhidi ya Yazid na jeshi la watu chini ya mia moja. Kwani tunaona kwamba Imamu Huseini huyu huyu, ambaye alikataa kula kiapo cha utii kwa Yazid kwa siku mmoja, aliishi miaka kumi chini ya utawala wa Mu’awiyah katika hali ile ile kama ndugu yake, ambaye vile vile alivumilia kwa muda wa miaka kumi chini ya Mu’awiyah bila kumpinga.

Lazima isemwe katika ukweli kwamba kama Imamu Hasani au Imamu Huseini wangelipigana na Mu’awiyah wangeuliwa bila kuwepo kwa faida yoyote kwa Uislamu. Vifo vyao vingelikuwa havina athari mbele ya sera za Mu’awiyah ambazo kwa nje zinaonekana kwamba ni sahihi, mwanasiasa hodari ambaye alisisitiza kuwa kwake sahaba wa Mtukufu Mtume (saw), “mwandishi wa wahayi,” na “mjomba wa waumini,” na ambaye alitumia kila aina ya hila iwezekanayo kuhifadhi pazia la dini kwa ajili ya utawala wake. Aidha, kwa uwezo wake wa kuweka jukwaa kwa ajili ya kukamilisha matamanio yake angeliweza kuwafanya wauawe na jamaa zao wenyewe na akafanya maombolezi ya kitaifa na kutafuta kulipiza damu yao, kama vile alivyojifanya kwamba alikuwa akilipiza kisasi kifo cha Khalifa wa tatu.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 15, 2015, in Habari na Matukio, Uncategorized and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: