SAFARI YA IMAM HUSEIN (A.S) TOKA MADINA HADI MAKKA

Baada ya Imam Hasan (a.s.) kufariki. Mashia waliokuwa Iraq walimuandikia Imam Husein kumjulisha kwamba wao waniempa baia na wako tayari kumnusuru.
Imam (a.s.) aliwajibu kwa kusema: “Baina yetu ma Muawiya upo mkataba kuhusu jambo hili, hivyo haifai kuuvunja mkataba huo”.

Katikati ya mwezi wa Rajab mwaka wa Sitini Hijiriyah Muawiyyah Bin Abi Sufian alikufa na Yazid mwanawe Muawiyyah akachukua mahali pa baba yake, na ile ahadi na makubaliano aliyoyafanya Imam Hasan na Muawiyyah yakavunjwa, kwani usia wa Muawiyyah ulitaka Yazid ndiyo awe Khalifa kinyume na makubaliano kwamba atakapokufa Muawiyyah ukhalifa urudishwe katika nyumba ya Mtume (s.a.w.).

Basi ilikuwaje alipochukua Ukhalifa Yazid yule mlevi asiyejali utu wake, mcheza na mbwa, hana akijuacho katika dini kama alivyokiri yeye mwenyewe ndani ya ibara ziftuatazo baada ya kukalia Ukhalifa akasema: “… na kwa hakika nimetawazwa baada yake (Muawiyyah) na wala sitowi udhuru (wa kuacha jambo hili) kutokana na ujinga (nilionao) na wala sijisumbui kutafuta elimu”.

Taz. Kitabu cha Qawaid AI-Lughatil-Arabiya Juz.3 Uk.48 chapa ya pili mwaka 1973-1393. Kitabu hiki kinatolewa na Wizara ya Elimu ya Saud Arabia kwa ajili ya shule za kati kwa wasichana ndani ya sahi ya tatu.”[1]

Jambo aliloona kwamba ndiyo maslahi kwake yeye Yazid, ni kuandika barua kumpelekea lbn Ami yake Walid bin Utba ambaye alikuwa ndiyo Gavana wa Madina siku hizo, akamuamuru achukue baia kutoka kwa watu wote na kutoka kwa Imam Husein (a.s.) kwa niaba yake yeye Yazid, akasema katika barua hiyo “Iwapo Husein (a.s.) atakataa kutoa baia basi muuwe na uniletee kichwa chake”.

Walid bin Utba alipoipata barua hiyo alimtaka ushauri Marwan.

Marwan akamwambia Walid “Hakika Husein (a.s.) hawezi kumbai Yazid, lakini Iau mimi ningekuwa na cheo kama chako ningemuua.”

Baadaye Walid alimwita Imam Husein (a.s), naye akaja kwa Walid akiwa na watu thelathini miongoni mwao wakiwa ni watu wa nyumba yake na wafuasi wake.

Imam Husein (a.s.) alipofika mbele ya Walid, yeye Walid akamjulisha Imam (a.s.) juu ya kifo cha Muawiyyah na pia akawa anamlazimisha ampe baia Yazid.

Imam Husein (a.s.) akamwambia “Hakika kiapo cha utii (baia) siyo jambo la siri, basi kesho waite watu nasi pia tuite (tutafanya hiyo baia).

Marwan akasema kumwambia Walid “Ewe Amir usikubali udhuru wake, kama ni baia atowe sasa hivi au sivyo muuwe.” Imam Husein (a.s.) akakasirishwa na maneno ya Marwan akamwambia “Ewe mwana wa Zarqaa unaniuwa wewe au yeye? Hakika wewe ni muongo tena umefanya jambo Ia uovu (Kutamka hivyo)”. Kisha Imam akamgeukia Walid akasema: “Kwa yakini sisi ndiyo watu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w.), na kwetu ndiyo kwenye kituo cha Ujumbe (wa Mwenyezi Mungu) na Mwenyezi Mungu alileta nusra kupitia kwetu sisi na akaukamilisha Ujumbe wake kwa Ulimwengu kwetu sisi, na huyu Yazid ni mtu mlevi, muuwaji wa nafsi bila sababu, anafanya maovu wazi wazi, kwa hiyo basi watu kama mimi hawawezi kumpa baia mtu kama yeye”. Kisha Imam Husein (a.s.) alitoka mahala hapo akaenda zake.

Marwan akamwambia Walid: “Unaona ulipinga ushauri wangu”. (Sasa Husein amekukatalia wazi wazi) Walid akamkemea Marwan akasema: “Kefule!!! Ulilokuwa umenishauri ni jambo la kuniharibia Dunia yangu na Akhera yangu, Wallahi sipendi kuona Dunia yote inakuwa yangu wakati nitakuwa nimemuuwa Husein eti kwa sababu amesema hatombai Yazid, walasidhani kama ye yote atakayemuuwa Husein kwamba atakutana na Mwenyezi Mungu akasalimika, bali mtu huyo atajikuta siku ya Qiyama mizani yake ni nyepesi (hana chochote) na Mwenyezi Mungu hatomtazama mtu huyo wala hatamtakasa na atapata adhabu kali”. (kwa kumuuwa Husein).

Basi Imam Husein alikaa Nyumbani kwake usiku huo ambao ulikuwa ni usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 27 Rajab mwaka wa Sitini.

Kulipokucha akatoka ili apate kujua habari zilizoko mjini, mara akakutana na Marwan, kisha Marwan akasema: “Ewe Abu Abdillah (Imam Husein) mimi ninayo nasaha kwa ajili yako tafadhali nitii kwa nitakayokuambia utafanikiwa”.

Imam Husein (a.s) akasema: “Ni nasaha gani hiyo sema niisikie”?

Marwan akasema: “Hakika mimi nakuamuru umtii Yazid kwani jambo halo ni bora kwako na ni bora katika Dini yako na Dunia yako”.

Imam Husein (a.s.) akasema: “Hakika sisi ni milki ya Mwenyezi Mungu na hakika sisi kwake tutarejea, Eti mimi kumtii Yazid ndiyo itakuwa ni amani kwa Uislamu? Hakika Ummah umepata mtihani mkubwa kwa kuwa na kiongozi mfano wa Yazid”.

Mazungumzo baina yao yalikuwa mengi kiasi ambacho Marwan aliondoka il-hali kachukia.

Jioni ya Jumamosi Walid alituma watu waende kwa Imam Husein (a.s.) ili aje afanye baia.

Imam Husein akawaambia: “Ngojeni kutapokucha kesho kisha mtaona ni lipi la kufanya, nasi pia tutaona la kuamua”. Wakanyamaza wala hawakuendelea kumlazimisha afanye baia.

Basi Imam Husein alitoka usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 28 Rajab kuelekea Makkah, pamoja na wanawe na ndugu zake na kikundi cha watu wa nyumba yake, akaondoka Madina hali anasoma Aya ya Qur’an isemayo: “Akatoka katika mji huo hali anakhofu, anangoja (lipi litamfika) akasema: “Mola wangu niokowe kutokana na watu madhalimu”. Sura Al-Qasas Aya 21.

Alipita njia kuu iliyo mashuhuri, akaombwa abadili njia kukwepa kufuatwa na adui kama alivyofanya Ibnuz-Zubair, akakataa kufanya hivyo na akasema: “Sitaiacha njia hii mpaka Mwenyezi Mungu aamuwe chochote atakachoniamulia”.

Imam Husein (a.s) alifika Makkah usiku wa kuamkia Ijumaa tarehe tatu Shaaban, na aliingia Makkah huku akisoma Aya ifuatayo:

“Na alipoelekea upande wa Madiyan alisema: Huenda Mola wangu ataniongoza njia iliyo sawa”. Sura Al-Qasas Aya 22.

Alikaa hapo Makka kuanzia Mwezi huo wa Shaaban mpaka mfungo pili na siku nane za Mwezi wa mfungo tatu, kisha aliona usalama wake pale Makka in mdogo.

Kwa hiyo Imam Husein hakuwa na utulivu tena wa kumuwezesha kukamilisha Ibada yake ya Hija kwa kuhofia kukamatwa na majasusi ambao wangemkamata hapo Makka na kumpeleka kwa Yazid Bin Muawiyyah.

Hivyo basi akafungua Ihram yake na akaifanya kuwa ni Umra.

Imam Husein (a.s.) akautoka Mji wa Makka ambao in Mji wa Mwenyezi Mungu uliotukuka, katika Mji huo ndege na wanyama wanapewa amani waingiapo, basi vipi kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.) kutishiwa amani yake?

Alitoka Makka kama alivyo uacha mji Mtukufu wa Madina mji wa babu yake ambaye in Mtume wa Mwenyezi Mungu, hali anakhofu mwenye kungojea lipi litamtokea.

Notes:
[1] Ibara hii haiko ndani ya Kitabu cha asili bali tumeiongeza tu ili kuonesha udhaifu wa Yazid

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 18, 2015, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: