SHEIKH JALALA: ATOA MKONO WA HERI NA PONGEZI ZA KRISMAS KWA WAKRISTO NCHINI

23/12/2015

Kigogo, Dar es Salaam.

Leo Uongozi wa chuo cha Dini ya Kiislamu Mawlana Sheikh Hemedi Jalala ametoa mkono wa Heri na Pongezi kwa Wakristo wote Nchini kwa Sikuku ya kukumbuka Kuzaliwa Yesu Kristo inayosherehekiwa kitaifa na kimataifa kila Tarehe 25 Mwezi Disemba.

Akitoa salaam za Krismas  na  Mwaka  Mpya kwa  wakristo wote  Duniani,  katika mkutano  wake na waandishi  wahabari  uliofanyika  katika  Chuo cha Dini ya Kiislamu cha Imam Swadiq  Kigogo jijini Dar es slaam, Maulana Sheikh Hemed  Jalala alisema:

“sisi  kama Waislaamu, viongozi  wa dini, watanzania, na kama wanaadam wadau wa Amani nchini tunayo haki  ya kuwapa mkono wa  kheri  ya  krismas ndugu zetu wa dini ya Kikristo  kwa kusema Hongereni kwa Sikuku ya Kukumbuka kuzaliwa Yesu Kristo (Nabii Issa  as)

Kwanini tumeitisha  vyombo vya  habari?

Aidha Maulana   alifafanua dhamira ya kuitisha vyombo vya habari na alisema “sababu kubwa  iliyotufanya  kuwaita  vyombo  vya  habari  ni  kuwatangazia Watanzania kuwa: Wakristo ni ndugu zetu, ndugu zetu katika  Asili moja, sote  tunatokana na Baba mmoja  Adam as na Hawaa (Eva).” Wakristo  na  waislaam  wote  baba yao  ni Adam na  mama  yao ni Hawa (Eva), kwanini  tusipongezane  wakati sisi  ni wa asili  moja?  Tofauti  tulizo nazo  za kiitikadi na Kiimani hazivunji  udugu huu  wa Asili. Sisi waislamu Mwenyezi  Mungu  (sw)  anatukumbusha  katika Quraan )Sura Hujurat Aya 39-13) akisema…. Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari”

Aliendelea Kusisitiza na kusema “sisi  ni ndugu  kwa kuwa  ni watu  wenye dini,  sote tunaamini  mungu  mmoja japo kua kuna  tofauti za kumtambulisha Mungu mmoja, tunaamini  kuwa  ipo siku ya  mwisho  (Kiama), siku  ya  kuhesabiwa, Tunaamini uwepo wa Malaika pia. Tunaamin  vitabu Vitukufu Vilivyoletwa  kwa Mitume  kuja kuwaongoza watu.  Torati aliyopewa  Nabii  Musa,  Zaburi  aliyopewa  Nabii Daudi, Injili  aliyopewa  Nabii Issa, (Yesu). Na  Qur aan  aliyopewa Mtume Muhammad  (Rehema za Mwenyezimungu ziwe juu yao wote), ikiwa  wakristo  wanaamini  katika  Tourat, injili  na  Zabuur,  ni mahala  pake  kuwapongeza, kwani watu  wa  kitabu, hata Qur aan  inawaita  kwa  majina  mazuri, Enyi  watu  wa kitabu.

Mawlana Sheikh jalala aliongeza kusema “waislaam  wanawaangalia Wakristo kuwa ni  ndugu  zetu, wanzetu, Wanaadam wenzetu na wala  sio maadui,  ndio  maana Mtume  Muhammad  (s.a.w.w) aliishi nao  vizuri  akiwa katika Mji wa Makkah  na  madina, na kuwekeana  nao  Makubaliano  ya  kuishi  kwa  Amani.”  Alisistiza kuwa tunayo haki  ya  kuwaambia  ndugu  zetu   wakristo  kuwa  tupo  pamoja  katika  sikukuu  hii  ya  kuzaliwa  kwa  Nabii  Issa  as,  (Yesu).

alianisha wazi na kusema…”kwa kuwa  sisi ni Watanzania  na  wadau  wa Amani, Tunaamini  vikao  kama hivi vinajenga  na  kuimarisha  umoja  baina yetu  na  mshikamano kwa  viongozi  wa  dini  na  waumini  kwa ujumla,

Mwisho Mawlana Hemedi jalala alimuomba Mwenyezi Mungu Aibariki  Tanzania, Mungu  Ibariki Afrika, na  viongozi  wake Mungu  awatie  nguvu na  afya  njema  katika  kuwahudumia  wananchi  wao,

Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kwenu wote.

 

photo_2015-12-23_17-41-05

Mawlana Hemedi Jalala (Kushoto) akiwa na Sheikh Mohamed Abdi (Kulia) katika hafla na waandishi wa Habari

photo_2015-12-23_17-43-26

photo_2015-12-23_17-43-10

Picha ya baadhi ya Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria katika Hafla.

photo_2015-12-23_17-43-03photo_2015-12-23_17-42-54

 

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on December 23, 2015, in Habari na Matukio, Matukio, Uncategorized and tagged , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: