UISLAMU HAUNA MAHUSIANO NA UGAIDI

12523044_809855422457788_7440510980672091577_nNeno ugaidi limekuwa likitumika na kusikika mara nyingi sana kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine, Ni neno linaloashiria hatari  pindi linaposikika au linaponasibishwa na mahali au sehemu, Katika akili kinachopita cha mwanzo ni fikra juu ya uuaji na umwagaji damu dhidi ya watu wengine kwa saDSC02385babu zozote zile,ila muhimu katika mazungumzo yetu si kuendeleza hofu hii na kuikuza bila kuieleza asili na machimbuko yake, Kwani kutokufanya hivyo kutawafanya watu waendelee kuelewa ndivyo sivyo na mwisho watahukumu batili na kuifanya haki kwa kuwa tu batili imesemwa sana bila kumpata anaeipinga na kuonyesha mbadala au asili halisi, Ninayasema haya kutokana na hali ya mambo ilivyo duniani kwani leo hii mtu anaweza kuvamia kanisa na shule katika moja ya majimbo ya marekani na kuua watu wasio na hatia kisha akachukuliwa kwenda kuchunguzwa akili na mwisho tendo lile likawa ni jinai ya kawaida kwa kuwa aliyefanya ni mzungu mweupe ,katika jimbo la wa marekani weusi wenyeasili ya afrika,Lakini ikatokea mtoto wa kiislamu mwenye umri wa miaka kumi na mbili (12) mwenye asili ya Afrika akatengeneza saa kwa ubunifu mkubwa na kwenda nayo shule kisha haraka tu akakamatwa na polisi kwa staili na namna anavyokamatwa muhalifu kwa kuwa mwalimu amedhani kilichobebwa na mtoto  huyo   ni bomu ambalo alitaka kulipua nalo shule na kufanya tukio la kigaidi, Hivyo ninatumia nafasi kutahadharisha watu kutolitumia hili neno kirahisi tu bila uchunguzi kwani neno gaidi au ugaidi limeshatumika mara nyingi tu ili kukandamiza watu wa dini au rangi Fulani. Tunatahadharisha hili kwa kuwa TUNAPINGA UGAIDI WA AINA ZOTE, lakini tunaamini kutumika vibaya hili neno na kunasibishwa kibaguzi kwa makundi Fulani kunaweza kuzalisha UGAIDI WA KIFIKRA ambao utawatafuna wasio na Hatia wala makosa.

Ugaidi ni ufisadi na uharibifu dhidi ya ubinadamu, unamdhuru binadamu katika Nyanja nyingi sana lakini ya msingi hasa
ni Nyanja ya ubinadamu wake kwanza, binadamu huyu kupitia ugaidi anakatisha maisha ya wengine bila sababu za msingi wala bila kuwa anaeuliwa amemuua binadamu mwingine au nafsi kwa dhuluma. Hapa athari ya kwanza ni binadamu kupoteza ule utu wake na ubinadamu mpaka kumpelekea kuweza kuinua mkono kumuua mtu ambae ni asili yake, ambae ni binadamu mwenzake, tukio hili hata mnyama pori halifanyi kwa mnyama mwingine mwenye asili sawa na yeye, ana nini binadamu wa sasa hata aweze kulifanya hili? Binadamu huyu bila shaka  amepoteza kitu kinachoitwa maadili, pamoja na kuwa amepiga hatua kubwa katika maendeleo ya kimaada, amefikia hatua ya kuongea na kumuona wa mashariki na magharibi yake, ameweza kubuni kipando cha kasi kabisa kinachombeba mpaka anga za juu na kukata masafa mengi ndani ya muda mchache lakini maendeleo ya ndani, maendeleo ya kibinadamu ,kitabia na kimaadili yanarudi nyuma kwa kasi kubwa sana isiyofanana na kasi yake ya nje anayoenda nayo katika kufikia maendeleo ya kimaada.

Binadamu ameoyesha umahiri mkubwa katika kutenda na kuzalisha vifaa na teknoloji kubwa duniani, hii inaonyesha uwezo wa akili kubwa aliyopewa na Mungu,lakini ninawaambieni maadili na adabu ndio shina la akili, bila maadili au adabu hakuna akili, ndipo unapoona akili ambayo ilikosa maadili ilitengeneza Bomu la atom na kuwaua binadamu wasiokua na hatia wala wasio na silaha hata ndogo ya kujikinga na kujihami, takwimu zinaonyesha vifo vilivyosababishwa na bomu hilo katika mji wa heroshima ni zaidi ya 150,000 na kwa mji wa nagasaki ni zaidi ya watu 75,000, idadi hii si ile halisi kutokana na hali ya tukio, inaweza ikazidi maradufu. Maafa haya ambayo kimsingi ni ugaidi mkubwa yalitokea kwa sababu ya kukosekana kwa maadili na adabu katika mipango na utekelezaji, kwa kuwa adabu ni shina la akili basi akili ilikosa shina na hivyo haikuwepo na ndipo yakatokea yaliyotokea. Tunamshukuru mungu kwa kuwa tukio hili halikufanywa na waislamu kwa maana dunia ya leo muislamu angelikosa pa kukanyaga kwa sababu kimsingi Ugaidi unatumika pia kama propaganda dhidi ya waislamu na ndipo UNAONA TUKIO KAMA HILI LA  HEROSHIMA NA NAGASAKI si katika matukio yanayotajwa kuwa ni matukio ya kigaidi kwa kuwa hayakufanywa na waislam, na huo ni ugaidi wa fikra tuliouzungumza mwanzo.Kimsingi ugaidi dhidi ya ubinadamu umeanza siku nyingi lakini hausemwi, nikiisoma historia nakutana na matukio mengi ya kutisha, miaka ya 1788 wakati uingereza wakiwa wamevamia maeneo ya watu wa australia waliwaua watu sehemu hizo kwa dhambi ya weusi wa ngozi yao watu hawa (aborigines) wanaripotiwa kuwa mpaka mwaka 1920 walikuwa washauawawa zaidi ya 60,000, hii ni aibu kubwa sana kwa ubinadamu na ni ugaidi kinamna yeyote ile. Ugaidi ni kitu kibaya sana na ni lazima upingwe kwa hali yeyote ile bila kujali anaeifanya.12573216_809855915791072_5298203784998549535_n DSC02365 DSC02374

Hatuwezi kuzungumzia ugaidi na athari zake bila kuizungumza hali ya mashariki ya kati, mashariki ya kati katika Arabia ambayo imetapakaa damu na mauaji, ugaidi wa kutisha unaotengenezwa kwa makusudi na mataifa pamoja na mashirika makubwa kwa malengo ya kuuza silaha unafanya jinai kubwa dhidi ya ubinadamu, huku wengine wasiojielewa wakisema wanachokipigania ni kusimamisha dini, Isis (Daesh), Jabhatu Nusra na makundi mengine yanayotekeleza jinai kubwa sana ambayo kimsingi tunatoa matamko ya kupinga moja kwa moja na kwamba wanachokifanya sii uislam. Ninapoizungumza mashariki ya kati siwezi kuiacha Palestine ambayo ubinadamu unavunjwa na haki za msingi hazitolewi, itashangaza kama nitaiacha Iraqi inayochemka damu kwa udhalimu na ugaidi wa makundi yanayojinasibisha na uislam, hatuwezi kuisahau Syria ambayo imezalisha wakimbizi wengi wanaokwenda ulaya utadDSC02392hani ni china inazalisha bidhaa kuja Afrika, yote haya ni madhara na athari za ugaidi kwa binadamu na ubinadamu, leo watu wameyakosa makazi yao, wametapanyika na kusambaratika kwa familia zao na hawana mwelekeo.Lakini katika mashariki ya kati hii ambayo sarakasi zote dhidi ya ubinadamu zinafanywa tunaikuta Saudia yenye utawala wa kibabe dhidi ya raia imeamua kufanya mauaji makubwa ya kikatili dhidi ya watu wasiokua na silaha zaidi ya sauti zao za kudai haki zao za msingi, kuwaua watu zaidi ya 47 akiwemo sheikh Nimri Baqir Nimri ni jinai kubwa na ni utekelezaji wa hukumu dhalimu ambayo haikuwahi kufanywa na wafalme waliopita tangu miaka ya 1980,ndani ya mashariki ya kati hii ukidai haki unafungwa, ukiongea unachinjwa na hata ikiwa ni nchi jirani wanakujia na mabomu kuja kuharibu nchi na raia, je ni kwa gharama kiasi gani saudia imenunua ukimya wa dunia dhidi ya jinai zake pale anakwenda kuishambulia yemen na watu wake ili amuweke raisi anaedai ni raisi kwa mujibu wa demokrasia hali kwake hakuna demokrasia? na haki ndogo tu dhidi ya mwanamke haziheshimiwi mpaka wakafikia kumnyima mwanamke uhuru wa kuendesha gari?Bahrain nao hivyohivyo raia hawana amani, nini Tatizo lililowakumba? Kuna haja ya kukaa chini na kuanza kufundisha na kurejesha maadili, adabu ndio shina la akili, akili bila adabu ni sawa na mbuzi aliyekata kamba na anajiendea atakavyo kokote atakapo.

KWA KUMALIZIA ZIFUATAZO NI ATHARI AMBAZO ZIMEPATIKANA KUTOKANA NA UGAIDI KATIKA MAENEO MENGI:

Mbali na maafa na uharibifu wa mazingira tunaweza kuzigawa hizi athari katika makundi matatu yafuatayo:

  1. ATHARI ZA KIFIKRA
  2. Athari za kifikra katika kukufurishana

Kuitana majina mabaya kwa sababu eti Yule hakati suruali kama mimi au kutikisa kidole cha shahada, Anasoma khitma na maulidi na hivyo ukampa jina la kafiri au mtu wa bidaa ili kuhalalisha damu yake.

  1. Kupotea kwa fikra za uislamu halisi

Makundi haya ya kitakfiri na kigaidi yanamalengo ya kupoteza fikra za uislamu halisi, uislamu wa rahma, leo hii ukisimama kwenye ndege ukasema kwa nguvu Allahu Akbar watu wanaweza kutaka kujirusha kwa kuwa ni neno linalotumika wakati wa kujilipua na kuchinja wasiokuwa na hatia.

  1. Kupoteza uislamu wa kimaadili

Kwa mfululizo wa matukio kibao yanayofanywa na wanaojinasibisha na uislamu ni dhahiri ya kuwa moja ya athari zake ni kupotea kwa maadili ya huruma na kuhurumiana ambao ndio msingi wa uislamu kama maana ya jina lenyewe.

  1. Kuufanya umoja baina ya waislamu ni swala gumu lisilowezekana

Umoja baina ya waislamu ndio silaha pekee ya ushindi, adui analijua hilo ndipo utaona mapandikizi katika uislamu yalivyo mengi ili kuhakikisha umoja huu haufikiwi. Njia inafanywa ngumu kwa kuwa kuna watu kwa makusudi wanatengenezwa kutukana maswahaba na wengine kukufurisha wengine.

  1. Athari za kutokubali mwingine.

Athari hii tunaiona Afrika ya kati Anti Baraka wanavyouwa watu, tunaiona Iraqi wanavyouliwa waislamu wa madhehebu zote, tunaiona Burmer jinsi waislamu wanavyouwawa na mabudha, Ugaidi hauna dini wala kabila, lazima tuukemee.

  1. Kupotea kwa uislamu unaolingania amani

Utampata muislamu anamchinja muislamu, wengine watalipiza na wengine wataanza kuhisi kuuana ndio dini,

  1. ATHARI ZA KIVITENDO

Moja ya athari za kivitendo katika kutokumkubali mwingine zinaweza kudhihirika katika maeneo yote ambayo matukio ya kigaidi yamewahi kufanyika, kwanzia Afrika tumeona kutokuwakubali wengine kumewafanya makundi ya wakiristo chini ya Anti-baraka kuwauwa waislamu kwa msingi wa kutovumiliana na kumkubalia anaetofautiana na wewe. Tumeona  wakiristo (Aqbat) wenye asili ya misri walivyouawa huko Libyaa. Saudia Arabia nayo imeshindwa kumsikiliza mwananchi na kiongozi wa kidini, imekandamiza uhuru wa kusema na ikafikia kumuua Sheikh Nimri na serikali ya Nigeria kumkamata Sheikh Zakzakiy. Pia tumeshuhudia makanisa na misikiti ya mashia na wasiokuwa mashia ilivyoshambuliwa huko mashariki ya kati, yote haya yanaonyesha hatari ya ugaidi.

  • ATHARI ZA KIUHARIBIFU

Ugaidi umekua ni chachu ya kuvunja na kuharibu turathi, umekua ni chanzo kikuu cha kufuta au kuharibu kumbukumbu za kihistoria mfano Somalia walivunja makaburi ya mawalii,Syria makaburi na makumbusho za kihistoria zimekua zikishambuliwa, na Iraqi nako ni zaidi si makaburi tu bali hata makanisa na misikiti ya karne nyingi, pamoja na hivyo hata makaburi ya mitume hayako salama  .

Imehaririwa na kitengo cha Habari,

Asadiq Media, Hawzat Imam Swadiq a.s

Email: asadiqmedia@gmail.com

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on February 8, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: