KUMBUKUMBU YA MAZAZI YA BIBI FATIMA 2016

BISMIHI TAALA.

BI FATMA NI KIELELEZO CHA NGUVU YA MWANAMKE.

Tunapomzungumzia Bi Fatima a.s tunamzungumzia mwanamke ambae ni kioo cha kiwiliwili ambacho si wanawake tu wanaweza kujitazama na kurekebisha tabia na maadili yao, bali hata mamia ya wanaume wengi mbali ya mitume na manabii wa Mungu. Huyu ni mtoto wa Mtume Muhammad s.aw.w, mtume wa uislamu ambae alitumwa kuja kufundisha maadili, tabia njema, upendo na mahusiano mema baina ya binadamu wa rangi na dini zote. Mwanamke huyu alilelewa katika nyumba bora miongoni mwa nyumba bora kabisa kuwahi kutokea katika mgongo wa dunia hii, nyumba ambayo ilichomoza duru iliyomfunza binadamu utu na ubidamu kamili, nuru ambayo ilimkataza Muarabu wa zama zile kuua mtoto wa kike kama ilivyokua ada yao, nuru iliyomuekea mipaka binadamu huyo na kumkataza vita zilizoshamiri na kuwa sehemu ya maisha yao,. Nguvu ya nuru hii iliangazia dunia na kuacha athari kubwa duniani na hadi hivi sasa wakawepo watu kila kona ya dunia wanaoweza kujinasibisha na uislamu wa Muhammad. Yote haya ni kwa sababu tabia njema ndio nguzo ya Uislamu na mpaka mtume mwenyewe anatuambiwa ametumwa kuja kukamilisha Tabia njema na kwamba dini ni maisha mema baina yako na jamii.ZAHRAA

Katika kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Fatima a.s mwaka huu, tunasherehekea kwa kutuma ujumbe katika jamii ya watanzania na dunia nzima juu ya nguvu na heshima ya  mwanamke katika uislamu na kutoa wito kwa watu wote wajifunze kutoka kwa binti huyu wa mtume, Bibi Fatima ambae ukisoma historia yake utampata kuwa ni kielelezo cha nguvu ya mwanamke. Nguvu hii inaakisi uwezo na utashi ambao wanaume wengi duniani hawakuwahi kuwa nao, hiki kinasimama kama kielelezo kinachothibitisha swala la uwezo, utashi, uwezo wa kuhudumia jamii na utambuzi wa mambo katika Nyanja mbalimbali haupimwi katika kigezo cha jinsia, na ikiwa utataka kutumia jinsia kama kigezo basi utapata Bibi Fatima a.s ni kielelezo cha nguvu ya mwanamke ambayo kamwe haina mfano.

Tunapomkumbuka bibi Fatima a.s hatumkumbuki kwa nafasi yake ya heshima aliyopewa ndani ya uislam pekee, bali tunamkumbuka kama mmoja wa walimu,  ambae historia ya maisha yake imejaa mafunzo yanayohitajiwa mno na jamii ya sasa, jamii ya sasa iliyopoteza muelekeo katika swala zima la maadili na malezi ya watoto na familia inamuhitaji mwanamke huyu aliyeweza kuwalea moja ya vijana bora katika ulimwengu, Hassan na Hussein a.s, vijana ambao walifundishwa kumhudumia wa kando na jirani kwanza kabla ya kuhudumia wa ndani, vijana ambao walikua ni nembo ya elimu na utu mpaka Hussein akaweza kuandika historia ya mapinduzi makubwa iliandikwa damu yake pale alipoona heshima na utu vinapigwa teke.

Tunamkumbuka mwanamke ambae alikuwa muasisi wa mfumo wa kiuchumi kwaajili ya kusaidia maskini wasiojiweza,mayatima na wajane kupitia shamba alilopewa na baba yake kama zawadi enzi za uhai wake, tunamkumbuka mwanamke ambae alikua akishughulishwa na matatizo ya jamii na kila mara alikua akiendea kwa kasi na shauku isiyoelezeka matatizo ya watu ili kuyatatua. Ni mwanamke ambae anatufunza malezi ya jamii na kututoa katika gereza la umimi na ubinafsi, lau kama ulimwengu wa leo ungemuiga katika kujitolewa na kujali maslahi ya binadamu basi tungeshi katika dunia ambayo haina maskini anaeomba wala yatima anaelala njaa kwa sababu kungekua na mgawanyo mzuri wa rasilimali, na tusingepata mafisadi wanaojilimbikizia mali hali wengine wanalala njaa.

Tunapomzungumzia Bibi Fatima tunamzungumzia mwanamke ambae aliishi ndani ya mipaka yake kama mke, mama na mlezi wa nyumba iliyokua mithili ya chuo kikubwa sana kilichotumika kufunza maadili na ukarimu, nyumba ambayo ilikua ikitoa chakula chake kwa sababu yatima amefika mlangoni, mara nyingine mateka akiwa amekuja kuomba na mara nyingine maskini akiwa amejisogeza katika mlango wa mwanamke bora huku akiwasilisha shida zake, tunamzungumzia mwanamke anayefunza huruma na kujitoa kwaajili ya wengine hata kama itakugharimu kushinda na njaa au kutoa vitu vya thamani, Bibi Fatima ni mfano wa kujitolea ambae hakuwahi kumrudisha muombaji hata katika siku ambayo aliombwa nguo ambayo ilitakiwa kutumika siku ya kesho katika harusi yake.

Tunamzungumzia mwanamke ambae alikua mama si kwa watoto zake tu bali hata kwa baba yake, Mtume Muhammad, mtume wa uislamu hakuwahi kuyajua mapenzi ya mama wala baba yake, alifiwa akiwa mdogo kabisa, lakini Fatima aliishi na kumlea baba yake mara tu baada ya kifo cha mama yake mpaka baba yake akasema “Fatima ni mama ya baba yake”. Kimsingi wasichana na wanawake wa zama hizi wakiweza kuiga mwenendo huu hatutapata vituo vya kulea wazee na watu wazima waliotekelezwa. Zahraa ni kielelezo cha nguvu ya mwanamke ambae lau atafananishwa na wanaume basi utampata hafanani na mtu yeyote katika wanaume na lau angekua mwanaume basi angekua miongoni mwa manabii.

Kwa upande wa uislamu tunamzungumzia mwanamke ambae mola wake anamuita ni kheri na neema nyingi alizopewa mtume wa uislam, ni kheri na neema kwa sababu mola muumba ameamua kuwa kizazi kitukufu cha utume na uongozi kitaendelezwa na Bibi Fatima a.s, hivyo watoto wa Bibi Fatima Zahraa a.s wanaunganishwa kwenye kizazi cha mtukufu mtume kupitia mama yao kama ilivyo mtume Issa a.s asiye na baba alivyounganishwa katika kizazi cha mtume Ibrahim a.s kupitia mama yake mtukufu Mariam bint Imran. kuendeleza kizazi hiki ni kukamilisha ndoto za manabii kwa kuwa kizazi chake ni kizazi cha uongozi na viongozi hawa ndio walinzi wa sheria za Allah. Kupitia Bibi Fatima a.s tunapata mtu atakaedhihiri mwisho wa dunia, mtu ambae hata kama dunia itakua imebaki saa moja ili iishe basi Allah atalirefusha saa moja hilo ili adhihiri mtu kutoka katika nyumba ya utume, katika kizazi cha Fatima ambae jina lake ni jina la mtume na sifa zake ni sifa za mtume, ataijaza dunia uadilifu kama ilivyojazwa na kuenezwa uovu, dhuluma haitokua na nafasi tena katika jamii ya wanaadam. Hivyo ndoto za mitume za kuona dunia ya Amani, maelewana na uadilifu wa kimungu inasimama itatimia kupitia mtu huyu, Imam Mahdi mwana wa Fatima Zahraa a.s. Ndoto hii inakamilika kupitia mwanamke huyu, na hapa ndipo inapodhihirika nguvu ya kiungu kupitia mwanamke huyu mteule.

Tunaposherehekea mazazi ya mwanamke huyu mwalimu wa maadili duniani, tunamaanisha kujivua na kila aina ya kiburi, tunajivua na utii wa asiyekua Allah, mungu anaefunza tabia njema aliyemuumba mwanamke kama huyu anafunza kukataa kila nguvu zinazozalisha mapigano na machafuko katika dunia, Tunaposherehekea mazazi ya mwanamke huyu tunajiweka katika nafasi ya kujisafisha kutokana na ukandamizaji, unyonyaji na ufisadi dhidi ya ubinadamu. Maana yake tunapinga kila jinai zinazofanyiwa binadamu kutokana na matukio ya kigaidi na vita zenye maslahi na ubepari.

Tunasherehekea mazazi ya bibi Fatima a.s ili kupaza sauti zetu katika jamii ya watanzania juu ya kuheshimu na kujali haki za wanawake, tunatoa ujumbe kutoka hapa kwetu Tanzania na usambae duniani kote juu kutaka kusitishwe unyanyasaji wa wanawake na ukatili dhidi yao. Si hivyo tu, bali tunakataa kudhalilishwa mwanamke hata kwa njia ya picha ambazo zinamuonyesha mwili wake kinyume na maadili, tunasema mwanamke anathamani kubwa Zaidi ya ile anayodhihirishiwa katika ulimwengu wa sasa unaomfanya kama mtangazaji wa bidhaa kupitia mwili wake, ajabu ya mambo ni imefikia hata katika mafuta ya kula anaweza kuwekwa mwanamke ili kuwavutia wanunuzi, tunawaambia mwanamke ni mlezi na kioo na si chombo cha starehe na kifaa cha matangazo.

Mwisho tunatoa wito kwa wanawake wa zama hizi kusimama katika nafasi zao, kusimama katika nafasi zao kama wanawake, kutimiza majukumu yao na hasa katika swala la malezi ya watoto na familia kwani wao wana nguvu yenye taathira kubwa sana katika jamii yote kwani wao ndio walezi wakuu wa jamii.

Tunatoa mkono wa hongera kwa mtukufu mtume Muhammad s.a.w.w kwa mazazi ya binti yake wa pekee kama tunavyotuma salamu za hongera kwa imam wa zama zetu Imam Alhujja Almahdi A.F. Salamu za pongezi pia zimuendee kiongozi wa waislamu duniani Sayyid Ali Khamenei pamoja na Marajii na wanazuoni wote wa kiislam.

 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI,

ASADIQ MEDIA, HAWZAT IMAM SWADIQ (A.S)

Web: https:// imamswadiq.com/

YouTube: youtube.com/asadiqmedia

Fb: https://www.facebook.com/SheikhHemediJalala/

 

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 29, 2016, in Hotuba na Mawaidha. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: